Viongozi wa CUF na gari lao wafukuzwa na wamachinga hapa soko la Kilombero, Arusha

Hivi CUF mna matatizo gani ? CHADEMA walishasema Huko kaskazini ni nchi yao ,nyinyi mnaenda kuwasumbulia nini ?
Kwanza mlikuwa na viza ? sawa sawa mlivyo dundwa, mnaingilia nchi ya kaskazini bila kufata taratibu...next time na nyinyi
wakikatiza anga zenu watieni adabu...mshasahau JINO KWA JINO ?
 
wamachinga wa dsm sisi tutajikusanya kuhakisha cdm hafanyi mkutano tutakwenda mbali zaidi kuhakikisha mali za washirika wa cdm maghorofa ya sabodo mahoteli club mbowe yani bilcanas tutahakisha njia zinazo ipa je uri cdm mashirika yao yakiporomoka wengi watakosa ajira jeuri itakwisha arusha wamachinga vyema mmetuonesha njia tunasema wamachinga wa dar tuna maliza tena kwakuwarudisha makwenu huko nchi ya kaskazini.
 
Hivi CUF mna matatizo gani ? CHADEMA walishasema Huko kaskazini ni nchi yao ,nyinyi mnaenda kuwasumbulia nini ?
Kwanza mlikuwa na viza ? sawa sawa mlivyo dundwa, mnaingilia nchi ya kaskazini bila kufata taratibu...next time na nyinyi
wakikatiza anga zenu watieni adabu...mshasahau JINO KWA JINO ?

wamachinga wadar sisi tutamaliza harakati za cdm.tutaporomosha mali na majengo ya mafisadi akina mbowe na mshirika wao sabodo kwani pesa za sabodo zimewatia mimba vijana wa cdm. Mpaka wanajisahau wao ni watz na kila mtu anafanya siasa popote
 
Usultani unaujua wewe? au unasukumwa tu.inafahamika Chadema wana nguvu baadhi ya meaneo ya Arusha.lakini ni sahihi kuwazomea na kuwafukuza na kuwarushia mawe Cuf wasitangaze mkutano wao? ikiwa hivyo ndivyo, na maeneo ambayo Cuf wana nguvu washabiki wake wakiwazomea na kuwafukuza chadema nchi hii itakuwaje? tusishabikie upumbavu, Chadema inaendeshwa na wasomi na sisi tunaamini hilo. Siku zote Elimu na Hekima ni vitu viwili vinavyokwenda sambamba. kuweni wastaarabu.Elimu mliyokuwa nayo na Demokrasia mliyokuwa nayo haijawafundisha kuwavumilia msiowataka?
 
Source Jambo Leo

Viongozi wa wafuasi wa chama cha wananchi CUF wanadai kushambuliwa na mawe na wafuasi wanaominika kuwa ni wa CHADEMA katika harakati za chama hicho kujitangaza na kuweka mikutano yake Mkoani Arusha
 
Nipo hapa sokoni Kilombero na wamachinga wanajigawia kwa utaratibu mzuri sana kuliko ule uliofanyika na Mkuu wa wilaya kule nmc.

Gari la CUF la matangazo likawa linakuja kuingia ili litangaze mkutano, wanawake wamachinga wamepiga ukunga CCM B wanafiki wanakuja wamachinga wote wakawapigia kelele na gari la CUF likaondoka na kuzima muziki mara moja.

"Imesemekana kuwa waliowapopoa CUF mawe ni wafuasi wa CDM" Kwani CCM hawajui kurusha mawe? ama kweli CDM inawatia kiwewe "Mtu na Mkewe" sa' nani atalinda nyumba kama bwana na bibi wote waoga wa kupiga mayowe?
 
kupiga ukunga ndio kufanya nini wakuu??

Kupiga ukunga ni KUPIGA YOWE LINALOASHIRIA HATARI....AU JAMBO LA KUTISHA ....MATHALANI.....Mtu akiwa anaibiwa au amevamiwa anahitaji msaada!, Au Mtu amefiwa !!! KUPIGA UKUNGA----Hutumiwa sana na WAMERU,WAPARE,WAARUSHA NA WACHAGA
 
"Imesemekana kuwa waliowapopoa CUF mawe ni wafuasi wa CDM" Kwani CCM hawajui kurusha mawe? ama kweli CDM inawatia kiwewe "Mtu na Mkewe" sa' nani atalinda nyumba kama bwana na bibi wote waoga wa kupiga mayowe?

