Viongozi wa CUF na wanachama 200 wahamia CCM Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CUF na wanachama 200 wahamia CCM Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Aug 12, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Lwakatare alipo amua mkasema Oh Chadema wanaisaidia CCM , leo mtasema CCM ...

  Na Felix Mwagara

  MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Keko Machungwa Jiji Dar es Salaam wa Chama Cha Wananchi (CUF) pamoja na katibu wake wamerudisha kadi ya chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiambatana na wanachama wapya 203.

  Tukio limetokea jana katika viwanja vya Bulyaga Temeke katika mkutano wa CCM ulioandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbass Mtemvu kwa ajili ya kuongea na wananchi na kutoa mambo ambayo ameyafanya katika jimbo hilo tangu alipopata ubunge.

  Mwenyekiti huyo wa Cuf anayetambulika kwa jina la Zuberi Mahami pamoja na katibu wake Christina Giddo walisema wameamua kukihama chama hicho kwakuwa kimepoteza mwelekeo katika uongozi.

  “Sikuona ubora na uzuri ndani ya chama cha Cuf zaidi ya yale niloyaacha ndani ya Chama Cha Mapinduzi, nilikuwa ndani ya uongozi ndani ya Cuf kwa muda mrefu nikiwa mwenyekiti wa chama hicho Keko machungwa nimeamua kurudi ndani ya CCM kwakuwa huku ndiko kwenye ukweli” alisema Mahami na kuongeza;

  “Natoa pongezi kwa wale wote waliokuwa wananiambia toka huko, njoo huku, kwa kweli viongozi mbalimbali wa CCM walikuwa wananiambia nitoke Cuf, nami nalikaa nikafikiria, nikaona hakuna umuhimu wowote ndani ya Cuf” Kwa upande wake Mtemvu akiwakabidhi kadi za Chama Cha Mapinduzi viongozi hao wa Cuf pamoja na wanachama 203 wapya aliwapongeza kwa kukikimbia chama cha Cuf.
  [FONT=verdana,geneva,lucida,'lucida grande',arial,helvetica,sans-serif]
  [/FONT]
   
 2. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ni hatari wanazidisha mafisadu tu huko CCM hawana lolote hela zitawatoa roho

  Tatizo la CUF sio wa kweli wataishia kuhama tu Pai Sasa kwa hilo jambo

  wanaona kutakuwa na maendele Tanzania kweli Mh Mh
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa nimekupata sawia
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa kifupi ni kuwa tunapoteza muda wetu mwingi kujadili siasa, vyama vya siasa, au nani yuko chama gani and so forth.. Tumekuwa na vyama vingi hapa Tz kwa zaidi ya muongo mmoja hivi sasa, na dalili zaonyesha wazi hata tukipewa miaka mingine 2000, bado tutakuwa masikini wa kutupa.

  Kitu kinachotakiwa kukifanya ili kuhakikisha utendaji wa serikali unakuwa murwa bin ok, ni kudhibiti influence ya siasa ktk utendaji wa serikali. Tukichagua hili mambo yetu yataenda kisayansi na kujali hali halisi na bila shaka tutaona mafanikio ktk kipindi kifupi. Kwa kuweka mfumo ambapo wanasiasa watakaa mbali na national stakes ndio siri pekee iliyobaki kwa taifa lililojaa mafisi wa utajiri kama Tz.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Bandiko nimeleta ili kutaka kujua wale walio ishanbulia Chadema siku za nyuma na mameno ya kwamba ina mpango wa kuia CUF .Hili ndilo nilitaka wajue kwamba watu kama Lwakatare hawa kununuliwa.Ila wimbi la watu kuhama waina ya hawa wa jana ni matokeo ya pesa na kadiri siku zinavyo sogea ndiyo utakuwa mradi wao .
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ukianza kudiscuss vyama unaweza kesha hapa hata mwaka hujapata jibu. Nafikiri siasa ni game fulani kama ya kishetani. Inabidi tuishi kwa imani vinginevyo tutalalama kila siku.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ndio Maneno yenu hayo kila siku... CCM inafanya kweli tu daima!
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kweli Kibs, CCM inafanya kweli daima e.g kwiba kura, kupigaj watu , kuuwa, kunyan'ganya, ufisadi....na hao wanachama "bandia" wanaodaiwa wa CUF, hawana waliloendea huko isipokuwa hayo hayo.
   
Loading...