Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini wamtuliza Dk Slaa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Saint Ivuga, Nov 8, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,912
  Trophy Points: 280
  Monday, 08 November 2010 01:07 0diggsdigg

  [​IMG] Dk Willbrod Slaa

  Salim Said
  JOPO la viongozi wa dini limefanya ziara ya ghafla kwa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Wiilibrod Slaa na kumtaka akubali matokeo au atumie njia za kisheria kudai haki yake, Mwananchi imebaini.

  Dk Slaa hakutokea kwenye hafla ya kutangaza mshindi wa kiti cha urais wala sherehe za kuapishwa kwa Jakaya Kikwete kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano na aliahidi kuwa angetoa tamko zito jana.

  Wakati Tume ya Uchaguzi (Nec) ikiendelea kutangaza matokeo, Dk Slaa aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kueleza kuwa hangekubaliana na matokeo kutokana na kubaini kuwa Nec ilikuwa inatangaza matokeo tofauti na yaliyo kwenye nyaraka walizosaini na hivyo kuitaka isitishe zoezi hilo ili kura zianza kuhesabiwa upya.

  Dk Slaa pia aliituhumu Idara ya Usalama wa Taifa kuwa ilihusika kuchakachua kura kwa lengo la kumbeba mgombea mmoja wa urais, tuhuma ambazo ziliifanya taasisi hiyo, inayofanya kazi kwa siri, ijitokeze hadharani kujibu na kumuelezea katibu huyo mkuu wa Chadema kuwa "ni mzushi".

  Tamko hilo la Dk Slaa lilionekana kuwashutua viongozi wa dini na kuhisi dalili za kutokea mvutano ambao ungeweza kusababisha kuvunjika kwa amani. Mwananchi imebaini kuwa ziara ya kimya kimya ya viongozi hao wa dini ilifanywa wiki iliyopita kabla ya Nec kumtangaza Kikwete kuwa ni mshindi.

  Kwa mujibu wa habari zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kwamba viongozi hao walimtaka Dk Slaa asisababisha mvutano ili kudumisha amani ya nchi. Habari za ziara hiyo ya dharura ya jopo hilo la viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu zilithibitishwa na meneja wa kampeni wa Chadema, Profesa Mwesiga Baregu. Profesa Baregu aliiambia Mwananchi kuwa ujumbe mkubwa uliofikishwa na jopo hilo ulikuwa ni kuwaomba viongozi wa Chadema kutumia njia sahihi za kudai haki yao ambazo hazitazusha vurugu, fujo wala uvunjifu wowote wa amani.

  "Ujumbe wao kwetu ulikuwa ni kutuomba kwamba kusiwe na vurugu, fujo wala uvunjifu wowote wa amani wakati wa kutangazwa matokeo na hata baada ya kutangazwa," alisema Profesa Baregu. "Badala yake wakatuomba kama hatujaridhika na matokeo basi tutumie taratibu za kisheria zilizowekwa kudai haki. Lakini sisi tuliwaeleza kuwa hatuna nia ya kufanya vurugu wala kuandamana, lakini uchaguzi umevurugwa na hatuwezi kukubali."

  Alisema jopo la viongozi hao wanne wa dini wakiongozwa na askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa lilifanya ziara hiyo baada ya Chadema kuitaka Nec kusitisha utangazaji wa matokeo kwa kuwa Usalama wa Taifa wamechakachua matokeo.

  "Sijui walikuwa na wasiwasi gani au nani aliwashauri kuja tena kuonana na viongozi wa Chadema, lakini nadhani ni baada ya kuona tumesema hatungekubali matokeo kwa kuwa uchaguzi umechafuliwa," alisema Profesa Baregu. Alisema pamoja na wasiwasi huo wa viongozi wa dini, Chadema haikuwa na mpango wowote wa kuunganisha nguvu ya umma na kuingia barabarani, kama ilivyofanyika Kenya, kudai haki. "Lakini hatujaridhika na matokeo kwa sababu uchaguzi ulikuwa mchafu.

  Rais amechaguliwa na robo tu ya wapigakura. Nec imeongeza majina kwa sababu kabla ya uchaguzi ilisema wapigakura wote ni 19.9 milioni, lakini akitangaza mshindi Jaji Lewis Makame anasema ni 20.1, hatujui wametoka wapi," alisema Profesa Baregu. Kwa mujibu wa Baregu wengine waliokuwamo katika msafara huo wa viongozi wa dini walikuwa ni kutoka Kanisa Katoliki na Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata).

  Dk Slaa, ambaye alishika nafasi ya pili kwenye kinyang'anyiro cha urais kwa kupata asilimia 26 ya kura, pia alitembelewa na jopo la viongozi wa dini kabla ya kumalizika kwa kampeni wakimtaka awe tayari kupokea matokeo yoyote yale. Jopo hilo lilidai wakati huo kuwa lingetembelea wagombea wengine wa urais, lakini halikufanya tena ziara kwa wagombea wengine hadi uchaguzi ulipofanyika.
  chanzo:mwananchi
   
 2. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa viongozi wa dini ni mamluki wa CCM. Kwanini wameshupalia kumsihi Dr Slaa ayatambue matokeo ya wizi? Kwanini wao wasiilaani kwanza NEC kwa kuvuruga uchaguzi? Inamaana hawajui haki ya wananchi ilivyoporwa? Hawajui kuwa mbali na CCM kulazimisha Kikwete kurudi ikulu, wagombea ubunge wengi wa CHADEMA wameporwa ushindi kama vile Karagwe, Shinyanga, Tarime, Mbeya vijijini, Kigoma mjini, Kilombero, Segerea kwa kutaja tu baadhi? Ni wa puuzi tu hawa! Wametumwa na CCM. Nilitegemea waseme kuhusu hii NEC ya CCM isivyofanya kazi kwa haki, uhuru na usawa badala ya kusema tu CHADEMA wakubali matokeo!!
   
 3. v

  vickitah Senior Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 18, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viongozi wa dini muda mrefu wamekuwa wametumika kulinda viongozi walioko madarakani.. tunasema wanamaintain the status quo' ndo mana the famous Karl Marx once said "religion is an opium of the people" ila mi nadhani tatizo sio dini ila ni jinsi watu tunavyojaribu kuitumia dini.. Nadhani viongozi wa dini wajue na wao kuna siku tutawashukia kwa ufisadi wanaoufanya (baadhi yao) ila kwa sasa watuache kwanza tuwatoe mafisad papa wanaoisumbua hii nchi.. Amani haiwezi kuletwa kwa kuongea na Dr Slaa wakati wananchi wamechoka kuishi kwenye umaskini, matokeo ya uchaguz pia yanachakachuliwa' watuache kwanza kwa sasa wasubiri j2 tutakuja kusali na kutubu.
   
 4. DCONSCIOUS

  DCONSCIOUS JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,272
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ningewaona wamaana endapo wange wafwata viongoze wa ccm kuwaomba watubu kwa mungu kutokana na zambi wailiyo ifanya.
   
 5. T

  Tanzania Senior Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mhumiri wa Amani ni Haki. Period
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,355
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Sawasawa! Nakubaliana na wewe! Kosa lolote lile linatengeneza laana flani,so wasipotubu wao litatengeneza maafa mbalimbali, so si jambo la zuri kufurahia ushindi uliotokana na matendo machafu ambalo limesheheni wingi wa madhambi!
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kiongozi makini hasa wa kidini lazima apoze viongozi walioathirika na mfumo kandamizi lakini vilevile lazima akemee waziwazi upande unaoonekana kutumia mbinu chafu. Sijaona kiongozi yeyote wa kidini si wakikristo wala kiislam aliyekemea hadharani vitendo viovu vilivyovuruga uchaguzi. Viongozi tubadilike pasipo kufanya hivyo, heshima yenu mbele ya jamii itapungua kama siyo kwisha kabisa.
   
 8. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndo ushangae,ila ninavyo amini mimi jamaa aliingia kila idara kumuunga mkono
   
 9. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nawashangaa hawa viongozi wa dini badala ya kukemea mwizi aache kuiba ili kutosababisha vurugu wao wanampoza aliyeibiwa wakati keshapata hasara halafu yule mwizi haambiwi chochote ili aendelee kuiba. Tunawaheshimu sana ila wajue kwamba wao ni viongozi wa dini sio viongozi wa kura za watu! Kama wako fair na hawajatumwa nawaomba watoe na tamko kukemea uchakachuaji wa kura sio waegemee upande mmoja..
   
 10. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nawashangaa hawa viongozi wa dini badala ya kukemea mwizi aache kuiba ili kutosababisha vurugu wao wanampoza aliyeibiwa wakati keshapata hasara halafu yule mwizi haambiwi chochote ili aendelee kuiba. Tunawaheshimu sana ila wajue kwamba wao ni viongozi wa dini sio viongozi wa kura za watu! Kama wako fair na hawajatumwa nawaomba watoe na tamko kukemea uchakachuaji wa kura sio waegemee upande mmoja..
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,648
  Likes Received: 4,754
  Trophy Points: 280
  Hawa viongozi wa dini ni wanafiki wakubwa na wanajipendekeza sana kwa JK hasa viongozi wa Kikristo.Viongozi hawa hasa maskofu na wachungaji wanakuwa kimya kukemea ufisadi uliovuka mipaka unaofanywa na viongozi wa Serikali ya CCM, nchi inaporwa usiku na mchana rasilimali zake kwa msaada wa viongozi waliopo madarakani kwa njia ya mikataba mibovu isiyozingatia maslahi ya nchi, yote haya yanafanyika viongozi wa dini wako kimya , sana sana wako beneti na mafisadi hao kuwaalika kwenye harambee za makanisa yao, huu ni unafiki. Viongozi hao wa dini wana kazi moja tu wanyojua kuifanya ya kuwafundisha waumini wao masomo ya utoaji sadaka na mafungu ya kumi ili wajineemeshe huku waumini wao hao hali zao za uchumi zikizidi kudorora kutokana ufisadi unaofanywa na watawala. Ningewaona wa maana kama wangeanza kwa kukemea wizi wa kura uliofanywa na NEC ili kumpa JK ushindi haramu, wizi wowote ule ni dhambi, iweje dunia nzima imeona wizi huu na kuukemea lakini viongozi wa Kanisa katika Tanzania wameshindwa kuuona. Wao walichoona na kuamini ni uwongo ulitungwa na JK kuwa Dr Slaa anataka kuanza vurugu na o wakaitia upuuzi huu wa JK na kwenda kumsihi Dr Slaa akubali na kubariki wizi wa kura ili kudumisha amani Tanzania , huu ni unafiki. TANZANIA HAKUNA AMANI BALI WATANZANIA NI WAOGA KUDAI HAKI YAO HIVYO MTU ANAYEKUWA JASIRI KUDAI HAKI HIYO HUONEKANA MVUNJIFU WA AMANI. HUU NI UWONGO WA JK KULINDA WIZI WAKE WA KURA. WACHUNGAJI NA MAASKOFU ANZENI KUKEMEA WIZI WA KURA KWANI HIKI NDIYO CHANZO CHA VURUGU. Nakumbuka hata wakati wa vita ya Kagera, Mwalimu alikataa suala suluhu na kuwataka wanaohubiri suluhu waanze kumkemea Idd Amin kwa uvamizi aliofanya kwenye ardhi yetu.
   
Loading...