Viongozi wa dini ni wajibu wenu kufanya upatanishi kwani viongozi wa kisiasa wameshindwa maridhiano yanahitajika sasa

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Wadau nawasalimu,

Nichukue nafasi hii kuwaomba viongozi wetu wa dini kutumia busara na hekima zao walizojaliwa na Mungu kuwakusanya Marais wote wastaafu bara na visiwani,Makamu wa Rais wote wa bara na visiwani,Mawaziri Wakuu Wastaafu, Maspika Wastaafu, Majaji Wastaafu na watu mashuhuri na viongozi wa dini zote ili kufanya upatanishi kwa wanasiasa wetu kwa maana ya ccm na upinzani.

Kutokana na matukio ya kutisha ya kisiasa yaliyoanza kujitokeza na kushamiri toka utawala wa awamu ya 5 chini ya Hayati Magufuli.

Hakuna mtanzania asiyejua nini kimetokea na nini kinaendelea kutokea.Matukio ya watu kupigwa risasi,kutekwa kupotea kubambikiziwa kesi za ugaidi na uhujumu uchumi wapinzani wamejaa magerezani kwa kesi za kutengenezwa.

Ni wakati sahihi kwa viongozi wa dini kusimamia maridhiano hayo kam a viongozi wa dini wa nchi nyingine wanavyofanya.

Chonde chonde viongozi wetu hakika Mungu atawabariki ktk kufanya upatanishi
 
Mm naomba hii hali iendelee mpaka tutakapo chapana. Tukichapana tutaheshimiana Sana. Tuzichape!
 
Neno la hekima. Mathayo 5:9
Heri wapatanishi;
Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
 
Kila mtu apambane na hali yake, upinzani wanapambania maslahi yao, CCM wanapambania ulaji wao pia na sisi wengine tunaendelea kupambania mikate yetu.
 
Kwenye kulinda maslahi yao CCM hawatasikia la mpatanishi yeyote kutoka popote, wakati huu usio wa uchaguzi watakaa chini muongee, ila uchaguzi ukifika huwa wanasahau makubaliano yote ya kabla, akili huwarudia uchaguzi ukishapita wakishatangazwa washindi na kina Mahera.
 
Viongozi wa CCM wanafaidika na mgawanyiko ulioko ambao wanauchochea kwa kutumia jeshi la polisi ili waendelee kutawala milele.
 
Back
Top Bottom