Viongozi wa dini wapokelewa na vilio Nyamongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wapokelewa na vilio Nyamongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Jul 20, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  VIONGOZI wa dini nchini na wenzao kutoka nje ya nchi, wamekutana na kilio kikubwa kutoka kwa wakazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Nyamongo unaomilikiwa na African Barrick North Mara, vinavyotokana na dhuluma waliyofanyiwa kuhusu fidia.

  Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Kanisa Katoliki Tabora, Paulo Ruzoka na makamu wake, Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Fereji, ilikuwa na lengo la kuona hali ilivyo na jinsi ya kuhakikisha amani inatawala.

  Mbele ya viongozi hao, Petro Naftari, kutoka Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) Nyamongo, alisema uamuzi wa wananchi kutoa maeneo inakochimbwa dhahabu kwa wawekezaji, matokeo yake ni vifungo na vifo.Naftari alisema hali ambayo imepelekea tatizo hilo kuwa ukubwa na hakuna uhusiano mzuri kati yao na wawekezaji, huku gharama kubwa zikielekezwa kujilinda badala ya kusaidia wananchi.

  “Mimi nilifanyiwa tathmini, lakini nilikaa kwa mwaka mmoja kisha nikalipwa nyumba moja Sh50,000, hivi kweli kwa hali hiyomtu anaweza asirudi mgodini kutafuta mawe kweli?" alihoji Naftari kwa uchungu.

  Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanasaidia kuunganisha wananchi na mwekezaji, kwa sababu hata wawekezaji wakijenga ukuta siyo suluhisho. Marwa Sasi, mkazi wa Kewanja, alisema hata matokeo ya sumu kwenye vyanzo vya maji yamecheleweshwa kutolewa kwa miaka miwili, lakini baada ya kusikia viongozi wa dini wamefika wakatoa kuwa hakuna sumu, bali ni madini ambayo yako ndani ya miamba.

  “Kwa miaka miwili kweli wanachunguza sumu, ambayo wanadai hakuna madhara kwa binadamu! hii inawezekanaje? naomba viongozi wa dini muweze kutusaidia kudai haki zetu maana serikali inawasiliza zaidi ninyi," alisema Sasi.

  Anthony Kyaro, mkazi wa Nyamongo, alisema licha ya mgodi kutoa ahadi hewa ikiwamo ujenzi wa hospitali ya hadhi uliishia kukarabati ili iliyojengwa na wananchi, ambayo haina umeme, maji na vifaa.

  Mwenyekiti wa Kitongoji cha Lamboni, Mgoye Mgoye, alisema kinachofanywa na kampuni ni usanii kwa kuwapiga picha au kuchora ramani kwa helkopita bila kushirikisha wananchi.Mwenyekiti wa Kitongoji cha Senta, Juma Marura, alisema watu Waliopa madhara kutokana na maji ya mto Tigithe, wanatakiwa kupata fidia na wale wanaomiliki maeneo yenye ukubwa wa ekari 672 hawajalipwa.

  Akizungumza na wananchi hao, Askofu Ruzoka alisema tatizo la Nyamongo litamalizwa na pande zinazohusika kukaa pamoja na kwamba, watalifikisha suala hilo ngazi husika.Askofu Ruzoka alisema kutokana na ugumu wa kuingia ndani ya mgodi huo, wanajipanga kutafuta kibali ili kukutana na uongozi wa wawekezaji hao wanavyojipanga kumalizika tatizo hilo.Awali, Mkuu wa wilaya hiyo, John Henjewelle, alitumia muda mwingi kueleza kamati hiyo ubaya wa watu wa Nyamongo bila kugusa uongozi wa mgodi.

   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii ndiyo Tz!
   
Loading...