Viongozi wa Dar ni majipu

Big Dy

JF-Expert Member
Dec 23, 2015
475
561
Salam wana JF,

Kwa wengi tulio wakazi wa Dar tangia utawala mpya uingie tumekua tukipata ahadi nyingi sana kutoka kwa viongozi wetu wapya ila nyingi zimegeuka kuwa ni za kisiasa tu hazina ukweli.
Kwa mfano;
1.Mh. Mkuu wa mkoa alivyoingia alitangaza walimu kupanda mabus bure sidhani kama jambo hilo limetelekezwa mpka sasa.

2.Bomoa bomoa iliyowaacha wakazi wengi wa mji huu bila hifadhi ila moka sasa hakuna kilichotelekezwa katika sehem zilizo vunjwa.

3.Usafi wa mwisho wa mwezi japo jambo hili limekua likitiliwa mkazo ila bado kasi iliyo anza inalungua siku hadi siku

4. Madada poa pembenizoni mwa barabara usiku, hii nayo ilionekana kuvaliwq njuga mwanzoni na kupotea juu kwa juu ambapo sasa ukipita sehem nyingi walizokua wanajiuza dada zefu hawa wameanza kurudi taratibu.

5. Machinga maeneo yaliyokua si rasmi kwa biashara zao, kuanzia last week jiji kushirikiana na Polisi wake wamekua wakiwatoa machinga maeneo mengi kama vile kariakoo na posta ila nguvu hii inaoneka kuisha na wafanya biashara hawa wameanza kurudi tena katika maeneo waliyokua wanafukuzwa.

Kwa mtamzamo wangu naona viongozi hawa wamejawa na siasa nyingi kuliko vitendo vya hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom