Lord OSAGYEFO
JF-Expert Member
- Feb 19, 2021
- 3,086
- 4,881
Hakika inashangaza sana kwa viongozi wetu wa dini kukaa kimya juu ya suala la katiba mpya. Viongozi wa dini wameshuhudia matumizi mabaya ya katiba iliyopo yalivyofanywa na mwendazake.
Watu wengi wameumizwa sana na katiba hiyo kwani mwendazake aliweza kuitumia atakavyo. Hayati baba wa taifa aliwahi kusema katiba hii ukipata kiongozi mbaya atawaumiza wananchi na ndivyo ilivyotokea.
Tunawaomba viongozi wa dini zote mkishirikiana na viongozi wa vyama na asasii za haki za binadamu tuidai katiba mpya ili nchi iongozwe kwa haki bila upendeleo na kumfanya mtu mmoja anakuwa mungu mtu.
Nchi za jirani tumewashuhudia viongozi wa dini wakishiriki kuwapigania wananchi kupata katiba mpya mfano jamhuri ya kidemokrasia ya kongo n.K. Viongozi wa dini mtamwambia nini Mungu atakapowauliza kwanini hamkuwasaidia watu wangu wasiteswe na watawala?