Viongozi wa Chama na Serikali kuendelea kufurika Chato na Geita, huku kwingine sisi si waTanzania?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Siyo vibaya kwa viongozi kutembelea wananchi mikoa yote na kujua matatizo yao pale walipo.
Lakini sasa imetokea tabia kwa viongozi wengi wa Kitaifa kuendelea kufurika Chato na Geita, ati kusimamia ahadi za chama na Ilani.

Sasa sisi wananchi wa mikoa mingine , hasa kwa mfano mikoa ya kwetu huku Mbeya,Katavi, Songea viongozi hatuwaoni kuja kutatua matatizo lukuki yanayotukabili.

Hatusemi msiende Chato hapana, nendeni tu hata kwa mapumziko ya weekend, lakini huku mkwetu nasi tuna matatizo mengi tu ya kijamii.

Ahadi zilizotolewa na chama toka miaka ya Mzee Mkpa hazijatekelezwa, lakini utasiki Chongolo anasimamia soko la Chato!

Tukumbuke kuwa hii ni "apartheid" ya kimaendeleo ya aina fulani tunazidi kujenga.
Nachokoza tu!!!

cc https://www.jamiiforums.com/members...miiforums.com/members/johnthebaptist.228646/;

Kinyungu

 
Tulikua tuingizwe kwenye mfumo kama wa North Korea wa kuamudu Makaburi ya Madikteta.
Kwa kweli ni aibu.
Au ni kwa vile wana uhakika wa kubaki madarakani, basi wanawadharau wananchi wa sehemu nyingine.?
 
Back
Top Bottom