Mimi natamani sana mabadiliko ya utawala yatokee tz,na kati ya vyama mbadala vilivyopo CDM kinanipa matumaini zaidi. Lakini napinga kwa nguvu zangu zote kitendo kilichofanywa na wamachinga wa Arusha, siamini kama ni washabiki wa ccm maana kama wana uwezo huo wangefanya kwa cdm sio cuf ambao sio saizi yao kwa Arusha. Uongozi wa juu wa cdm inabidi wakemee tabia hii haraka maana ina madhara kwa chama, kwanza itafanya wenye busara washawishike kuamini kuwa ni cha wahuni, pili cha kikanda na si cha uvumilivu kwenye ushindani wa kisiasa. Mbona m4c imefanyika mikoa ya kusini kwa mafanikio bila fujo toka kwa mashabiki wa cuf japo wameumia kuona ngome yao inatekwa? Ushabiki wa namna hii sio mzuri kwa mustakabali wa cdm na ata taifa letu, ccm wanaweza kutumia fursa hii kuzigombanisha cuf na cdm na kuipa wakati mgumu kama si kuifuta kabisa cdm katika baadhi ya maeneo hasa Zanzibar japo ilishaanza kukubalika.
 
Hivi CUF mna matatizo gani ? CHADEMA walishasema Huko kaskazini ni nchi yao ,nyinyi mnaenda kuwasumbulia nini ?
Kwanza mlikuwa na viza ? sawa sawa mlivyo dundwa, mnaingilia nchi ya kaskazini bila kufata taratibu...next time na nyinyi
wakikatiza anga zenu watieni adabu...mshasahau JINO KWA JINO ?

Acha ushabiki wa kiccm katika mambo ya maana, naona unatumia nguvu nyingi kuchonganisha zaidi badala ya kukemea vitendo hivi vya kiuni visivyo na tija kwa demokrasia na maendeleo ya taifa letu.
 
Hivi CUF mbona mnakosa la kusema?.Hivi ina maana kwamba wakati mnapita pale,kulikuwa na viongozi wa CHADEMA?,na hao viongozi walijua kwamba mtapita mkitangaza halafu wawapige mawe?.Ukweli ni kwamba wananchi wameichuikia sana CCM na wanaona kwamba CUF ile ya zamani,sio ya sasa.Licha ya hivyo,wakati CUF wanapita wananchi walikuwa na hasira kwasababu ya kusumbuliwa na manispaa.Hivyo,waliowarushia mawe ni Wanachi,na sio CHADEMA.Hivi pia ule mkutano wenu mlioshindwa kufanya, pia mtasema ni CHADEMA walifanya hila,nyie hamkubaliki Arusha,na ukweli utakuwa ni huo.
 
Kupiga ukunga ni KUPIGA YOWE LINALOASHIRIA HATARI....AU JAMBO LA KUTISHA ....MATHALANI.....Mtu akiwa anaibiwa au amevamiwa anahitaji msaada!, Au Mtu amefiwa !!! KUPIGA UKUNGA----Hutumiwa sana na WAMERU,WAPARE,WAARUSHA NA WACHAGA

Hiyo kitu wasukuma huiita NG'WANO.
 
By asigwa kupiga ukunga ndio kufanya nini wakuu??
Ni kupiga kilio cha kuashiria msiba
Ukunga ni YOWE ambayo inatumika kujulisha jamii iliyopo uwepo wa hatari, msiba au kitu kingine ambacho si cha kawaida katika jamii husika
 
Wewe utakuwa hukumsikia yule mbunge mstaafu alivyosema kuwa CUF wamewavamia huko north !!!!!Cha kushangaza hawa CHADEMA Walivyoenda NCHI YA CUF ( PEMBA NA UNGUJA) walikaribishwa TENDE NA HALWA .....
 
Acha ushabiki wa kiccm katika mambo ya maana, naona unatumia nguvu nyingi kuchonganisha zaidi badala ya kukemea vitendo hivi vya kiuni visivyo na tija kwa demokrasia na maendeleo ya taifa letu.

Wewe utakuwa hukumsikia yule mbunge mstaafu alivyosema kuwa CUF wamewavamia huko north !!!!!Cha kushangaza hawa CHADEMA Walivyoenda NCHI YA CUF ( PEMBA NA UNGUJA) walikaribishwa TENDE NA HALWA .....
 
kosa walilofanya CUF ni kuwanyooshea kidole cha kati wananchi waliokuwepo pembezoni mwa barabara ndiyo MALIPO waliopata CUF.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom