Viongozi wa dini dua zenu kwa wanasiasa zimejaa machukizo na unafiki

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,301
12,600
Huwezi kuwa unaomba Mungu kwa dhati halafu Mungu azibe masikio yake kwako. Tatizo mnaombea wanasiasa na taifa kinafiki kwa maslahi yenu ya duniani.

Mh. Rais JPM aliwapenda sana lakini mlishindwa kumuomba Mungu ampe afya na maisha marefu kwakuwa hamkuwa na dhamira ya kuomba bali maslahi.

Mtu anaambiwa aombee mkutano wa hadhara kama Mei Mosi iliyokusanya watu wengi mbalimbali ili mkutano uanze na kuisha salama lakini utamsikia kiongozi wa dini anaiombea CCM, Rais, Bunge, kusifu viongozi nk. hii ni njaa iliyochanganyika na unafiki, na dua za aina hii ni chukizo kwa mwenyezimungu, na Mungu anazitupilia mbali sala na dua za hizi.
 
Twende na PM ^Car-phone^ ama Hussein Jr ileeee 2025 maana hii namba ya awamu ya 4 inaturudisha upigajini & udilini
 
Kuzunguka note huko lakini point inayoonekana hapa ni kuiombea CCM.
Watu wanakosea sana kuitenganisha CCM na serikali. Ilikuwa ni lazima chama kilichosimamisha serikali kiombewe. Hakuna namna nyingine mkuu.
 
Kiombewe ili kipite bila kupingwa au nini? Mimi sikuwa na maana ya ccm wewe ndiye unasema hivyo.
 
Kuzunguka note huko lakini point inayoonekana hapa ni kuiombea CCM.
Watu wanakosea sana kuitenganisha CCM na serikali. Ilikuwa ni lazima chama kilichosimamisha serikali kiombewe. Hakuna namna nyingine mkuu.
Kila mtu mwenye maoni tofauti ni mpinzani, mtalifikisha taifa kubaya.
 
Sio wakweli na zaidi ya yote ni waoga. Hawana ujasiri wa kukemea uovu.
Huwezi kuwa unaomba Mungu kwa dhati halafu Mungu azibe masikio yake kwako. Tatizo mnaombea wanasiasa na taifa kinafiki kwa maslahi yenu ya duniani.

Mh. Rais JPM aliwapenda sana lakini mlishindwa kumuomba Mungu ampe afya na maisha marefu kwakuwa hamkuwa na dhamira ya kuomba bali maslahi.

Mtu anaambiwa aombee mkutano wa hadhara kama Mei Mosi iliyokusanya watu wengi mbalimbali ili mkutano uanze na kuisha salama lakini utamsikia kiongozi wa dini anaiombea CCM, Rais, Bunge, kusifu viongozi nk. hii ni njaa iliyochanganyika na unafiki, na dua za aina hii ni chukizo kwa mwenyezimungu, na Mungu anazitupilia mbali sala na dua za hizi.
.
 
Ila kiukweli tunawalaumu kwa kuwa tunatarajia wao kuwa na nguvu ya kusimama mbele yetu kama makuhani wa Mungu. Ila sasa, kiuhalisia enzi za hayati 2tanzania wote waliufyata. Waliojitutumua kuwa majasiri hatimaye walilazimika kukimbia. Salama ya kila mmoja wetu ilikuwa kuimba mapambio ya kusifu tu. Tunatakiwa tujifunze kuwa wakweli. Tusilete mchezo linapokuja suala la Katiba mpya yenyekulinda haki za watu na maslahi ya nchi. Yenye kudhibiti mamlaka ya watawala bali inayowapa uwezo wa kuongoza kwa ushirikiano na mamlaka za uwakilishi wa wananchi. Collective leadership and responsibility. Daima tukumbuke , "majuto ni mjukuu"
 
Hili nalo neno asee... Very true.
 
Kuna mtu hata hajali kitu ilimradi miradi yake itapata ahueni kwa atakaepokea kijiti. Hana haja na nchi inaelekea wapi bali wasiwasi yake ni miradi yake yake itakuwaje kwa rais yule. Kuna kiongozi mkubwa anasema tumuongezee miaka rais kinafiki ilimradi atimize agenda yake nyuma ya pazia.
 
Huwezi kuwa unaomba Mungu kwa dhati halafu Mungu azibe masikio yake kwako. Tatizo mnaombea wanasiasa na taifa kinafiki kwa maslahi yenu ya duniani.

Mh. Rais JPM aliwapenda sana lakini mlishindwa kumuomba Mungu ampe afya na maisha marefu kwakuwa hamkuwa na dhamira ya kuomba bali maslahi.

Mtu anaambiwa aombee mkutano wa hadhara kama Mei Mosi iliyokusanya watu wengi mbalimbali ili mkutano uanze na kuisha salama lakini utamsikia kiongozi wa dini anaiombea CCM, Rais, Bunge, kusifu viongozi nk. hii ni njaa iliyochanganyika na unafiki, na dua za aina hii ni chukizo kwa mwenyezimungu, na Mungu anazitupilia mbali sala na dua za hizi.
Aisee 🤔🤔
 
Usichululie seriously mkuu! Kumbuka Mungu hapangiwi.
Wengine kutimiza protocal tu
 
Nilimuona yule kionhozi wa dini ya Hindu akikuwa akiomba kwa usahihi kutoka moyoni kwake kuliko haya madhehebu ya dini zetu zilizokuja na majahazi. Ni mpaka hapo tutakapotambua kosa letu kwenye dini tunazozitumia kuliombea taifa letu la tanganyika ndipo uokovu utakapoturudia
 
Mama yetu Samia aache kabisa kuongozana na viongozi wa dini kwaajili ya kumuombea kwa Mungu. Kila mtu kwenye mkutano amuombe Mwenyezingu wake yeye mwenyewe kwa sauti, lugha na matamanio yake kutoka kwa Mungu wake. Wachungaji na Masheikh ni wanafiki wanaoganga njaa zao. Wanatarajia malipo ya duniani badala ya yale ya Mungu.
 
Back
Top Bottom