Viongozi wa dini walivyoshiriki kwenye biashara za udanganyifu kwa macho makavu na bila haya

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,721
Ni ule mlolongo wa tiba mbadala ulioibuka enzi za JK... Hapa namtoa kwenye orodha babu wa loliondo kwakuwa yeye hakujitangaza, hakupigia debe dawa yake na malipo yake hayakubadilika iwe kwa masikini, tajiri, viongozi ama watu maarufu.. Kwakwe alichaji mia tano tuu... Na ilikuwa ni lazima kikombe chenye dawa akupe mwenyewe... Hakubagua wala kuchagua wa kumpa... Kwakwe wote walikuwa sawa... Na katika hiyo mia tano... Yeye alichukua mia mbili tuu.. Mia tatu iliyobaki ikaenda kwa wasaidizi wake.... Ni nani mwingine angeweza kufanya hivi?

Tiba hii ya babu wa loliondo ilifungua fursa mpya kwa viongozi wengine wa kidini... Waliona yale mafuriko ya Loliondo, wakaichangamkia fursa.... Zikaanza kumiminika clinic zinazosimamiwa na wanaojiita viongozi wa kidini... Ama clinic hizo matangazo yake kusindikizwa na nyimbo za kidini.... Kumbuka si kwenye ukristo tuu bali na uislam pia... Tiba kwa njia ya visomo zilipamba moto... Wengi wakitumia mitishamba, tibalishe na vidonge vitokanavyo na mitishamba, majani na vyakula vya asili...

Huduma za hospital na vituo vya afya kidogo zililemaa... Matangazo ya kuvutia kuhusiana na tibalishe ama tibambadala huku yakisindikizwa na ala laini za nyimbo za kidini viliwavuta wengi... Kuanzia viongozi mbalimbali mpaka watu maarufu...

Kurasini pale kwenye kituo kimoja cha redio ya kidini walipigia debe mno ile tiba ya kunyonywa sumu mwilini kupitia beseni la maji... Yani ukifika pale huduma hiyo moja ililipiwa viwango tofauti kulingana na hadhi yako... Bei ilikuwa kati ya elfu 30 mpaka laki mbili... Basi ukishafanya malipo unaingizwa kwenye chumba chenye viti na mabeseni yenye maji... Hayo mabeseni ya maji kazi yake ilikuwa kuloweka miguu kimashine kikishatumbukizwa... Basi dakika chache baadae ukitoa miguu maji yote yanakuwa yamegeuka rangi na Kuwait kama maji yenye kutu nyingi na hapo unakuwa tayari umeshapata tiba...
Shuhuda zilikuwa nyingi kupitia matangazo ya mitandaoni na kwenye vyombo vya habari...
Vituo vya namna hii viliendelea kufunguliwa chini ya umiliki wa viongozi wa kidini, kukawa kuna mpaka vimashine vya kuchua mwili na misuli vya kichina...

Leo hii sizisikii tena zile tiba na waliotumia wengi ni marehemu huku waanzilishi na wamiliki wakiwa wameshapiga pesa ndefu na kupata misingi ya kufanya uwekezaji mwingine....!!!!

 
.
04.jpeg
Image066-1.jpeg
2.jpeg
 
 
 
Kiukweli viongozi wa dini wamekuwa ndyo matapeli namba moja, kwa maisha ya sasa heri ukutane na jambazi kuliko hao wanaojiita watumishi wa Mungu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom