Viongozi wa dini wakiri kuhusika na dawa za kulevya

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
Viongozi wa Dini Wakiri Kuhusika Na Dawa za Kulevya


Viongozi sita wa madhehebu ya dini wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.

Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa baada ya kuhojiwa, Viongozi hao waliiomba Kamati hiyo kutowataja hadharani majina ama madhehebu yao kwa kuhofia kubezwa kwa madhehebu wanayoyaongoza.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yao Visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, amesema kuwa orodha hiyo na nyingine ya watu 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na Wanasiasa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu zote zitafikishwa kwa Mkuu wa kitengo cha Polisi cha Kupambana na dawa za kulevya nchi.

Mchungaji Mwamalanga amesema kuwa, tatizo la ongezeko la dawa za kulevya pia inazihusu nchi mbalimbali duniani na kwamba kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kwa maana ya Afrika ya Mashariki kuzungumzia ufumbuzi wa suala hilo.

Amesema mkutano huo pia utapendekeza kwa mabunge ya nchi hizo na Bunge la Afrika ya Mashariki kutunga sheria za kuwafilisi wale wote waliojilimbikizia mali kutokana na biasha za dawa za kulevya kwa nchi wanachama.
 
Hao viongozi wa dini wanaojihusisha madawa ya kulevya wachukuliwe hatua za kisheria maana wanachokifanya ni chukizo kwa mwenyezi mungu na wanaharibu kabisa jamii yetu.
 
Mwenye
kudhulumu na azidi kudhulumu;
na mwenye uchafu na azidi
kuwa mchafu; na mwenye haki
na azidi kufanya haki; na
mtakatifu na azidi kutakaswa.
(Soma Ufunuo wa Yohana
22:11)
 
Utakuwa ni ujinga lazma watajwe na wajulikane wasitake kuleta janja ya kuendelea kuwadanganya wa'tz wenzetu na mapepo na majini wanayowapndkizia.
 
Watajwe majina hakuna cha kuwaficha wala nn, kama wao wameamua kuliangamiza taifa kwa tamaa zao kwann wastajwe hadharani na wakamatwe. ntaishangaa Serikali ikileta uwendawazimu wake wa kuwasamehe kisa wamejisalimisha wenyewe kama watu wa EPA! HAKUNA CHA KUWAFICHA HAPA, HATA HAO WANA SIASA WATAJWE ILI WAJIUZURU NYAZIFA ZAO KWANZA ILI WASHITAKIWE VIZURI. WASHENZI TENA WAUAJI WAKUBWA!
 
wawataje mimi siamini kama kuna hata mmoja kutoka kanisa katoliki au lutheran au anglican au sabato au pentecoste siamini....tutakuja sikia ni madhehebu ya kinaijeria
 
Vyama vya upinzani shinikiza watajwe watanzania wawajue kama ni madhehebu ya hapa nchini tuchukue tahadhali sisi waumini na viongozi wetu na kuwaonya waumini wao wawe macho na viongozi wao
 
Deal jingine la kama ya EPA laja.
Hii ni kutokana na kiongozi mkuu wa nchi kuwa dhaifu kiasi cha kusukumia mbali utawala wa sheria na kuendekeza maridhiano ya kisiri na wahalifu.
NDIO MAANA KATIKA KIPINDI CHA UTAWALA WA JK, TANZANIA IMEGEUZWA KITUO KIKUU KTK UKANDA WA AFRICA KUPITISHIA MADAWA YA KULEVYA.

.
 
Sasa kunafaida gani kuwaficah majina yao? Au ni mkakati wa kuimarisha hoja ya Kikwete?
 
wawataje mimi siamini kama kuna hata mmoja kutoka kanisa katoliki au lutheran au anglican au sabato au pentecoste siamini....tutakuja sikia ni madhehebu ya kinaijeria

Kweli sasa watu hawatumii hata matumbo kufikiri, sasa naona wameanza kutumia Nyeti kufikiri. Kama ni kweli kwanini wasiwakamate na kuwafikisha mahakamani badala ya kuja kutuletea mchezo wa kuigiza hapa! Ina maana leo hii mtu akijitokeza akisema mimi ni muuaji, hawa Magamba wasio na akili watakuja kutuambia kwamba kuna watu kumi wamekiri kwamba ni wauaji au watawakamata na kuwafikisha mahakamani! Sasa ni nini kinachowazuia wasiwafikishe mahakamani kama hii sio fiction!

Hizi habari zinapaswa ziwe zinaandikwa kwenye KIU, IJUMAA, JAMBO LEO, RISASI, SANI, AMANI, UWAZI au ANNUR na si magazeti tunayoyaweka kwenye kundi la magazeti serious.
 
Hizi siasa mfu,haina maana ya kutamba kwa kazi ambayo hujamaliza
wamalize huo uchunguzi uchwara ndo wawapandishe kizimbani
............bla blaa za sirikali kujisafisha...........
 
Source?
Kama ni kweli hakuna haja ya kuficha
.
Hawa kwanza ni kuwataja, pili,ni kukamatwa na kuchukuliwa hatua
 
Ingawa hii habari imeandikwa na karibia vyombo vyote vya habari vya leo, nahisi bado ni maigizo flanni tu hivi; kuna vitu ambavyo havihitaji sana akili kubaini hayo; mfano; walipataje ujasiri wa kujitokeza mbele ya hio tume/kamati ya maadili na ku-declare? wanasema kulikua na prior uchunguzi.....well kama kulikuwa na uchunguzi sasa kwa nini wasitaje hayo majina? Pengine hatuajahiyaji, sawa, basi kwanini wasipelekwe mahakamani? Was it so necessary tuuifahamu habari hiii au muhimi kwetu ilikuwa ni wao wapelekwe mahakamani? Hata hivyo, sijawahi ona mwizi aka-declare wizi wake in such simple statements; nimefurahi kidogo japo inaonekana ni hadithi flani hivi kwamba wamekimbilia kwenda kutangazia huko visiwani maana walijua mziki wake huku ungekuaje....is way of trying to neutralize the upcomimg impact...
 
Hii mambo ya kuficha ficha hii inapalilia rushwa!
Kwanini wasitajwe na wao si watu wazuri?
Au wametoa rushwa?
 
Hii mambo ya kuficha ficha hii inapalilia rushwa!Kwanini wasitajwe na wao si watu wazuri?Au wametoa rushwa?
Nina uhakika kuwa kati ya wote waliochangia Thread hii hawamjui William Mwamalanga. Kama kuna mtu anamfahamu atuambie je William Mwamalanga ni mchungaji wa kanisa gani? Nani alimtawaza kuwa mchungaji? Waumini wake wako wapi?Ukijibu maswali haya ndiyo utabaini Kama kweli hiyo kamati ipo, na hao viongozi wa makanisa wapo. Mimi ninachojua nikwamba huyu ni tapeli tu na ame fabricate taarifa hizo na ndiyo maana wachangiaji wanahangaika sana kuhusu hayo majina
 
Back
Top Bottom