Viongozi wa dini aina ya Gwajima, Mwingira na Kakobe ni wa kupuuzwa, wanachojali ni matumbo yao tuu.

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,311
"Nilitumia miaka 15 kumlilia Mungu tupate mtu atakayeipenda Tanzania, atakayewapenda Watanzania, Mungu akakuleta Rais Magufuli." Mwingira Mbele ya JPM 2018.

"Nilinusurika kuuwawa mara tatu,awamu ile ilikuwa inadhulumu haki za watu na kupora uchaguzi." Mwingira chini ya Rais Samia 2021.

Hawa wanaojiita maaskofu na wana makanisa yao wengi sio wasafi kama tunavyofikiri. Maneno yao tuu yanawafunga, sembuse matendo? Wengi maneno yao yanalenga kujifanya kuendana na upepo wa serikali iliyopo madarakani, na wanapenda sana kubebwa hata kwenye mambo yasiyobebeka. Sasa wakikutana na kisiki kama JPM hawalalamiki, ila siku hiko kisiki kikitoka ndiyo wanaanza kujifanya kutoa ya moyoni.

Hawa maaskofu wachumia tumbo wakajifunze kwa mababa zao kina Askofu Shoo, Askofu Bagonza, Askofu Niwemugizi nk. Hawa hawajawahi kubadilisha nyeupe kuwa nyeusi kwenye maneno na vitendo vyao. Hawaogopi kuusema ule ukweli hata kama unakinzana na watawala.

Baada ya huyu Mwingira, tutegemee na Kakobe naye kuja na yake, maana hawa wote ni wachumia tumbo tuu.
 
Inasikitisha sana..hata wewe mleta uzi ni mchumia tumbo..umekuja kutetea upande unao chumia tumbo lako..njaa mbaya sana.

Ila ukweli utawala uliopita kwenye haki na demokrasi ulifeli pakubwa.

Mwisho..mwanadamu ni kiumbe mnafiki haaminiki.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwingira ni moja ya wahuni alias wezi na mafisadi hapa nchini. Ni wa kupuuza.

#kataawahuni
 
"Nilitumia miaka 15 kumlilia Mungu tupate mtu atakayeipenda Tanzania, atakayewapenda Watanzania, Mungu akakuleta Rais Magufuli." Mwingira Mbele ya JPM 2018.

"Nilinusurika kuuwawa mara tatu,awamu ile ilikuwa inadhulumu haki za watu na kupora uchaguzi." Mwingira chini ya Rais Samia 2021.

Hawa wanaojiita maaskofu na wana makanisa yao wengi sio wasafi kama tunavyofikiri. Maneno yao tuu yanawafunga, sembuse matendo? Wengi maneno yao yanalenga kujifanya kuendana na upepo wa serikali iliyopo madarakani, na wanapenda sana kubebwa hata kwenye mambo yasiyobebeka. Sasa wakikutana na kisiki kama JPM hawalalamiki, ila siku hiko kisiki kikitoka ndiyo wanaanza kujifanya kutoa ya moyoni.

Hawa maaskofu wachumia tumbo wakajifunze kwa mababa zao kina Askofu Shoo, Askofu Bagonza, Askofu Niwemugizi nk. Hawa hawajawahi kubadilisha nyeupe kuwa nyeusi kwenye maneno na vitendo vyao. Hawaogopi kuusema ule ukweli hata kama unakinzana na watawala.

Baada ya huyu Mwingira, tutegemee na Kakobe naye kuja na yake, maana hawa wote ni wachumia tumbo tuu.
Usiweke vipande weka hotuba/mahubiri yote.. nasi tuchambue.!!
 
Back
Top Bottom