Viongozi wa Chadema waliokamatwa kwa kufanya mkutano ofisini kwao wakati huu wa janga la Corona wamwomba radhi DC na kuachiwa huru

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,561
Viongozi watatu wa CHADEMA wilayani Magu walikamatwa na polisi na kushikiliwa kwa zaidi ya saa 6 kwa kosa la kujifungia ofisini na kufanya kikao cha siri wakati huu wa Corona wameachiwa huru baada ya kuomba radhi.

Viongozi hao wakiongozwa na Katibu wa kanda wamesema ni kweli wamefanya kosa kwa kukusanyika wakati kuna kataxo la serikali kuzuia mikusanyiko ili kudhibiti Corona, wameapa kutorudia kosa.

Mkuu wa wilaya kwa kutumia wadhifa wake kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na msamaha aliwataka wasirudie tena upuuzi huo kisha akamuagiza OCD awaachie huru.

Chanzo: Star tv!
 
Badala ya kufunga makanisa ya gwajima .nyie mnakamata viongozi waangamizi wenye nia nzuri na Taifa letu la Asali , na maziwa.
 
Watu watatu?shame!Maana yake hata mtu akirudi nyumbani kwa mkewe na watoto ni mkusanyiko!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom