the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
Jana Jumatano Machi 02, 2022 Viongozi wetu wa Dini walikutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya nae mazungumzo mbalimbali pale Ikulu.

Katika hali iliyonishangaza Mimi na nadhani hata kwa Watanzania wengine wengi ni hatua ya Viongozi wa Dini kuomba Rais Samia na Mamlaka zake zitumie busara kumaliza kesi iliyoko mahakamani ya tuhuma ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe na wenzake.

Binafsi nimeshangaa na kushtushwa na ajenda hii ya Viongozi wa Dini kwa Mkuu wa Nchi kwasababu kila mmoja anafahamu kwamba kesi ya Mbowe kwasasa iko mahakamani na tayali ushahidi wa pande za mashtaka na utetezi zimeanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo, sasa kitendo cha Viongozi wetu wa Dini kutaka Rais atumie busara kumaliza kesi hiyo na ikiwezekana akina Mbowe waachiwe huru sijui inatoka wapi na kwa sheria ipi? Nimeshtuka.

Kesi hii iko mahakamani lakini kwa maajabu mazito ama kwa makusudi ama kwa kutojua ama kwa mtego, Viongozi wetu wa Dini wanataka Mamlaka iingilie kazi ya mahakama na kuipoka na badala yake itumie busara kumaliza kesi. Busara, so what?

Mimi nadhani tungeiachia mahakama ifanye kazi yake kwasababu hakuna sheria ya Mamlaka au Rais kuingilia masuala ya mahakama. Tuiachie mahakama ifanye shughuli yake na kama Mbowe si Gaidi ama Gaidi basi mahakama baada ya uchunguzi kukamilika na ushahidi wote kutolewa itasema na kumaliza kesi hii lakini sio habari hii ya kutaka Rais au Mamlaka ziingilie Uhuru wa mahakama, hii si sawa kabisa.

Nchi hii haiendeshwi kwa busara wala huruma ya mtu bali inaendeshwa kwa sheria na taratibu ambazo ziko wazi kwenye Katiba na sheria zetu zingine. Tukiruhusu hivi, hii haitakuwa nchi na kama ni hivyo basi hiyo busara na huruma isitumike kwa Mbowe tu, bali itumike kwa watuhumiwa wote walioko mahabusu na kwenye mahakama zetu hizi, kama ishu ni busara na huruma. Busara hii ya kutaka kupoka kazi ya mahakama na kumaliza kesi kibusara na kihuruma basi isiombwe kwa Mbowe tu, iombwe kwa wengine wote watuhumiwa.

Hapa kwa akili ya kawaida tu panatengezwa mazingira ya kumwingiza Rais au mamlaka zake kwenye chaka zito sana halafu kesho na keshokutwa busara na huruma inatumika halafu hao hao waomba busara na Wanaharakati wengine ndo wanakuwa wa kwanza kupiga kelele kwenye Club House au Spaces kwamba mahakama na mifumo yetu ya sheria inaingiliwa. Hii si sawa. Rais Samia asikubali kuingizwa kwenye hili boko la kuvunja na kukanyaga sheria. Aiachie mahakama ifanye kazi yake. Hiyo busara na huruma anayoombwa leo itamchafua na kumletea shida nchini na hata kwenye Mataifa mbalimbali huko mbele, asikubali. Full stop

Mimi nadhani tuheshimu sheria zetu na tumshauri Rais Samia masuala mengine mengi tu ya ujenzi wa Taifa letu na kumueleza changamoto zingine nyingi tu zilizopo kwa Wananchi na kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu lakini sio hii ya kumshauri Mkuu wa Nchi kuingilia kazi na uhuru wa mahakama, chombo huru kabisa.

Niwe mkweli, Viongozi wa Dini nawaheshimu sana sana sana lakini kwenye hili, wamenikwaza sana sana sana sana.

