Viongozi wa dini wanaodai kuponya ukimwi kukamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wanaodai kuponya ukimwi kukamatwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Dec 7, 2009.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Suzy Butondo, Shinyanga

  SERIKALI mkoani Shinyanga imetangaza kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini wanaowapotosha waumini wao kwa kusema kuwa wanaponya ugonjwa wa ukimwi.

  Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika viwanja vya Shycom manispaa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Amina Masenza alisema kuna baadhi ya viongozi wa dini na waganga wa jadi wanawapotosha na kuahidi wakibainika watachukuliwa hatua.

  Mkuu huyo wa wilaya alisema kiongozi yeyote wa dini atakayebainika anawapotosha wananchi atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kwani hali hiyo inachangia kuongezeka kasi ya maabukizi ya ugonjwa huo.

  Alisema mbali na viongozi wa dini pia kuna waganga wa jadi ambao kazi yao ni kuwarubuni wananchi kwa kuwaeleza kuwa wanazodawa za kutibu ukimwi wakati ni uongo mkubwa na kwamba hadi leo dawa ya kuponya ugonjwa huo haijapatikana huku akiwataka wananchi kutokubali kurubuniwa na kwamba hao ni matapeli.

  Aliwataka wazazi kuvunja ukimya na kukaa na watoto wao na kuwaeleza athari za ugonjwa wa ukimwi badala ya kuwaacha waendelee kuangamia huku akisisitiza kuwa tiba ya VVU bado haijapatikana.

  Katika risala iliyosomwa na mmoja wa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga, Mathias Chidama ilisema kuanzia kipindi cha Julai hadi Septemba mwaka huu, watu 13,847 walijitokeza kupima VVU kati yao wanaume walikuwa 6,924 na wanawake 6,923 na waliokutwa wameathirika ni 1,113.

  Ilisema maambukizi ya VVU katika manispaa hiyo, ni asilimia 7.7 ambapo kati ya idadi ya watu waliopima na kukutwa na vvu na kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo ARV ni 3,381 sawa na asilimia 41.
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuna tofauti gani kati ya viongozi wa dini wanaodai kuponya ukimwi kwa maombi, na wale wanaodai kufanya hivyo kwa ugonjwa wa malaria na magonjwa mengine?

  Kama hatua hizi zitatokana na sababu za kisayansi, hakuna kiongozi wa kidini anayeweza kuthibitisha kwamba anaweza kufanya "faith healing" kwa hiyo it is absurd kwamba wame limit hii effort kwenye ukimwi.
   
Loading...