Viongozi wa dini mkanyeni Makonda!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,236
Kunukuliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akisema kuwa anapokuwa amesimama yeye basi anakuwa amesimama Mungu, kumeleta mfadhaiko miongoni mwa watu wenye akili timamu wanaojua nini inamaanishwa inaposemwa neno "Mungu". Lakini kauli hiyo pia imezifedhehesha dini zote zilizoko duniani.

Kila watu wakienda wanakoabudu wanaambiwa wanamuabudu "Mungu", halafu anasimama mtu na kusema akisimama yeye anakuwa amesimama Mungu, hili ni dharau kwa waabudu Mungu. Makonda anataka kusema yeye ni Mungu ama ni Mwakilishi wa Mungu?

Kama waislamu wanasema "hakuna apaswaye kuabudiwa ila ni Mungu pekee..." nao ndugu zao Wakristo wanasema "Mungu ni mwenye wivu.." inakuwaje wanakaa kimya mtu mwingine anapojifananisha na Mungu? Au viongozi wa dini nao wanaamini anaposimama Makonda anakuwa amesimama Mungu?

Ukimya wa viongozi wa dini juu ya kauli ya Makonda kuhusu Mungu unapalilia ile dhana kwamba viongozi wa dini Tanzania wana Shirika na viongozi wa Serikali wanaotokana na CCM. Maana kuna wakati watu waliuliza inakuwaje viongozi wa vyama vya upinzani huwa hawaalikwi kwenye yale matamasha ya "amani"? Kumbe inawezekana waandaji labda huwa wanaogopa kumuudhi Mungu kwa kuwaalika Mashetani.

Hata kama aliahidi kusaidia kujenga Makao Makuu ya BAKWATA ama alimtembelea Kadinali Pengo Ofisini kwake, ni lazima Makonda aonywe na akemewe hadharani kwa tendo lake la kujilinganisha na Mungu. Viongozi wa dini huo ukereketwa wenu wa CCM unawaondolea sifa ya kuwa viongozi wa dini kwani sifa mojawapo ya kuwa kiongozi wa dini ni kuzuia Mungu KUDHIHAKIWA!!
 
Umenikumbusha ile hadithi ya nani mwenye uwezo wa kumfunga paka Kengele??

Viongozi wa dini awamu hii wote wanampigia makofi Mukulu na wasaidizi wake na kuimba nyimbo za mapambio, hawataki kumuudhi Mukulu wala wasaidizi wake maana "hawajaribiwi"
 
Wanachukua sadaka zetu, wanatuhimiza tutoe zaka na tuwe watu wema kwa kuwa Mungu anataka tuwe hivyo. Anakuja mtu anasema akisimama yeye anakuwa anasimama Mungu na viongozi wetu wote wa dini wako kimya. Kuna nini?
 
Mkuu, umelala na kuamka. Na kifungua kinywa chako ni Makonda?
Chakula chako cha machana na jioni ni Makonda?

Tafadhali NENDA KAFANYE KAZI iliuendelee na ujenzi wa taifa.
HOJA ama MADA hiyo ilishajibiwa zamani.
Hivyo ni STALE news/KIPOLO cha habari ambacho si kitu cha muhimu KUKIRUDIA RUDIA.
Taifa lina mambo muhimu zaidi kuliko hizo fitina ndogo ndogo.
By the way,
Je umefikia wapi na huo MRADI wako uliouanzisha????
 
Viongozi wa Dini wanasiasa hawawezi kufanya kitu,

Wapo viongozi wa Dini wana kesi mpaka Leo, mm namwamini Sana Gwajima, Ponda na wachache wao,

Wengine waoga kuwapigania waumini wao, wakiogopa vitisho vya Serikali,

Bado tunasafari ndefu,
 
Drama zake azifanyie uko kwenye siasa. Yeye anataka aonekane kama Mungu kwa lipi hasa alilo nalo la kufananishwa na Mungu. Ndiyo maana watu kama hawa FaizaFoxy huwa anawauliza "uko shuleni mlikwenda kusomea ujinga?"
Padre Mapunda, Sheikh Khalifa na Sheikh Ponda ndio wanajinasibu kuisemea jamii. Wengine naona kama wanaogopa kufutiwa leseni zao. Wapo kimyaa na jana huyo Mheshimiwa alikuwepo kwenye ibada siti ya mbele kabisa na hakuna wa kumwambia kwamba hilo alilonena ni upotovu.
 
Kunukuliwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akisema kuwa anapokuwa amesimama yeye basi anakuwa amesimama Mungu, kumeleta mfadhaiko miongoni mwa watu wenye akili timamu wanaojua nini inamaanishwa inaposemwa neno "Mungu". Lakini kauli hiyo pia imezifedhehesha dini zote zilizoko duniani.

Kila watu wakienda wanakoabudu wanaambiwa wanamuabudu "Mungu", halafu anasimama mtu na kusema akisimama yeye anakuwa amesimama Mungu, hili ni dharau kwa waabudu Mungu. Makonda anataka kusema yeye ni Mungu ama ni Mwakilishi wa Mungu?

Kama waislamu wanasema "hakuna apaswaye kuabudiwa ila ni Mungu pekee..." nao ndugu zao Wakristo wanasema "Mungu ni mwenye wivu.." inakuwaje wanakaa kimya mtu mwingine anapojifananisha na Mungu? Au viongozi wa dini nao wanaamini anaposimama Makonda anakuwa amesimama Mungu?

Ukimya wa viongozi wa dini juu ya kauli ya Makonda kuhusu Mungu unapalilia ile dhana kwamba viongozi wa dini Tanzania wana Shirika na viongozi wa Serikali wanaotokana na CCM. Maana kuna wakati watu waliuliza inakuwaje viongozi wa vyama vya upinzani huwa hawaalikwi kwenye yale matamasha ya "amani"? Kumbe inawezekana waandaji labda huwa wanaogopa kumuudhi Mungu kwa kuwaalika Mashetani.

Hata kama aliahidi kusaidia kujenga Makao Makuu ya BAKWATA ama alimtembelea Kadinali Pengo Ofisini kwake, ni lazima Makonda aonywe na akemewe hadharani kwa tendo lake la kujilinganisha na Mungu. Viongozi wa dini huo ukereketwa wenu wa CCM unawaondolea sifa ya kuwa viongozi wa dini kwani sifa mojawapo ya kuwa kiongozi wa dini ni kuzuia Mungu KUDHIHAKIWA!!
Hatari sana hiyo.
 
shige2 wewe unadhani kuandika JF kunazuia kufanya kazi? Kwani umeambiwa mimi nafanya kazi ya kuosha masufuria kwa mama ntilie?
 
Hilo neno kutoka kwa makonda wala silioni kuwa lina tatizo.

Simply amemaanisha kuwa yupo na Mwenyeezi Mungu na anasimamia haki.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom