Viongozi wa CUF na gari lao wafukuzwa na wamachinga hapa soko la Kilombero, Arusha

Madhila ya kukubali kutumiwa yatatufikisha pabaya.

Kwanini CUF walienda/walipita eneo lile lile ambalo wamachinga walikuwa wanajitafutia nafasi ktk soko ambapo ilisemekana kuna purukushani. Je akili na busara ya CUF iko wapi hapo? Kwani wasingeweza kwenda maeneo mengine kisha baadaye kuja kupita eneo hilo likiwa shwari?

Pili, je wamejuaje kuwa waliowapopowa mawe na wana-CHADEMA? Au ndio ktk kukubali kuwa Arusha YOTE nii CHADEMA!
Kama CUF mkishindwa kuthibitisha hii hoja ya uanachama wa waliopiga mawe..... basi msitafute mchawi, busara inasema ondokeni Arusha kwa amani na ustaarab
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
27/09/2012​
WANACHAMA WA CUF KUPONDWA MAWE NA WAFUASIA WA CHADEMA ARUSHA.ONYO KWA CHADEMA
CUF Chama cha wanachi kinalaani kitendo cha wafuasi wa CUF kupondwa mawe na wafuasi wa CHADEMA walipokuwa wakiendelea na shughuli kutangaza mikutano inayoendelea Arusha . Chama cha wananchi CUF kinasikitishwa nakulaani kitendo cha viongozi wa chadema mkoani Arusha kuwashawishi wafuasi wao kuwaponda mawe wanachama wa CUF wanaoendelea na mikutano ya kisiasa inayofanywa na CUF tangu mwanzo wa wiki hii.Hii imedhihirishwa na maeno na Godbless Lema juzi alipokuwa waapowahutubia wafuasi wa Chadema kwenye viwanja vya Stendi ya Nduruma alisema kwamba CUF wametuvamia na kuwasihi ile slogan ya “kamata mwizi men” sasa ianze.Na ushahidi tuanao. Hata hivyo wameshawishi vijana kugawa kiwanja vya Levorosi stendi ya Nduruma kwa kisingizio kwamba wanataka kuweka meza za biashara kiwanja ambacho CUF tuantegemea kufanya mkutano wa hadhara siku ya Jumapili. Leo asubuhi wanachama wa CUF wamepondwa mawe walipokuwa mtaa wa Kilombero kata ya Levorosi.Kutokana na vurugu hilo gari la matangazo la CUF limepondwa mawe na mwanachama mmoja aitwaye Athuman Abdurahman alipigwa jiwe jichoni na taarifa tumezifikisha polisi. CUF kinaona Chadema kama chama kisichoweza siasa za ustahimilivu,hawajiamini na bado ni wachanga kisiasa.Hii inadhirishwa na kutoelewa maana ya demokrasia na uhuru wa Mtanzania kuamua kujiunga na chama chochote atakacho.Bado hawajakomaa kisiasa kama jinsi CUF ilivyokaomaa kisiasa hatukudhuru chama chochote wanapofanya siasa maeneo mbalimmbali hapa nchini. CUF inatoa onyo kali kwa viongozi wa Chadema kwamba hali hii ikiendelea wajue hawataweza kufanya shughuli zao sehemu yoyote Tanzania kwani uwezo wa kuwafanya tutakavyo tunao na kwasababu wameanza tuanaweza kumaliza.Ile NGANGARI kwa polisi tunaweza kuwahasishia wao wakose pa kukaa, ila hatupendi tufikie huko na kama wanabusara na ni wanasiasa kweli wenye nia ya kutumia hoja badala ya vurugu kumkomboa mtanzania watafakari hilo. CUF inaendelea kusisitiza tutaendelea na shughuli za kisiasa mkoani Arusha hakuna wa kutuzuia na tutaendelea Oparesheni MCHAKAMCHAKA na mikutano itaendelea kufanyika na kama wao ni wababe kweli na wanatumia hoja ya vurugu waendelee na mipango yao ya hujuma na tutawafundisha siasa kwani bado hawajakomaa. Imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari ,Uenezi na Haki za Binadamu CUF. Mh.Abdul Kambaya Simu:0719566567 Chanzo www.cuf2015plus@worlpress.com
Hivi nyie cuf mna akili timamu kweli??
Mnavyosema eti chadema wamewatuma wamachinga waweke meza za biashara kwenye uwanja mliopanga kufanya mkutano siku zijazo ina maana hamjui kuwa eneo hilo liliporwa na lilikuwa limezungushiwa mabati hawa wamachinga wameyatoa mabati haya ndo wakaanza kujipimia maeneo.
Je nyie cuf iyo jumapili mlipanga kuja kuyatoa hayo mabati na kufanya mkutano wenu?????
Acheni kutoa matamko ya kujitia aibu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kupiga ukunga ndio kufanya nini wakuu??

Jeshini wanaita "bigula" ni yowe la kutahadharisha kuwa kuna hatari ipo katika eneo husika, hivyo jamii ijihami kwa chochote iwezavyo na kuchukua hatua ya haraka kubaini na kufika kwenye eneo la tukio tayari kwa lolote.
 
Mimi hata siwafahamu nyie gwandaz,kila siku mnasema arusha ni CDM hakuna CCM huko lakini vijana wakifanya fujo mnasema ni wa CCM, hebu kuweni na msimamo mmoja basi.

kwa hiyo nawe wakitiri kwa kinywa chako kuwa arusha ccm kwishney. ccm itakufanya u-paralyse kabla ama kunako 2015.
 
Nipo hapa sokoni Kilombero na wamachinga wanajigawia kwa utaratibu mzuri sana kuliko ule uliofanyika na Mkuu wa wilaya kule nmc.

Gari la CUF la matangazo likawa linakuja kuingia ili litangaze mkutano, wanawake wamachinga wamepiga ukunga CCM B wanafiki wanakuja wamachinga wote wakawapigia kelele na gari la CUF likaondoka na kuzima muziki mara moja.

asante sana kwa kutabanaisha hivyo kuliko mtatiro anayesema chadema wamewafanyia fujo cuf
 
hali isiyo ya kawaidia gari la matangazo la cuf limepata wakati mgumu kwa machalii wa arusha baada ya kuwa na maamzi ya kulipiga gari lao mawe na kuwataka watoke maeneo ya kilombero ambako wamachinga wamevamia maeneo ya wazi na kujijengea vibanda kwa ajili ya biashara, ndipo cuf au kwa jina lingine ccm b walipo jikuta wanawakati mgumu sana nakupigwa mawe,
 
Chadema siasa ilishawashinda....safari hii cuf watawanyoosha
OK kumbe wewe ndo kambaya kwa kweli kwa style hii ya kuonyesha mahaba live na ccm ni dalili tosha kuwa cuf imeamua kutumika nimekuwa ninafuatilia mijadala yako kibao kwenye vyombo vya habari unatetea ccm sana wewe pamoja na udini usio na maana kwa watanzania sasa jana mlikuwa pale mbauda sokoni haibu mliyopata haijawatosha tu Arusha ni KITOVU Cha UKOMBOZI, ACHANA NA SIASA ZA CCM WAMEZISHINDWA KINA NAPE NYIE VIBARAKA MTAZIWEZA WAPI............. KIKWETE NA PINDA WANAFIKA ARUSHA KIMYA KIMYA NYIE Mnajifanya kupiga kilele kweli kazi yenu kwisha mliona CHADEMA Wameenda kusini na nyie mkaiga kuja arusha M4C Moto wewe, CHEZEA A. Town muone.
 
ha ha ha yaan R chuga ni noma nilikuwa hapo 1 week,dah!c o siri tungekuwa hivyo tz ccm tungekuwa tushawang'oa kitambo
 
Nipo hapa sokoni Kilombero na wamachinga wanajigawia kwa utaratibu mzuri sana kuliko ule uliofanyika na Mkuu wa wilaya kule nmc.

Gari la CUF la matangazo likawa linakuja kuingia ili litangaze mkutano, wanawake wamachinga wamepiga ukunga CCM B wanafiki wanakuja wamachinga wote wakawapigia kelele na gari la CUF likaondoka na kuzima muziki mara moja.

.
Hivi ule msemo wa ''ukiiga tembo kunya utapasuka msamba''bado upo?
Hili nalo ni tatizo la ku-copy na ku-paste.
.
 
Hizi propaganda za CUF ni za kijinga sana na za kizamani sana, mambo ya kitoto kabisa,

Hata Igunga CUF walikuwa wanafanya kama haya huku tayari tayari wamejitega mitandaoni na taarifa kabla ya tukio la kutengeza halijatokea.
 
Back
Top Bottom