Viongozi wa CHADEMA ziarani mkoani Tanga...!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CHADEMA ziarani mkoani Tanga...!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Feb 19, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jopo la viongozi wa Baraza la vijana wa Chadema (BAVICHA) limeanza ziara ya kukiimarisha chama mkoani Tanga. Jopo hilo linaongozwa na Mwenyekiti wa Bavicha bw. John Heche akipewa support na Naibu katibu mkuu bara Mh. Zitto Kabwe (MB) pamoja na Mh. John Mnyika (MB) na ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi.

  Ratiba kamili ya ziara yao ni kama ifuatavyo;
  Jumamosi (jana) tarehe 18/02/2012 -Walikuwa Mkata, Handeni.
  Jumapili (leo) tarehe 19/02/2012 - watakuwa Korogwe mjini (uwanja wa manundu) na baadae Mombo.
  Jumatatu tarehe 20/02/2012 - watakuwa Muheza.
  Jumanne tarehe 21/02/2012 - watakuwa Pangani.
  Jumatano tarehe 22/02/2012 - watakuwa Tanga mjini.

  Kazi kwenu wanaTanga, waja leo warudi leo. Makamanda wako nyumbani kwenu kwa kazi moja tu, kuwaletea ujumbe wa matumaini na ukombozi ili ikifika 2015 msirudie kufanya makosa.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Safi ni vema pia mkatupa na feedback ya kinachojiri nashauri tuweke mbali ushabiki usio na tija itolewe taarifa ya kila eneo lilatombembelewa tujue ikiwa chama kinakubalika au la kama hakikubaliki tujue nini cha kufanya
   
 3. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hapo umenena,itatusaidia kujua uimara wa chama.
   
 4. kilght

  kilght JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 626
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  waendelee kusema chama cha msim:lol:
   
 5. S

  Selungo JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  HESHIMA MBELE NA HONGERENI MAKAMANDA WETU!

  Wakuu! Hapo kwenye nyekundu kuna tatizo la maji la kufa watu na umeme tangu MAGAMBA waongoze nchi hii. Ahadi zimekuwa zikitolewa ikiwa ni pamoja na kuambiwa kuna mradi wa maji wa Bilioni 9 umeanza kujengwa wakati hata mahali unapo jengwa hapaonekani hapo MUHEZA. Mto Zigi ambao ndiyo chanzo kikuu cha maji kwa mji wa Tanga na vitongoji vyake, upo umbali wa kilometa kama saba hivi toka Muheza mjini. Licha ya mto Zigi, pia lipo bwawa la maji kwenye mlima wa magoroto ambalo nalo lingeweza kuondoa tatizo la maji hapo Muheza. Ambacho kingetakiwa ni kuunganisha bomba la sasa na bwawa la maji la Magoroto (umbali wa kilometa mija), ili kupata maji ya uhakika. Kwa vile wamelenga kwenye ufisadi wa mradi mkubwa wa maji, hawataki kuunganisha hii kilometa moja ili watu wapate maji ya uhakika.

  Rais JK na Mbunge wake watoa ahadi zisizo na mashiko hadi watu wamekata tamaa. Hivi ninavyo andika shida ya maji kwa sasa haielezeki hapo MUHEZA. Umeme pia limekuwa tatizo kiasi cha kutisha. Shughuli za uzalishaji zimesimsimama kwa kipindi kirefu sasa. Barabara ya Amani imekuwa ni njia ya kwenda jehanam maana hatamaniki kabisa.

  Hata mkichukuwa bodaboda hapo Muheza mngeweza kwenda na kujionea hilo bwawa hapo juu Magoroto. lakini sababu zimekuwa zikitolewa, eti maji ya kwenye bwawa hayatoshi wakati hata hayo yanayo tosha hakuna matumaini ya kuyapata.

  Wilaya ya Muheza inazalisha matunda mengi aina ya machungwa na maembe. wanaMuheza wamekuwa maskini wa kutupwa na kuwa wakuwekeza machungwa kwa Madalali kabla hayaja komaa kwa ukosefu wa kiwanda cha kusindika matunda. Ujenzi wa kiwanda umekuwa ni ahadi ya wana MAGAMBA isiyo tekelezeka kila mwaka wa uchaguzi.

  Mkiangalia barabara za mitaani hapo mjini Muheza mtashangaa jinsi zilivyo mbaya. Hazija fanyiwa matengenezo kwa miongo kadhaa sasa. Fedha zote kwa ajili ya matengenezo ya hizo barabara zinaliwa na wajanja hapo Halimashauri. Na kwa vile madiwani wote ni kutoka MAGAMBAZ kila kitu ni ZIDUMU.

  Kazi ni moja tu. ELIMU YA URAIA KWA WANA MUHEZA.

  NAWASILISHA.

  Mngekuwa na muda wa kutosha, mngetembelea huko kwenye milima ya Amani ndiyo mgeshuhudia umasikini wa kutisha.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jana ZITTO KABWE alishindwa kufika Lushoto, sijui kwa leo kama ameonekana kwenye mikutano mingine!
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Viva makamanda.
   
Loading...