Viongozi wa DARUSO na TAHLISO mmelala, hamjui majukumu yenu mpo mpo tuu!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,145
2,000
Nilikua najaribu kufuatilia tatizo la mikopo ya elimu ya juu mfano kwa vyuo vikuu vilivyoko mkoani Dar es salaam, yaani mtu una uweza kutokwa machozi. Ni idadi kubwa sana ya wanafunzi ambao hawana mkopo wanalia na familia zao ni za hali ya chini kabisa. Mfano chuo kikuu cha UDSM, kuna wanafunzi wengi hawana mikopo kabisa na hawajui shule zao zitakwenda vipi.

Kuna wanafunzi waliodahiliwa kwa vigezo vya diploma, hawa ndio utafikiri nchi hii sio ya kwao. Yaani wanateseka utawaonea huruma. Viongozi wa nchi wapo na wamewawekea vigezo vizito ili kuua ndoto zao, viongozi wa nchi hawana huruma kabisa na vijana hawa. Wakati wanaingia madarakani waliahidi kwa vinywa vyao kua kila mwanafunzi atakayedahiliwa atapata mkopo, sasa hawa ambao wako vyuo vikuu na walidahiliwa kwa vigezo kuna tatizo gani nao kunufaika na mkopo? Ni lina vijana hawa watakua wazalendo na taifa lao kama wananyanyasika kiasi hiki?

Wakati wengine tunasoma hatukuwahi kukumbana na fedheha hizi, vijana jana wale waliosoma kozi za vipaumbele wote walipatiwa mkopo. Lakini hivi sasa unaweza kufika pale DIT unakuta kijana anasoma engineering hana mkopo, Unaweza kupita chuo kikuu chochote cha afya unakuta wanafunzi wanasomea udaktari lakini hana mkopo. Huu ni uonevu mkubwa.

Viongozi wa wanafunzi hasa DARUSO,TAHLISO wamepigwa ganzi wapo wanawatazama wenzao wakiteseka bila utetezi wowote. Wanaiogopa serikali utafikiri watafukuzwa vyuo wakiongea. Wanawasaliti wenzao na hawafai kabisa kua watetezi wa wanafunzi. Mbona enzi za TAHLISO ya kina Mh Makonda watu tulikua active na tuliweza kubadili mambo lukuki? Hawa watoto wa sasa wakoje? Wamelishwa nini?
 

SuperSub

Member
Aug 19, 2017
52
125
Wewe unataka hao viongozi wa DARUSO wafanyaje?
Wahamasishe Maandamano au?
Mkopo wanatoa serikali sio DARUSO,komaa na serikali iongeze pesa kwani kila mwez mimi nakatwa laki 4 za heslb naamini pesa wanayo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom