Viongozi wa CHADEMA watekwa na majambazi Kahama wakitoka kwenye kampeni

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,739
4,732

Msafara wa viongozi na wanachama wa chama Demokrasia na Maendeleo Chadema wa Kanda ya ziwa Magharibi wametekwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakati wakitoka kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za serikali za Mitaa kata ya Bulyanhulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.


Akizungumza na waandishi wa habari ikiwemo Malunde1 blog, Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Kahama, Juma Protas(PICHANI)alisema tukio hilo lilitokea juzi katikati ya Kijiji cha Kalagwe kata ya Ntobo na Kijiji cha Nyambula Kata ya Ngongwa majira ya Saa 3:30 Usiku wakati wakitoka kwenye Kampeni Kijiji cha Kakola.

Akizungumzia tukio hilo Protas alisema walipofika eneo la Daraja walikuta magari matatu yamesimama pembeni ambayo ni Basi la Jordan ambalo lilikuwa linatoka mkoani Geita kuelekea Kahama,Roli aina ya Fuso na Gari ndogo inayomilikiwa na Kampuni ya TBL kupitia bia ya Balimi ambayo nayo yalikuwa yametekwa.

Alisema wakati wanajaribu kuyapita magari hayo ghafla waliona Mawe na Miti ambayo ilikuwa imetandazwa barabarani na ndipo majambazi hao waliamuru Msafara huo ambao ulikuwa na magari mawili wenye watu 10 wasimame na watoe simu na fedha walizokuwa nazo.

“Tulisikia sauti wakisema zimeni taa za gari na muziki na hatuwezi kuwadhuru nyinyi Makamanda ila tunataka fedha na simu, na tupo kazini mnatakiwa kuwalaumu viongozi waliokula Pesa za Escrow bila hiyo tusingefanya haya mnayoyaona”alifafanua Protas.

Aliwataja waliokuwemo kwenye msafara huo kuwa ni mratibu wa Kanda ya ziwa mashariki Renatus Mzemo, Mwenyekiti wa Kamati ya Rasilimali Kanda ya ziwa Magharibi, Emmanuel Mbise na Mwenyekiti wa Kamati ya Uenezi wa chama hicho Kanda hiyo Juma Protas ambaye ndiye Mwenyeki wa Chadema.

Viongozi hao wa Chadema walikuwa wamepanda gari aina ya Toyota Prado yenye no. T 707 BBP ambayo hata hivyo ilivunjwa baadhi ya vioo.

“Tuliibiwa fedha tathimini zaidi ya shilingi laki tisa pamoja na simu 11 ambazo hazikufahamika mara moja thamani yake na gari yetu moja ambayo ni ya mdau alyejitolea kutusaidia ilivunjwa vioo na ile ya M4C yenyewe walisema hawawezi kuivunja maana ni wananchi walichanga kuinunua”,aliongeza Protas

“Kulikuwa na magari mengi tuliyoyakuta yametekwa na abiria walinyang’anywa simu na fedha zao, pia kulikuwa na Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Lunguya ambaye alitekwa akiwa na pikipiki na wakamfunga Kwenye mti pamoja na ddugu yake na baada ya kuchukua fedha walitoweka kusikujulikana”,AliongozeaMwenyekiti huyo.

Hata hivyo Jeshi la Polisi wilayani Kahama lilifika eneo hilo baada ya kupewa taarifa na abiria waliokuwa kwenye basi ambalo lilitekwa na kukuta majambazi hayo yakiwa yametokomea kusikojulikana na kutoa msaada wa kiusalama kwa magari yote na abiria waliotekwa.


Na Ndalike Sonda-Malunde1 blog Kahama
 
Duh!! Poleni sana Makamanda!! Sipati picha ungekuwa ni msafara wa ma CCM, lazima tungepunguziwa idadi ya majizi ya escrow kwa kusema RIP!!
 
Mkuu nimecheka sana na habari hii.
Mleta mada siyo mzima.
Sasa nani kamanda alieteka au alietekwa? Hao wamejiteka wenyewe kutafuta huruma ya wananchi, huo ni uongo mtupu.
Tushawazoea hawa, wanaendeshwa na matukio, ndio maana kila uchaguzi, wanabuni matukio ili waonewe huruma.
Unakumbuka Mzee Slaa aliwahi kuzusha kuwa amekamata Kontena lenye kura feki huko Tunduma?
 
Tushawazoea hawa, wanaendeshwa na matukio, ndio maana kila uchaguzi, wanabuni matukio ili waonewe huruma.
Unakumbuka Mzee Slaa aliwahi kuzusha kuwa amekamata Kontena lenye kura feki huko Tunduma?

Huyo mzee ndiyo muongo kabisa, Mbowe nae wakajilipua kisha anasimama eti anao mkanda wa video, sijui anaangalia na familia yake, hawana hoja wao wanaenda na matukio, kama sasa wameshupalia escrow bila hiyo hawana hoja ya kutafutia huruma ya wananchi.
 
Badilisha kichwa cha habari kisomeke, "Viongozi wa CHADEMA watekwa na Maintarahamwe."
 
Habari hii nimeidhibitisha toka kwa mdau aliyeko Kahama. Poleni sana wote mliokumbwa na tukio hilo ila kwa kweli watu wana hasira na Escrow saga.
 
Poleni sana makamanda,hakuna kulala hadi hawa majizi wa lumumba wajisalimishe kwa umma
 
Kuanzia saa 1 usiku barabara inayopita kalagwe huwa si salama kabisa. Anyway poleni makamanda.
 
Naamini siku maccm yakitekwa haki ya nani yatakuwa tigo, haya majamaa yalivyo na hasira na fedha za escrow sijui!!
 
Wamejiteka wenyewe hao wahuni!

Mkuu nimecheka sana na habari hii.
Mleta mada siyo mzima.
Sasa nani kamanda alieteka au alietekwa? Hao wamejiteka wenyewe kutafuta huruma ya wananchi, huo ni uongo mtupu.

Rich Pol, ndio kauli za mazuzu wa CCM, kila kitu wao wanageuza siasa. Kule Arusha Cdm walipopigwa bomu na watoto kuuwawa mkutanoni super star wao wa enzi zile Mwigulu alitoa kauli kama hiyo "wamejilipua wenyewe!" yaani upuuzi mtupu.

Leo, huyu mwanalumumba, abiria wa basi wanatekwa na kuporwa, yeye haoni, anawaona Chadema tu.

Ndio maana Watz wanakufa kwa kukosa dawa hospitali, wao wanakwiba tu kama vile hawaoni athari zozote.

Vv
 
Rich Pol, ndio kauli za mazuzu wa CCM, kila kitu wao wanageuza siasa. Kule Arusha Cdm walipopigwa bomu na watoto kuuwawa mkutanoni super star wao wa enzi zile Mwigulu alitoa kauli kama hiyo "wamejilipua wenyewe!" yaani upuuzi mtupu.

Leo, huyu mwanalumumba, abiria wa basi wanatekwa na kuporwa, yeye haoni, anawaona Chadema tu.

Ndio maana Watz wanakufa kwa kukosa dawa hospitali, wao wanakwiba tu kama vile hawaoni athari zozote.

Vv

Mleta mada ameweka uongo mwingi sana mpaka uzi umeharibika, eneo lile lina tatizo la utekaji kwa miaka mingi ndiyo maana kukawa na escort kupita eneo lile, eti majambazi ya kirundi yaulizie escrow? Ukawa itayasaidia nini? Ameharibu mwenyewe uzi kwa kuweka tukio la kijambazi kuwa la kisiasa na kuweka ushabiki.
 
Back
Top Bottom