Viongozi wa Dini tusaidieni kupambana na Rushwa, Ufisadi - Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa Dini tusaidieni kupambana na Rushwa, Ufisadi - Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maxence Melo, Jun 4, 2009.

 1. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  VIONGOZI WA DINI TUSAIDIENI KUPAMBANA NA RUSHWA, UFISADI - PINDA

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewaomba viongozi wa dini nchini waweke mkazo katika kuisadia Serikali kupambana na mmomonyoko wa maadili miongoni mwa jamii jambo ambalo amesema limesababisha kuwepo vitendo viovu kama rushwa na ufisadi.

  Ametoa ombi hilo leo asubuhi (Alhamisi, Juni 4, 2009) wakati akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwenye ukumbi wa Mikutano wa CCT/CTC mjini Dodoma.

  Akizungumza na maaskofu na viongozi wa jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema wao kama viongozi wa kiroho wana wajibu wa kusaidiana na Serikali kulionya kundi kubwa la waumini wao linalojumuisha watumishi wa umma na viongozi mbalimbali.

  “Ninawaomba tuweke mwelekeo wetu katika kuisaidia Serikali kupambana na maovu haya ili viongozi na watumishi wa umma ambao ni waumini wenu washiriki kupunguza kero za wananchi wanaowaongoza… ninyi ni sehemu ya uongozi na pia ni sehemu ya jamii, tafadhali sana msiwe watazamaji,” alisema.

  Alisema ukosefu wa maadili miongoni mwa watumishi wa umma na viongozi kwa kiasi kikubwa hautokani na kiwango kidogo cha elimu bali unasababishwa zaidi na hulka za watu na tabia ya watu wachache kutaka kutumia fursa zinazojitokeza kujinufaisha wao binafsi.

  Alisema mada kuu ya Mkutano huo: “Changamoto za Serikali katika kuimarisha Maadili ya Viongozi na Watumishi wa Umma” imekuja kwa wakati muafaka kwani Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali ili kuboresha utendaji kazi wake.

  “Tunapozungumzia kuimarisha maadili ni dhahiri kwamba maadili yamemomonyoka. Kwa lugha nyingine, hayapo katika kiwango chake na hivyo yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili yaendane na kile kilichotarajiwa,” na kuongeza kwamba walichotarajia maaskofu hao na viongozi wa jumuiya hiyo ni kusikia jinsi Serikali inavyoziona changamoto zilizojitokeza kuhusu maadili ya viongozi na watumishi wa umma na hatua zinazochukuliwa ili kukidhi matarajio ya wananchi.

  Alisema kwa mujibu wa Taarifa ya Utafiti kuhusu Maadili katika Utumishi wa Umma (Ethics Baseline Opinion Survey of Stakeholders) ya mwaka 2006 uliohusisha watu 734, ilibainika kuwa vitendo vya ukosefu wa maadili vipo zaidi katika maeneo ya Ucheleweshaji wa utoaji huduma kwa asilimia 84; Upendeleo asilimia 49; Mienendo mibaya asilimia 63; Ubinafsi katika kazi asilimia 67; Rushwa asilimia 61; Vitendo vya Jinai (Wizi, uporaji) asilimia 38; na Matumizi mabaya ya madaraka asilimia 52.

  “Walipoulizwa ni hatua zipi zinapaswa kuchukuliwa ili kupambana na vitendo vya ukosefu wa maadili, kati ya watu hao 734 waliofanyiwa utafiti, asilimia 81 walitaka hatua za kinidhamu na kisheria zichukuliwe dhidi ya watumishi walioonyesha upungufu wa Maadili,” alisema Waziri Mkuu.

  Akifafanua zaidi, Waziri Mkuu alisema, asilimia 80 walitaka kuongezwa uelewa juu ya umuhimu wa maadili miongoni mwa watumishi na asilimia 77 walitaka kuanzishwe mijadala ya kimaadili. Asilimia 72 walitaka maslahi ya watumishi yaboreshwe, asilimia 71 walitaka yaendeshwe mafunzo kwa watumishi kuhusu maadili na asilimia 69 walitaka kuwe na usimamizi imara wa watumishi. Vilevile, walitaka kuwepo na mifumo ya kuwasikiliza wateja.

  Waziri Mkuu alisema tafiti hizo zinaonyesha dhahiri kwamba, wananchi wanajua kwamba yapo matatizo ya ukosefu wa maadili na wangependa hatua kadhaa zichukuliwe ili kukabiliana na vitendo hivyo.

  Alisema ili kuongeza uwajibikaji na usikivu kwa umma (responsiveness), mwaka 2007 Serikali kupitia Mpango wa Uboreshaji wa Umma, ilianzisha utaratibu wa kushughulikia malalamiko ya wananchi kwa kufanya majaribio katika taasisi saba kwa miezi mitatu na baadaye taasisi hizo zilianza kutekeleza mfumo huo.

  Alizitaja taasisi zinazotekeleza mfumo huo mpaka sasa kuwa ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii; Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Hospitali ya Amana (Wilaya ya Ilala) na Manispaa ya Ilala.

  Alisema mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa taasisi zote za umma zinaanzisha mfumo huu kuanzia mwaka ujao wa fedha.

  Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es Salaam leo mchana ili kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu ya CCM.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, JUNI 4, 2009
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Huko nako kuna ufisadi wa kutisha ambao unaanzia kutokufanya wanayoyaamini na kuyahubiri! sawa kabisa na wanasiasa wanaosema na kuzungumzia rushwa kwa maneno hili hali wanauwezo wa kuchukua hatua mmoja wa wanasiasa hao ni wewe Pinda.
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  labda mafisadi waombewa dua baya na waumini wa dini zote au vipi?
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Swali: Je endapo akina Pengo na Malasusa wakibarikiwa kupata courage ya kuwataja akina RA na wenzake kuwa ni mafisadi papa nao pia wataitwa kwenye vyombo vya dola kujieleza?
   
 5. p

  popo Member

  #5
  Jun 13, 2009
  Joined: Aug 30, 2008
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is completely Rubbish.hawa Viongozi wa siasa hawana akili hata kidogo Viongozi wa dini wakikemea kuhusu rushwa na hali mbaya ya nchi wanaambiwa wasichanganye Dini na Siasa, sasa leo anawaomba Viongozi wa Dini wasaidia wanasiasa wasiwaibie watanzania kivipi? Wao inakuwa rahisi sana kusema lakini wanashindwa kutekeleza kwa vitendo kuhusu rushwa na hali mbaya ya wananchi watanzania.

  Upuuzi mtupu na nimechoka na wanasiasa wetu ambao wanaongea lakini wanashindwa kutekeleza vitu ambavyo vinawezekana kabisa kwenye nchi yetu..........................Red Tape
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mazee afadhali umeliona hili.

  Nadhani mzigo wa lawama pia utuendee sisi wananchi kwani kwa namna moja au nyingine sisi pia tumeiangusha nchi kwa kukaa kimya badala ya kumtetea yeyote anayesema ukweli. Tu waoga mno. Tumegawanyika kivyama na kidini. Kwa jinsi hii nchi yetu inatumbukia shimoni na hamna anayejali, zaidi kuishia kulaumiana nakushutumiana.
   
Loading...