Viongozi wa Dini ishurutisheni Serikali ijisafishe suala la Lissu kama inasingiziwa

superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
5,610
2,000
Viongozi wa dini mpaka sasa ishu ya Lissu vs Serikali mmeikalia kimya huku kila upande ukijihisi una haki.

Mpaka Sasa Lissu ni mshindi kwasababu hana kosa lililompasa kuuwawa katika mazingira Yale. Na Wala hana kosa lolote lililomstahili kifo.

Binafsi sijamsikia igp siro akisema lolote ila Kama serikali inataka kumkamata lisu akija nchini basi iseme wazi kosa lake ni lipi na kama kosa wanalomkamatia ndio Hilo lilimstahili kifo maana mpaka sasa ishu ya lisu sio ya kitaifa ni ya dunia nzima.

Lolote lisu atakalofanyiwa litaandikwa katika historia ya Tanzania.

Kifupi serikali ya awamu ya tano imejitengenezea zimwi lake liitwalo Tundu Lissu .

Viongozi wa dini kama mpo Tanzania liangalieni suala la Lissu unbiased.
 

jmushi1

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
22,870
2,000
CCM wanasema kosa lake ni usaliti ndo maana wakataka kumuuwa, ndo maana Siro hawezi fanya lolote kwasababu nao ni Policcm.
 

superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
5,610
2,000
CCM wanasema kosa lake ni usaliti ndo maana wakataka kumuuwa, ndo maana Siro hawezi fanya lolote kwasababu nao ni Policcm.
Amemsaliti nani ? Taifa? Kwa lipi? Mbona ishu yake iko wazi sana ? Je ni mikataba? Kama ndivyo kwanini mikataba waliweka Siri? Lissu haikumpasa kufa kabisa Lissu alipaswa kuhojiwa kama ni mkosefu agaisnt our mother land Lissu haikumpasa kuuwawa. Viongozi wa dini kabla hawajamuombea Magufuli na kumuita nabii wanapaswa kumhoji kwanza kuhusu lisu na Beni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom