Viongozi wa CHADEMA wapelekwa gereza la Isanga

NGOWILE

JF-Expert Member
Sep 8, 2011
454
258
Mkurugenzi wa organisation na mafunzo wa Chadema Taifa bwana Benson Kigaila na mratibu wa kinamama Chadema mkoa wa Dodoma Bi Kunti Yusuph leo wamepelekwa gereza la Isanga hapa Dodoma baada ya kukosa wadhamini katika kesi inayowakabili.

Hii ilitokana na aliyepewa jukumu la kuandaa wadhamini bwana Iddi Kizota ambaye ni katibu wa vijana mkoa wa Dodoma kutolewa nje ya mahakama na polisi kwa kitendo kilichodaiwa ni kudharau mahakama kwani alikuwa anataja majina ya wadhamini badala ya watuhumiwa wenyewe ambapo ilipelekea hakimu kuamuru atolewe nje ya mahakama na kupelekwa kituo cha polisi.

Kitendo hiki alichofanya katibu huyu wa vijana kilikuwa ni cha kizembe kwani alishauriwa kabla, kuwapa watuhumiwa majina ya wadhamini ili wawataje wenyewe mbele ya mahakama, hivyo ikapelekea watuhumiwa hawa wawili kati ya kumi na moja (11) kupelekwa Isanga hadi tarehe 08/11/2011 kesi itakapo tajwa tena.

Hata hivyo niliongea na diwani wa kata ya makulu Mh.Biringi akasema kesho watashughulikia remove order.

Makosa waliyotuhumiwa nayo ni pamoja na kufanya mkutano ambao haujaruhusiwa, kushawishi wananchi kufanya vurugu kwenye kitongoji cha njedengwa, kuwashawishi wananchi wa njedengwa kuwapiga askari kwa mishale ya sumu pamoja na kuvunja amani.

Naomba kuwasilisha.

Source nilikuwa mahakamani.
 
Ukiona kamata kamata imekuwa kwa sana basi fahamu kuwa FREEEEDOM IS COMING TOMORROW!!

Kamata weka ndani, kamata Slaa, Kamata Mbowe, kamata wote wapinzani kukandamiza sauti za wanyonge. Ole wenu watawala siku wananchi wakichoka.
 
Kamata weka ndani, kamata Slaa, Kamata Mbowe, kamata wote wapinzani kukandamiza sauti za wanyonge. Ole wenu watawala siku wananchi wakichoka.

Tulishachoka yani tunasubiri tu pakulipukia! nionavyo mie kwenye katiba mpya lami itakuwa mto wa damu! WACHAKACHUE TU! atusubiri tena watu wa dar tutalianzisha sisi huku mikoani.
 
Ukiona kamata kamata imekuwa kwa sana basi fahamu kuwa FREEEEDOM IS COMING TOMORROW!!

Hakika Setrikali chini ya CCM kuendekeza tabia ya kukamata viongozi na wanachama wa CDM ni kukaribisha kitu kinaitwa UKOMBOZI.Ni mbaya kuisikia masikioni mwa viongozi wengio wa dola na chama cha mapinduzi lakini huo ndio ukweli halisi.Mnaongeza chuki na picha iso faha kwa wanachama na wapenzi wa chadema,wnazingatia kuwa kuna uonevu na hivyo kinachofuata ni movement ya kujibu mapigo kwa namna ambayo Serikali itakuja kustuka ni vulugu wasio weza kuizibiti.Italipuka kama petroli kwenye kituo cha mafuta.
 
Nawaomba ndugu zangu chadema msije mkalipiza visasi 2015 ikifika.poleni sana.mia
 
Tutalipiza kwenye masanduku ya kura tu na kuwaeleza watanzania ukweli
 
So sad news to be heard! But they mustnt rest until our heroes are out! We mustnt allow this to continue otherwise it's tragedy.
 
hapa tusiweke siasa ni sheria kama hayo ni makosa ya kisheria watuhimiwa wanasitahili kwenda rumande
 
Hakika Setrikali chini ya CCM kuendekeza tabia ya kukamata viongozi na wanachama wa CDM ni kukaribisha kitu kinaitwa UKOMBOZI.Ni mbaya kuisikia masikioni mwa viongozi wengio wa dola na chama cha mapinduzi lakini huo ndio ukweli halisi.Mnaongeza chuki na picha iso faha kwa wanachama na wapenzi wa chadema,wnazingatia kuwa kuna uonevu na hivyo kinachofuata ni movement ya kujibu mapigo kwa namna ambayo Serikali itakuja kustuka ni vulugu wasio weza kuizibiti.Italipuka kama petroli kwenye kituo cha mafuta.
Labda ukiwambia wewe mfuasi wa CCM watakuelewa ukweli wanachemsha petrol kwenye pipa karibu na moto wa mwitu hakuna kitu kibaya kama kunyanyasa viongozi wa Chadema kiasi hicho wakati wa CCM wanafanya mikutano mahala popote na wakati wowote hii mbaya wanataka kutumbukiza nchi kwenye machafuko yatakayochukua muda kurekebishwa,nadhani wanadhani watawakatisha tamaa wanawapa ushujaa na wafuasi wao ndio wanazidi kuwa na imani nao
 
Back
Top Bottom