Pia, soma: Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe
 
Mimi sijasoma gazeti lako lote, lakini unauliza rais amalize hiyo kesi kwa sheria ipi?! Ile kesi wote tunajua ni ya mchongo, na kosa kubwa la Mbowe siyo ugaidi! Kosa la Mbowe ni kuwa mpinzani wa kweli na kudai katiba mpya!

Pia, kama hujui kusoma between the lines, viongozi wa dini, kwa maneno mengine wanamwambia Mazaa, wanauona mchongo wote, watu wanaona kwamba yupo uchi, achutame!
 
Linganisha hizi dots.
1. Rais samia akihojiwa na BBC akakiri kuwa kweli mbowe alitenda ugaidi.
2. Mbowe akakamatwa, kesi ikaanza kuunguruma.
2.Judge siyani akapokea maelezo ya Watuhumiwa kinyume na sheria, hapa ndipo kesi ilipotengenezwa, katikati ya kesi Kikaandaliwa kikao cha vyama vya siasa, moja ya ajenda ilikuwa ni mbowe asamehewe
3.. Mbowe akaambiwa aombe msamaha ili atoke gerezani lakini akagoma kuomba msamaha.
3. Judge Tiganga akatumia amri zake kupokea ushahidi akamtia mbowe na wenzake hatiani.
4. DPP akaanza kufuta kesi nyingi za ugaidi.
5. Viongozi wa dini wakaitwa ikulu, na clip iliyotolewa na ikulu ni viongozi hao wa dini wakiomba mbowe aachiwe.

Kwa hizo step huwezi kujua nini kinafanyika??? kumbuka katika uongozi wae mama Samia, doa kubwa kabisa alilonalo ni kumshitaki kiongozi wa chama kikubwa cha siasa kwa kesi ya ugaidi.
 
Jana Jumatano Machi 02, 2022 Viongozi wetu wa Dini walikutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya nae mazungumzo mbalimbali pale Ikulu.

Katika hali iliyonishangaza Mimi na nadhani hata kwa Watanzania wengine wengi ni hatua ya Viongozi wa Dini kuomba Rais Samia na Mamlaka zake zitumie busara kumaliza kesi iliyoko mahakamani ya tuhuma ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe na wenzake.

Binafsi nimeshangaa na kushtushwa na ajenda hii ya Viongozi wa Dini kwa Mkuu wa Nchi kwasababu kila mmoja anafahamu kwamba kesi ya Mbowe kwasasa iko mahakamani na tayali ushahidi wa pande za mashtaka na utetezi zimeanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo, sasa kitendo cha Viongozi wetu wa Dini kutaka Rais atumie busara kumaliza kesi hiyo na ikiwezekana akina Mbowe waachiwe huru sijui inatoka wapi na kwa sheria ipi? Nimeshtuka.

Kesi hii iko mahakamani lakini kwa maajabu mazito ama kwa makusudi ama kwa kutojua ama kwa mtego, Viongozi wetu wa Dini wanataka Mamlaka iingilie kazi ya mahakama na kuipoka na badala yake itumie busara kumaliza kesi. Busara, so what?

Mimi nadhani tungeiachia mahakama ifanye kazi yake kwasababu hakuna sheria ya Mamlaka au Rais kuingilia masuala ya mahakama. Tuiachie mahakama ifanye shughuli yake na kama Mbowe si Gaidi ama Gaidi basi mahakama baada ya uchunguzi kukamilika na ushahidi wote kutolewa itasema na kumaliza kesi hii lakini sio habari hii ya kutaka Rais au Mamlaka ziingilie Uhuru wa mahakama, hii si sawa kabisa.

Nchi hii haiendeshwi kwa busara wala huruma ya mtu bali inaendeshwa kwa sheria na taratibu ambazo ziko wazi kwenye Katiba na sheria zetu zingine. Tukiruhusu hivi, hii haitakuwa nchi na kama ni hivyo basi hiyo busara na huruma isitumike kwa Mbowe tu, bali itumike kwa watuhumiwa wote walioko mahabusu na kwenye mahakama zetu hizi, kama ishu ni busara na huruma. Busara hii ya kutaka kupoka kazi ya mahakama na kumaliza kesi kibusara na kihuruma basi isiombwe kwa Mbowe tu, iombwe kwa wengine wote watuhumiwa.

