viongozi wa dini chonde chonde tena chonde! msituletee balaa! tusaidieni kuleta umoja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

viongozi wa dini chonde chonde tena chonde! msituletee balaa! tusaidieni kuleta umoja

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kituro, Jan 18, 2011.

 1. k

  kituro Senior Member

  #1
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Viongozi wetu wa dini, tuwaombe msitujengee uadui kati ya watu wa dini na dini eti sisi tuone watu furani ni bora kuliko wengine!. kumbukeni sisi sote ni ndugu kwakuwa kwasasa karibu kila familia ina angalau mtu mmoja wa dini nyingine! hivyo kutupandikizia chuki na kuona kuwa kila dini ni wababe hii haitatusaidia, pia lazima mjue ya kuwa dini zote ni mpango wa mungu kuwepo kwasababu ingekuwa dini furani mungu haipendi nanyi mmetuhakikishia ya kuwa mungu ni muweza wa kila kitu hivyo dini ambayo MUNGU hajaikusudia ingepotea au mungu angewalinda watuwake wasiingie dini hiyo!

  viongozi wetu wa dini tunawathamini sana na tunajuwa mnafanya kazi nzito ya kutuongoza kiroho, tunawaomba tena mtusaidie kutuongoza ili kuujenga na kuulinda umoja wetu.

  tusaidiane kuhamasisha umoja wa kitaifa na si kujenga ubaguzi wa aina yoyote!. nchi ni yetu nasi ndo sehemu ambayo tunaweza kuishi kwa amani kuliko sehemu yoyote ile duniani!. mtu kwao!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  HAKI kwanza!!!!!

  Amani na umoja wa kitaifa ni matunda yake. Usitegemee matunda kama mbegu uliopandanda ardhini ni DHULUMA na UFISADI!!!
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wametumwa hao,kwa ufupi ni kwamba wamechoka kuimba wimbo wa amani wana tafuta kibwagizo kingine
   
Loading...