Viongozi wa dini wakiri kuhusika na dawa za kulevya

Source?
Kama ni kweli hakuna haja ya kuficha
.
Hawa kwanza ni kuwataja, pili,ni kukamatwa na kuchukuliwa hatua

Mbona hata mkuu wa kaya mwaka 2005 alisema ana orodha yote ya watu wanaohusika na bishara hii haramu ,lakini mpaka leo hatujaona wala hawo watu kutajwa.

siasa za bong bana
 
jaman dunia hii inakwenda wap? Viongoz wa dini wanauza madawa? Mungu wangu kwel tutaadhibiwa kama sodoma na gomola
 
Hao viongozi wanapaswa kwanza kujiuzulu nafasi zao kwani tayari wameshapoteza mwelekeo. Pili wachukuliwe hatua za kisheria baada ya kutajwa hadharani. Sioni ni vipi tutashinda vita ya madawa kwa kufichana namna hii. Serikali ilishasema itaonyesha mkanda wa video wa watu hao...hilo silipongezi kwani kwa nini wasionyeshe kwa wananchi baada ya kuwa wameshawakamata watuhumiwa hao? Kama mchezo ni huu basi sioni ni vipi vita hii itawezekana. Mkuu wa nchi alishawahi kupewa orodha ya wauza unga, akaificha Ikulu kisha analalamika. Simuelewi na silielewi jeshi la polisi na mtu yeyote atakeyewaficha watu hawa.
 
Jamani mbona muna hangaika na hii thread? Huyu Anayejiita Mchungaji William Mwamalanga si mchungaji Kama anavyojiita bali ni tapeli tu. Vyombo vya habari haviko makini katika kufuatilia CV za watu controversial kama hawa
 
tusipokuwa wawazi hatutaweza asilani kuwajibika na eventually kuiendeleza nchi. kuna sababu gani ya kulificha hili? Hili ni kosa la jinai. Sio tu watajwe, bali washitakiwe. au hili nalo linaingia kwenye yale maamuzi magumu yaliyoshindikana kufanyika? sasa hata jinai za wazi hivi haziwezi chukuliwa hatua, uongozi huu unaweza chukua maamuzi gani?
 
Nina uhakika kuwa kati ya wote waliochangia Thread hii hawamjui William Mwamalanga. Kama kuna mtu anamfahamu atuambie je William Mwamalanga ni mchungaji wa kanisa gani? Nani alimtawaza kuwa mchungaji? Waumini wake wako wapi?Ukijibu maswali haya ndiyo utabaini Kama kweli hiyo kamati ipo, na hao viongozi wa makanisa wapo. Mimi ninachojua nikwamba huyu ni tapeli tu na ame fabricate taarifa hizo na ndiyo maana wachangiaji wanahangaika sana kuhusu hayo majina

Viongozi wa dini zipi waliokutana? Kama ni hao wachungaji wa kujipa sishangai.

Ni lazima watu watambue tofauti kati ya Makanisa mama na madhehebu ya dini. Roman sio dhehebu. Madhehebu ni kama ya akina Kakobe, Mwamalanga , Upako mbali mbali akiwemo Geo Dave etc. Wengi wao ni matapeli , kwa hiyo kujiingiza humo sishangai kama yule Mnigeria tuliyeambiwa na kamanada .
 
Mimi sielewi hapa kuna kitu gani kinachotaka kutengenezwa, kwanza kiongozi wa nchi alitaja juu juu tu na kuwaeleza kuwa viongozi hao wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya. Baadhi ya viongozi hao walikuja juu na kutoa masaa 48 kuwa awataje. Mpaka leo zimepita sijui wiki ngapi hajataja. Leo gazetinalo linakuja na kichwa cha habari ambacho hakina kiwiliwili wala miguu na mikono. Hizi zawezakuwa habari za kutengenezwa kama ni kweli Polisi waliopewa kazi hii watoe habari ama umma hawatawelewa na kazi yao.
 
kichwa cha habari kizuri then ndani hamna hata jina?..siasa uchwara hizi
umesema kweli ndugu, habari isiyo na majina.aah! habari Siku hizi. Kanisa yapo wapi? Na madhehebu gani? Na majina yao hatutaki usanii wa habari hata anayetoa habari awe wazi kama ana habari
 
Halafu Kikwete aliposema watu walimbeza. Kinachomponza sana Kikwete ni kuwa mwana diplomasia, nadhani baada ya wachache kulalama akawaita hawa viongozi na kuwaambia huyu na huyu na huyu wanahusika na tukianza kuyaweka wazi tutayumbisha dhehebu zima sasa amueni wenyewe. Mtalishughulikia au mtataka bado sisi tushughulikie tunavyojua? Hapo sasa.

Ahsante Kikwete.
 
hakuna lolote,hii serikali ni ya kisanii,wanakaa wanaona waibuke na habari gani mpya ambayo itawafanya wadanganyika wasahau kile kitu cha msingi,wanachopigia kelele kwa wakati huo(tatizo la umeme)ili wa2utoe kwenye mstari,kwa sasa hatudanganyiki.kwa m2u mwenye akili timamu haiwezi kukuingia akilini eti wameomba wasitajwe majina!kweli hili ni shamba la bibi.
 
Yaaaani Wakati wanatoa hii ripoti ilitakiwa hao wahusika wawe kunakostahili yaani rumande. otherwise wamewapa muda wa kujisafisha na kupanga jinsi ya kujisafisha.

Sasa si jamii inazidi kupeka kete. lol
 
Ndiyo maana tunaona Makanisa mengi yanajengwa, shule nyingi za St. zinajengwa; kumbe sasa tunapata ukweli wa hizo hela zinapotoka. Sasa sijui kwa nini hizo shule zao bado zinaitwa Saint!!?
 
Ama kweli mtoto wa ******* hata ukimtia kwenye chupa atatoa kidole nje.
 
Back
Top Bottom