sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,488
Tumeyasikia maneno ya mwenyekiti wa CWT mwalimu Gratian Mukoba lakini nani asiyemjua,? Tangu amekuwa mwenyekiti wa chama hicho amekuwa akiongea hayo hayo kuwahadaa walimu.
Tujikumbushe uchaguzi wa mwaka juzi wa kumpitisha tena yeye na team yake ile ile uliofanyika AICC ARUSHA uliofunguliwa na kusimamiwa na raisi mstaafu daktari JAKAYA MRISHO KIKWETE. Mwenyekiti aliyepitishwa na raisi ambaye ndiye mwajiri ana uthubutu wa kumpinga kweli?
Mukoba na team yake ni sehemu ya serikali hivyo hawana uwezo wa kumtetea mwalimu. Wanatumbua tu fedha za walimu hakuna cha CAG kuwakagua na wala serikali haiwagusi na wenyewe hawaigusi serikali kwenye maslahi ya walimu wala matatzo yao, ni kama kila mmoja anamtega mwenzake kwamba "mwaga ugali nimwage mboga" hivyo matatizo ya walimu hayawezi kutatuliwa chini ya kina Mukoba, hivyo wanapaswa kukaa pembeni kuinusuru elimu ya watoto wetu maana hili la kufeli kwa watoto hadi kwenye mia bora zinaingia shule 2 tu za serikali, lina uhusiano na mslahi na matatizo ya walimu. Na chanzo ni kuwa na viongozi wabovu wanaowahadaa wale wanaowaongoza.
Nawasilisha.