Hapa kwa akili ya kawaida tu panatengezwa mazingira ya kumwingiza Rais au mamlaka zake kwenye chaka zito sana halafu kesho na keshokutwa busara na huruma inatumika halafu hao hao waomba busara na Wanaharakati wengine ndo wanakuwa wa kwanza kupiga kelele kwenye Club House au Spaces kwamba mahakama na mifumo yetu ya sheria inaingiliwa. Hii si sawa. Rais Samia asikubali kuingizwa kwenye hili boko la kuvunja na kukanyaga sheria. Aiachie mahakama ifanye kazi yake. Hiyo busara na huruma anayoombwa leo itamchafua na kumletea shida nchini na hata kwenye Mataifa mbalimbali huko mbele, asikubali. Full stop

Mimi nadhani tuheshimu sheria zetu na tumshauri Rais Samia masuala mengine mengi tu ya ujenzi wa Taifa letu na kumueleza changamoto zingine nyingi tu zilizopo kwa Wananchi na kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu lakini sio hii ya kumshauri Mkuu wa Nchi kuingilia kazi na uhuru wa mahakama, chombo huru kabisa.

Niwe mkweli, Viongozi wa Dini nawaheshimu sana sana sana lakini kwenye hili, wamenikwaza sana sana sana sana.

View attachment 2137091
View attachment 2137093
View attachment 2137094

Pia, soma: Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe
Viongozi wa dini ni jukumu lao kushauri pale wanapoona upendo ktk jamii unamong'onyoka, visasi na uonevu vinatamalaki, na laana inakaa ktk jamii,
 
Tangu Mwendazake aasisi kuwa Sifa Kuu ya lazima ili kuteuliwa kwenye Teuzi hapa Tanzania, kwamba ni lazima Kumuumiza Freeman Mbowe! Hakuna mtu au Jaji wa hapa Tanzania ambaye atapata nafasi ya Kumuumiza Freeman Mbowe atakosea shabaha ya Kumuumiza Freeman Mbowe. Tanzania bado tunaenzi Legacy ya Jiwe.
Yaani ni hovyo sn
 
Katika hali iliyonishangaza Mimi na nadhani hata kwa Watanzania wengine wengi ni hatua ya Viongozi wa Dini kuomba Rais Samia na Mamlaka zake zitumie busara kumaliza kesi iliyoko mahakamani ya tuhuma ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe na wenzake.
Usishangae. Viongozi wa dini wanatoa meseji kwa rais Samia kwamba yeye ndiye kambambikia kesi mhe Mbowe. Na hivyo aachane na huo ujinga (upumbavu).
 
Jana Jumatano Machi 02, 2022 Viongozi wetu wa Dini walikutana na Rais Samia Suluhu Hassan na kufanya nae mazungumzo mbalimbali pale Ikulu.

Katika hali iliyonishangaza Mimi na nadhani hata kwa Watanzania wengine wengi ni hatua ya Viongozi wa Dini kuomba Rais Samia na Mamlaka zake zitumie busara kumaliza kesi iliyoko mahakamani ya tuhuma ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe na wenzake.

Binafsi nimeshangaa na kushtushwa na ajenda hii ya Viongozi wa Dini kwa Mkuu wa Nchi kwasababu kila mmoja anafahamu kwamba kesi ya Mbowe kwasasa iko mahakamani na tayali ushahidi wa pande za mashtaka na utetezi zimeanza kutoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo, sasa kitendo cha Viongozi wetu wa Dini kutaka Rais atumie busara kumaliza kesi hiyo na ikiwezekana akina Mbowe waachiwe huru sijui inatoka wapi na kwa sheria ipi? Nimeshtuka.

