Viongozi wa dini...jk akija mumkumbushe haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa dini...jk akija mumkumbushe haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewDawnTz, Nov 19, 2010.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Amesema atakuja kuongea na nyie kuhusu mgawanyiko wa kidini uliokuwepo.

  Sina uhakika kama mlishiriki nae kuunda huo udini kiasi cha kuja kuwauliza namna ya kuumaliza, maana kama hamkushiriki huenda hamjui sababu ya mgawanyiko wa udini na msiweze kumsaidia bali kuongeza mgawanyiko uliopo.....Nina wasiwasi juu ya hili.

  Hata hivyo mwambieni anahitajika kufanya yafuatayo kati ya mengi,

  (i) Kuwaomba radhi watanzania kwa yeye na mwenzake makamba kuasisi siasa za udini Tanzania. Kwa kuwa wote tunajua yeye na makamba ndio waasisi, wasipofanya hivi tutawaona wanafiki tu wakiendeleza unafiki wao wa ku-win mioyo ya wabongo ili 2015 watuletee bomu jingine

  (ii) Kuomba radhi viongozi wa CHADEMA tena mbele ya umma uleule ambao waliwasingizia kuwa wanasiasa za udini jambo ambalo uthibitisho wake ni mfinyu maana unajengwa kwa akili za kuku wa kafara

  (iii) Kuunda tume mpya ya uchaguzi itakayokuwa huru na isiyo mikononi mwake ili isendelee kubeba uchakachuaji

  (iv) Katiba mpya itakayotoa mwanya wa kuwajibisha viongozi wasioingia madarakani kwa haki na wanaotumia madaraka yao vibaya

  Kwa leo haya yanatosha labda kama wadau watawaongezea mengine viongozi wa dini

  Bila haya hatutawaelewa, hata kama wewe ni askofu wangu au nani,


  HII NI HATMA YA NCHI YANGU AMBAYO NI ZAIDI YA DINI YANGU
   
 2. nginda

  nginda JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 745
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa mchanganua mzuri na wakuleta mwanzo wa mjadala ya JK. Mimi naomba niongeze moja ambalo JK anaona aibu kulisema. Siyo athari za kidini kama anavyojichnganya, ni athari za umimi (kama ilivyodhihirika kwenye kampeni za BMW-baba mama watoto).
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ni kweli ningependa JK afanye hayo mkuu hata mimi yananitatiza baada ya kumshutumu chama kuwa cha kidini unataka yaishe kirahisi namna hiyo
  jingine mkuu UFISADI JAMANI NITATIZO KUBWA ZAIDI YA TUNAVOLIONA!
   
 4. Double X

  Double X Senior Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIi nafikiri uyu mkwere akija kwen nyie viongozi wa dini kuongea masuala ya udini, dont bother yourself to discuss with him,mwambieni wakati wa kampeni yeye na makamba ndio wamehubiri sana mambo ya udini ivyo wakayamalize wenyewe.
   
 5. i

  ifolako Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania bila udini haiwezekani-akina kobe wamenywea kimya,giza totolo.
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mgawanyiko wa kidini umo ndani ya ccm-ashughulike nao humo kwanza.
  chadema na uraiani hakuna tatizo-chadema ni 50/50
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mpaka siku mtu wako wa karibu zaidi atakapopigwa mapanga kwa misingi ya kidini ndo utajua kwa nini tunataka Tanzania isyo na udini.

  Chukua hatua bana ya kukomesha sio kukalia bongo za kijinga kuwa Tanzania bila udini haiwezekani, mbona iliwezekana hapo kabla???

  Sasa hivi tulipofikia watu tunaulizana dini zetu kabla hata ya mambo mengine ya msingi kama elimu, uwezo, ujuzi na mengineyo. Huku tuliko ni kubaya na ni lazima tutoke huku.

  OLE WENU MAKAMBA NA KIKWETE KAMA HII MBEGU MLIYOIPANDA HAITAKUFA, HAKIKA ITAWATAFUNA NINYI NA VIZAZI VYENU ZAIDI
   
Loading...