Viongozi wa ‘Deci’ nyingine wakamatwa Dar-MMMH KOVA WE!!!WATAKULA WAPI ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa ‘Deci’ nyingine wakamatwa Dar-MMMH KOVA WE!!!WATAKULA WAPI ??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Apr 25, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,583
  Likes Received: 5,764
  Trophy Points: 280
  Jumamosi Aprili 25, 2009
  Habari za Kitaifa

  Viongozi wa ‘Deci’ nyingine wakamatwa Dar-
  Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 25th April 2009 @ 00:03 Imesomwa na watu: 238; Jumla ya maoni: 0


  Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili, wamiliki wa Kampuni ya Masebe Business Group kwa tuhuma za kuhusika na biashara ya upatu. Kamanda wa Kanda hiyo, Suleimani Kova jana aliwaambia waandishi wa habari, kuwa watuhumiwa hao Benos Tadu (32) na Samwel Tupa (33) walitiwa mbaroni baada ya Polisi kupata taarifa kuwa wanaendesha shughuli hizo Buguruni.

  Masebe Business Group ni kampuni ya pili kudhibitiwa na serikali kutokana na upatu katika kipindi cha wiki chache zilizopita, nyingine ikiwa ni Development of Entrepreneurship for Community Initiative (DECI) ambayo sasa inaandikisha majina ya wanachama ili kuwarudishia fedha zao.

  Alisema walipofanya upekuzi katika ofisi za kampuni ya Masebe, walikuta kitabu cha orodha ya wanachama, viwili vya stakabadhi za malipo na mihuri ya kampuni, vyote vikionyesha kuwa inafanya upatu kinyume cha sheria. Kamanda Kova alisema uchunguzi ukikamilika dhidi ya watu hao watafikishwa mahakamani.

  Katika hatua nyingine, Kampuni ya Deci kupitia ofisi zake za Mabibo, Dar es Salaam imetoa tangazo rasmi kuwa siku ya kuwarudishia wanachama ‘mbegu’ zao itajulikana baada ya kukamilisha uandikishaji na uhakiki wa majina na stakabadhi za malipo. Kwa mujibu wa tangazo hilo, hatua ya ulipaji itajulikana baada ya miezi miwili ijayo, kutokana na ratiba ya kampuni hiyo kuonyesha kuwa wanachama wa mwisho kuandikishwa ni waliopanda mbegu Oktoba mwaka jana na wataandikishwa, Juni 15 mwaka huu hatua za kurudisha mbegu zitatangazwa.

  Awali ratiba na matangazo ya kampuni hiyo yalisema wateja wataanza kurudishiwa mbegu (fedha) zao leo na kazi hiyo ingeendelea hadi Juni 16 mwaka huu. Aidha katika hatua ya kushangaza, uongozi wa Deci makao makuu jana uliwatangazia wanachama wake kuwa, kulingana na kauli ya Waziri Mkuu bungeni juzi, serikali ndiyo itasimamia na kulipa fedha za wanachama, hivyo Deci isiulizwe mpaka serikali itakapoamua.

  Sehemu ya tangazo ilieleza: “ Zoezi la kurudisha mbegu litaanza mara tu Tume iliyoundwa na serikali kushirikiana na uongozi wa Deci itakapotangaza rasmi kuanza kwa zoezi.” Hata hivyo, baadhi ya wanachama waliozungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, waliiomba serikali kusitisha pia hatua ya uandikishaji na uhakiki kwa kile walichodai kuwa wanahofu huenda utapeli unafanyika, kwani Deci iliwatangazia waliokwishavuna wasifike katika ofisi hizo tena, jambo ambalo ni kinyume na mapatano.

  “Tumetangaziwa hapa kuwa waliokwishavuna mara moja, wasije tena hapa, sasa mimi nilikatwa Sh 20,000 ya uanachama na asilimia kadhaa za fedha kama kodi kwa serikali na pia nilirudisha mbegu kwa ajili ya kuvuna tena, nashangaa wanasema eti sipati kitu, naomba serikali iingilie kati,” alidai Christopher Michael. Katika eneo la ofisi hizo baadhi ya wanachama waliokuwa na namba za kuandikishwa majina walichangisha fedha kwa wenzao kati ya Sh 500 na Sh 2,000 ili waingie na stakabadhi zao kwa ajili ya kuhakikiwa kutokana na msururu wa watu uliokuwapo.

  Deci ni kampuni iliyoandikishwa Julai 25 mwaka jana chini ya usimamizi wa kidini na Msajili wa Kampuni nchini (Brela) kwa ajili ya kusaidia waumini wenye uwezo mdogo, lakini ilibadilika na kufanya upatu kinyume cha sheria jambo lililosababisha serikali iifungie na uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo kuanza. Vilevile serikali ilisema ilichukua uamuzi huo pamoja na wa kushikilia akaunti za kampuni hiyo na za wakurugenzi wake ili kuhakikisha kuwa wanachama wote wanapata amana na fedha zao zote.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ni bora hiyo wameishtukia mapema kabla haijaleta madhara makubwa kama ya DECI!
   
 3. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kanda Maalum ya polisi Dar-es-Salaam inahitaji msemaji maalum zaidi ya huyu Kova ambae kiiiila siku yuko kwenye vipaza sauti vya TVT.

  Kamanda Kova, weka spokesperson. Huwezi kuwa kwenye kumbi za habari kila siku, nenda kafanye kazi.
   
Loading...