Kesi hii iko mahakamani lakini kwa maajabu mazito ama kwa makusudi ama kwa kutojua ama kwa mtego, Viongozi wetu wa Dini wanataka Mamlaka iingilie kazi ya mahakama na kuipoka na badala yake itumie busara kumaliza kesi. Busara, so what?

Mimi nadhani tungeiachia mahakama ifanye kazi yake kwasababu hakuna sheria ya Mamlaka au Rais kuingilia masuala ya mahakama. Tuiachie mahakama ifanye shughuli yake na kama Mbowe si Gaidi ama Gaidi basi mahakama baada ya uchunguzi kukamilika na ushahidi wote kutolewa itasema na kumaliza kesi hii lakini sio habari hii ya kutaka Rais au Mamlaka ziingilie Uhuru wa mahakama, hii si sawa kabisa.

Nchi hii haiendeshwi kwa busara wala huruma ya mtu bali inaendeshwa kwa sheria na taratibu ambazo ziko wazi kwenye Katiba na sheria zetu zingine. Tukiruhusu hivi, hii haitakuwa nchi na kama ni hivyo basi hiyo busara na huruma isitumike kwa Mbowe tu, bali itumike kwa watuhumiwa wote walioko mahabusu na kwenye mahakama zetu hizi, kama ishu ni busara na huruma. Busara hii ya kutaka kupoka kazi ya mahakama na kumaliza kesi kibusara na kihuruma basi isiombwe kwa Mbowe tu, iombwe kwa wengine wote watuhumiwa.

Hapa kwa akili ya kawaida tu panatengezwa mazingira ya kumwingiza Rais au mamlaka zake kwenye chaka zito sana halafu kesho na keshokutwa busara na huruma inatumika halafu hao hao waomba busara na Wanaharakati wengine ndo wanakuwa wa kwanza kupiga kelele kwenye Club House au Spaces kwamba mahakama na mifumo yetu ya sheria inaingiliwa. Hii si sawa. Rais Samia asikubali kuingizwa kwenye hili boko la kuvunja na kukanyaga sheria. Aiachie mahakama ifanye kazi yake. Hiyo busara na huruma anayoombwa leo itamchafua na kumletea shida nchini na hata kwenye Mataifa mbalimbali huko mbele, asikubali. Full stop

Mimi nadhani tuheshimu sheria zetu na tumshauri Rais Samia masuala mengine mengi tu ya ujenzi wa Taifa letu na kumueleza changamoto zingine nyingi tu zilizopo kwa Wananchi na kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu lakini sio hii ya kumshauri Mkuu wa Nchi kuingilia kazi na uhuru wa mahakama, chombo huru kabisa.

Niwe mkweli, Viongozi wa Dini nawaheshimu sana sana sana lakini kwenye hili, wamenikwaza sana sana sana sana.

View attachment 2137091
View attachment 2137093
View attachment 2137094

Pia, soma: Viongozi wa dini waliokutana Rais Samia Wamemshauri kuifuta kesi ya Mbowe
Mjinga mmoja.

Nikuambie tu sasa hyo ni mipango ya ikulu kufanya hivyo. Na soon ataachiwa ila ilikua lazima itumike mbinu hii kuonyesha kwamba mama amesikia ombi la viongozi wa dini na hatoshupaza shingo yake.
 
Kama hajui, kampaisha chati sana mh Mbowe kisiasa huko upinzani.
Asubiri kulinywa.
 
Kalime MATOBOLWA...
 
Ngoja kwanza; kesi ulikua unaifatilia hasa wale mashahidi walivyokua wanautoa ushahidi wao? Kama hukufatilia then achana na kutoa comments zako cause hujui kilicho kua kinaendelea mahakamani na kama uliifatilia, je unatazama mambo kwa jicho la HAKI au la ki ccm? Sina hakika kama kuna Mtanzania mwenye akili timamu kabisa, asiependa uonezi anaweza kufikiria kwamba Mbowe anaweza kua na kesi ya kujibu pale, achilia mbali issue ya yeye kua GAIDI!?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom