Viongozi wa CHADEMA walikwepa mazishi ya mjumbe wa kamati kuu (mamake zitto)

wabungenjaa

JF-Expert Member
Feb 21, 2014
1,782
336
Ukweli kuhusu Viongozi wa CHADEMA kukwepa mazishi ya Mama Zitto:

Kuhusuviongozi wakuu wa chama (Mbowe na Slaa)

Kumekuwa na upotoshaji mkubwa unaofanywa nawanaojiita makamanda wa CHADEMA na viongozi wao. Cha kushangaza zaidi ni pale Mbowe mwenyewe aliposikika akisema kwamba walimkodishia Wenje ndege kwenda Kigoma kukiwakilisha chama katika mazishi ya Marehemu Shida Salum, mamaye Zitto.Lakini wakati huo huo Wenje mwenyewe akinukuliwa akisema kwamba alikwenda Kigoma kwa lift ya ndege ya Mzee Nimrod Mkono.

Nimeamua kufanya ufuatiliaji na upeleleziwa kina ili kubaini ukweli kuhusu jambo hili.

Naomba sasa niuanike ukweli wote kama ifuatavyo:

Mtu aliye karibu sana na Zitto amenidokeza kwamba tangu mama alipoanza kuugua mpaka wakafikia hatua ya kumpeleka India, Zitto alikuwa akiwataarifu akina Mbowe na Slaa kwa njia ya sms kila hatua ya ugonjwa wa mama yake.

Chaajabu hakuna hata mmoja kati yao aliyewahi kwenda kumsalimia Mama Zitto mpaka anapelekwa India.

Baada ya mama huyo kurudishwa kutoka India, ndipo siku moja Mbowe akatokea nyumbani kwa mama Zitto usiku usiku kama mwivi.

Katika safari yake hiyo Mbowe alitokea akiwa yeye na dereva wa gari la serikali likiwa na namba za STK.

Hakuwa na mlinzi wala msaidizi yeyote wala kiongozi yeyote wa chama aliyeongozana naye.

Hiyo iliacha maswali kwamba je alikuwa anawatoroka wenzake na kusaliti makubaliano yao?

Baada ya kumsalimia mgonjwa, na yeye aliingia mitini mpaka hivi leo. Hakuwahi hata kuulizia tu kwamba hali yamgonjwa inaendeleaje.

Mdokezaji huyo alimnukuu Zitto leo mchana wa saa nane akisema hivi, naomba kunukuu: “Slaa hakufika kabisa hospitali wala hata kutoa salaam. Mpaka sasa (leo saa nane mchana) sijapata hata smsya Mbowe au Slaa au Lissu”, mwisho wa kunukuu.

KuhusuWenje na uwakilishi wa chama kwenye msiba:

Habari za uhakika ni kwamba kulikuwa na wazo kutoka kwa mbunge Grace Kiwelu (mjumbe wa kamati kuu) aliyekuwa anamshauri mbunge mwenzake na mjumbe mwenzake wa kamati kuu (Ezekiah Wenje) kwamba waende hospitali kumtazama MamaZitto akiwa mgonjwa.

Baada ya kukubaliana waliungana na wabunge wengine Halima Mdee na Esther Buraya na walifika hospitali majira ya saa 3 mpaka saa 4 asubuhi tarehe 1Juni.

Baada ya kumtazama mgonjwa ambaye wakati huo alikuwa haongei,walishuka chini na wakiwa bado wapo hapo maeneo ya hospitali, mgonjwa alikata roho! Hivyo walilazimika kubaki hapo mpaka wakaambatana na mwili wa marehemu kwenda msikitini Upanga.

Wakiwa msikitini Upanga walisikika Wenje na Kiwelu wakiambizana kwamba wawatafute kwenye simu Mbowe na Slaa wawashauri watafute hata ndege ya kukodi ili wahudhurie mazishi maana wasipofika itakuwa ni stori.

Mpaka sasa haijafahamika kama walifikisha ushauri huo kwa Mbowe na Slaa na waliupokeaje mabosi wao hao.

Wakiwa pale pale msikitini akina Kitila Mkumbo walikuwa wakifanya arrangement ya usafiri wa mwili, watoto na ndugu wakaribu wa marehemu kuondoka siku hiyo hiyo jioni kuelekea Kigoma na wakati huohuo wakifanya arrangement kwa waendaji wengine wanaotaka wachangie nauli ya kiasi cha shilingi 450,000/= (kwenda na kurudi) ili wapande ndege ya ATC kesho yake asubuhi kuelekea Kigoma kuwahi mazishi.

Wakati huo huo Mzee Nimrod Mkono alisikika akiwa anafanya arrangement ya ndege ya kukodi kwenda kuhudhuria mazishi.

Wenje akaona kuliko atoe shilingi 450,000/= yake, alisikika akimbembeleza mzee Mkono ampe lift kwenye ndege yake. Ni mzee Mkono yule yule wanayemwita fisadi na yeyote wa upinzani anayeonekana hata amesimama na mzee Mkono wanaongea, naye anaitwa fisadi. Ndiye huyo huyo aliyempa Wenje lift kwenye ndege.

Labda naWenje naye siku hizi ni fisadi!!!

Pale msibani, waliitwa wawakilishi wa makundi mbalimbali kutoa salaam za rambi rambi. Mwakilishi wa bunge la Jamhuri(Ndugai), Bunge la Afrika mashariki (Kimbisa), Kamati ya bunge ya hesabu zaserikali (Filikunjombe), Kamati ya wabunge wa CCM (Vita Kawawa) na bunge laKatiba (Lipumba).

Kisha wakaitwa viongozi wawakilishi wa vyama vya siasa kutoa salaam za rambirambi: CUF (Lipumba), NCCR (Machari), ACT-Tanzania (Mwigamba),CCM (Amani Kabourou) na hatimaye wakaitwa CHADEMA ambapo hapakuwa na mtu aliyejitokeza,ndipo kuona hivyo Wenje akaruka kutoka miongoni mwa waombolezaji na kukimbiapale mbele. Akazungumza maneno yafuatayo, naomba kumnukuu:
“Mimi naitwa Ezekiah Wenje. Ni mjumbe wakamati kuu ya CHADEMA. Shida Salum alikuwa mjumbe mwenzangu wa kamati kuu. Nahapa naweza kuzungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa chama taifa. Bahati mbaya jambo hili limemkuta mwenyekiti wa taifa akiwa mbali sana kijijini ambako alikuwa anafanya harambee. Shida Salum alikuwa mtu ambaye kwa kiingereza huwa tunasema, she speaks her mind. Alikuwa akizungumza kile anachokiamini.

Tunatoapole kwa familia yote na kwa kweli tunawaombea. Kimsingi hapa hata tukitoamchango wa namna gani hautasaidia lolote! Cha muhimu ni kuwaombea”. Mwisho wakunukuu.

Ni muhimu kukumbuka kwamba wakati Wenjealasiri ya Jumapili akiwa Kigoma alidai Mbowe yuko mbali sana kijijini anafanyaharambee, taarifa ya habari ya ITV ya jioni ya siku hiyo hiyo, ilimwonyeshaMbowe akiwa Arusha na Lema wanafanya mikutano ya hadhara.

Katika mazingirahayo, je ni halali kwa Mbowe mwenyekiti wa chama taifa, kiongozi wa kambi rasmiya upinzani bungeni, kudanganya umma kwamba walimkodishia Wenje ndegekuhudhuria mazishi? Tumwogope Mungu.

Yule jamaa hakutumwa kukiwakilisha chamabali alikurupuka kukinusuru chama baada ya kuona hakuna hata mwenyekiti wa katawa chama aliyejitokeza kukisemea chama na viongozi wake wakuu wamepuuza ushaurialiowapa jana yake akiwa msikitini.

Hata Anthony Komu, Mkurugenzi wa Fedha waCHADEMA ambaye naye alihudhuria mazishi, alifika pale kwa urafiki wake binafsina Zitto na kimsingi alipewa lift na Dr. Kitila kwenye ndege ya ATC kwa urafikihuo huo kati ya Komu na Kitila.


Hivyo ndivyo ilivyokuwa, mwenye kubisha aje na ushahidi..
kama mjumbe wa kamati amekimbiwa vipi mimi na wewe wenye kadi tu?
 
Hizi ni cheap politics, huwezi kutumia propaganda ya kitoto kiasi hiki, CHADEMA haijengwi kwa kuhudhuria mazishi, kuna mambo mengi ya kufanya ili kumuenzi mama Shida na sio kelele za kutumia misiba.

Viongozi wa juu wa CHADEMA walimtembelea Mama Shida pale hospital lakini hawakuona umuhimu wa kupiga picha na kuzianika magazetini kama alivyfanya JK, kwa CHADEMA ugonjwa wa mtu sio wa kujijengea kisiasa kujifanya uko karibu na watu wakati nafsi yako inakusuta kwa dhambi unazowafanyia watu
 
ni kitu ambacho akiwezekani mbowe au silaa kukutana na zito kabwe, itakuwa ni sawa na kuchanganya maji na mafuta,
 
hizi ni cheap politics, huwezi kutumia propaganda ya kitoto kiasi hiki, chadema haijengwi kwa kuhudhuria mazishi, kuna mambo mengi ya kufanya ili kumuenzi mama shida na sio kelele za kutumia misiba.

Viongozi wa juu wa chadema walimtembelea mama shida pale hospital lakini hawakuona umuhimu wa kupiga picha na kuzianika magazetini kama alivyfanya jk, kwa chadema ugonjwa wa mtu sio wa kujijengea kisiasa kujifanya uko karibu na watu wakati nafsi yako inakusuta kwa dhambi unazowafanyia watu

wewe unatapatapa nini, ukweli ni kuwa mtu kama mbowe mwenye roho ya kutu uwezi mkutanisha na zito kamwe, mbowe ni mtu wa vinyongo sana, kwanza hata wewe unayemtetea ukikaa naye vibaya anakugeuka na anakufyeka
 
Hizi ni cheap politics, huwezi kutumia propaganda ya kitoto kiasi hiki, CHADEMA haijengwi kwa kuhudhuria mazishi, kuna mambo mengi ya kufanya ili kumuenzi mama Shida na sio kelele za kutumia misiba. Viongozi wa juu wa CHADEMA walimtembelea Mama Shida pale hospital lakini hawakuona umuhimu wa kupiga picha na kuzianika magazetini kama alivyfanya JK, kwa CHADEMA ugonjwa wa mtu sio wa kujijengea kisiasa kujifanya uko karibu na watu wakati nafsi yako inakusuta kwa dhambi unazowafanyia watu
Huna hoja wewe, mbona kwenye msiba wa dada yake walifanya matangazo? Double standards. Ukweli ni kwamba hawajashiriki mazishi ya kiongozi mwenzao wa juu wa chama.walimtuma tu kimaslahi akiwa hai
 
Kama mwanaChadema..sikufurahishwa na ushiriki wa Chadema kama chama kwenye msiba wa kiongozi wa chama, pia mama wa aliyekuwa kiongozi wa chama. waTanzania hatuna hulka ya kususiana misiba...hata ukisema fulani hasije kukuzika, mara kibao tunaona anakuja na wala hufufuki kumfukuza!
 
Mama amekufa amezikwa basi!! Biashara ya kipumbavu sana kumjadili mama wa watu ambaye amepumzika katika nyumba yake ya milele.

Mbowe au Slaa siyo madaktari wala wafufuaji wa maiti.

Kuna mambo mengi sana ya kujadili, kama wizi wa bilioni 200 za escrow, bilioni 3 za Tanroads na katiba yetu, pamoja na bunge la bajeti, siyo kujadili maiti ambayo funza wameshaanza shughuli zao!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Msioelewa maana ya kifo ndio mtaangaishwa na hizi mambo.

Maandiko matakatifu yanahabari juu ya mfalme daudi ambaye baada ya kumkosea Mungu,Mungu alimuambia mtoto wake ambaye ndo amezaliwa lazima afe.

Ibrahimu akamsihi sana Mungu,kwa vilio na kujigaragaza mavumbini,na kugomea chakula.

lakini,mtoto alipofariki,daudi akaacha kulia,akaenda kuoga,akaomba apewe chakula kizuri,akala fresh.kisha akaendelea na taratibu za kumzika mtoto wake.

Hivi ndiyo namna msiba unapaswa kuchukuliwa,kulialia na kutoa malalamiko yasiyo na msingi ni ishara ya ukosefu wa busara wa hali ya juu.

Hata Kama Mbowe na slaa wangeenda kuweka kambi hospitali,kama wakati wa mama kupumzika ulikuwa umewadia,kifo kingemchukua tuu.

Hayo maradhi yaliyosababisha kifo cha huyu mama,ni maradhi yanayomsumbua bibi yangu,kwa muda mrefu sana,hajaenda india wala wapi,hositali kubwa aliyoishia ni bugando mwanza na anaendelea kuishi kijijini maisha ya dhiki kabisa. Nisemeje sasa,kwamba anabahati au nini? Tuwe makini,kama kweli ni waamini wa mafundisho matakatifu tusiwe wepesi kutangaza njaa zetu au kukumbatia shibe zetu.

Hizi propaganda ama zinatokea ccm kwa sababu zinazojurikana au zinatokea kwa wafaidika wa mapesa ya zitto,akina mwigamba and co kwa sababu zinazoeleweka pia.

Bahati mbaya,zitto naye anapenda kwelikweli kuzipamper hizi kitu.
 
Jaman mbona wanaccm mmeishiwa hoja hivi kweli swala la msiba ni la kuleta hapa jf kwelii mcba cyo siasa jaman ebu tufikiri mambo ya kureta hapa
 
Mama amekufa amezikwa basi!! Biashara ya kipumbavu sana kumjadili mama wa watu ambaye amepumzika katika nyumba yake ya milele.

Mbowe au Slaa siyo madaktari wala wafufuaji wa maiti.

Kuna mambo mengi sana ya kujadili, kama wizi wa bilioni 200 za escrow, bilioni 3 za Tanroads na katiba yetu, pamoja na bunge la bajeti, siyo kujadili maiti ambayo funza wameshaanza shughuli zao!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
Elimu yako ni kiasi gani? Kinachojadiliwa hapa ushiriki wa chadema kwenye msiba/mazishi ya mama zitto.uwe mwlewa,usijitoe ufahamu
 
Yaan unafaa uolewe maana umbeya umekutawala sana. Mtu mwenye mawazo mgando hujadili watu lakini mwenye mawazo pevu huangalia nini kinafaa kifanywe na kwa Wakati gani. Pole
 
Hii ilikuwa mbaya sana, mara zote kwenye matukio kama haya watanzania tuna utamaduni wa kuzika tofauti zetu na kufarijiana.
 
Hizi ni cheap politics, huwezi kutumia propaganda ya kitoto kiasi hiki, CHADEMA haijengwi kwa kuhudhuria mazishi, kuna mambo mengi ya kufanya ili kumuenzi mama Shida na sio kelele za kutumia misiba.

Viongozi wa juu wa CHADEMA walimtembelea Mama Shida pale hospital lakini hawakuona umuhimu wa kupiga picha na kuzianika magazetini kama alivyfanya JK, kwa CHADEMA ugonjwa wa mtu sio wa kujijengea kisiasa kujifanya uko karibu na watu wakati nafsi yako inakusuta kwa dhambi unazowafanyia watu
SUALA LA WIZI WA FEDHA TSH200BILS NI HATARI KWA TAIFA YAPO MAMBO YA MSINGI KAMA IFUATAVYO:
1. Singh Sethi wa PAP amesajiliwa Kenya Kama raia wa Afrika Kusini mwenye asili ya Asia
2. Singh Sethi wa PAP amesajiliwa Afrika Kusini Kama raia wa Kenya mwenye asili ya Asia
3. Singh Sethi wa PAP amesajiliwa Tanzania Kama raia wa Tanazani Mzaliwa wa Ruvuma
4. Singh Sethi alishirikiana na Geodion Moi mtoto wa Rais Mio kwa wizi wa US$600million na kuangusha serikali ya KANU
5. Singh Sethi ametajwa kushirikinana Riziwan (Albert Marwa) ndungu wa familia ya JK na kusababisha wizi wa Tshs200Bls
6. Mwanamke Mbunge wa UK alipambana sana kwenye Bunge la UK wakati wa wizi wa fedha za Rada ulifanyika na BAYE na hatimaye fedha zikarudi Tanzania. Serious Fraud ilikuja hapa na kuwadaka akina Chenge na wizi ule lakini CCM ikawalinda.
7. Leo UKAWA wanapewa document ya ukweli juu ya Wizi wa akina Werema na wametoka nje kushinikiza akina Eliakimu Maswi wakamatwe. Ukweli ni kwamba Benki ya Standard Chater ya UK imetapeliwa zaidi ya Tsh1770bls na Singh Sett na wenzake. Serious Fraud wapo hapa na kila kitu kinafahamika
8. Kumufukuza balozi wa UK ni sawa na kumufukuza nzi badala ya kuondoa Kinyesi.
9. Prof Muhongo na Lugora wanasema pesa Tshs200Bils sio za serikali ,Je pesa zisizokuwa za serikali zinawapa CCM kuiba??. Mbona Mbunge la UK walijadili pesa zetu na kuwataja akina Chenge hadi zikarejeshwa?? Huu ni upuuzi wa CCM na serikali yake

10. Kule Malawi watendaji wa Malawi wakiongozwa na Rais Joyce Banda waliiba Zaidi ya US$320 sawa na saidi ya Tshs 500bils wizi huo unaitwa CASHGACSANDAL na Ubalozi wa UK umesususia kutoa Misaada Malawi. Rais Mpya Peter Muthariaka ametangaza Kumushughurikia Kwanza Rais Banda na watu wake ndipo aangalie katiba.
Hapa Tanzania kuna wizi wa Escrow Scandal na Kikwete ameamua kuficha wizi huo na kufanya propaganda za msiba wa Mama Zitto kabwe(shida salumu) huku akijificha kwenye ugonjwa wa dengue na Ukawa!
CCM na watawala wachague Kuwatetea Watuhumiwa kwa malengo ya kuangusha serikali nzima au kuwashughurikia watuhumiwa na kuokoa serikali
 
Yaani watz sijui tuna laana!!??

Viongozi wa CDM hawakufanya vizuri kutoudhuria msiba wa Mama yetu, wewe umefanya vizuri kuutumia mwili wa Mama yetu kisiasa!!!??

Hivi hebu fikiria mtu kama Zitto na familia yake, bado tuko kwenye masikitiko na huzuni ya kuondokewa na Mama yetu, wewe unapata wapi ujasiri wa kuja kuuuliza maswali ya kumdhihaki Mama yetu!!? Sisi tunaomboleza wewe unauliza maswali ya Mbowe na Slaa!!? Ili roho ya Bi Shida irejee au!? Lakini yote haya ni kwasababu ya huyu mjinga anayewapa fursa ya kuuliza maswali ya kipumbavu!! Hayo ndiyo yaliyowapeleka msibani!? Hii ndiyo pole mnayotupa kwa kumdhihaki Mama yetu!!?

"POLE SANA NDUGU ZITTO NA FAMILIA KWA UJUMLA KWA KUONDOKEWA NA MTU MUHIMU DUNIANI"
 
Elimu yako ni kiasi gani? Kinachojadiliwa hapa ushiriki wa chadema kwenye msiba/mazishi ya mama zitto.uwe mwlewa,usijitoe ufahamu

Wewe ndiye unayejitoa ufahamu kwa kujadili mtu aliyekwisha kufa na kuzikwa, amepumzika tujadili mambo mengine. Kama unataka kuzikwa kwa heshima na cheni ya dhahabu shingoni nenda ccm.

Mama Shida Salum (RIP) alijua jukumu kubwa walilonalo viongozi wa chadema, siyo kushiriki mazishi tu.....

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hivi unaweza kuipenda ccm kwa hii propaganda ya mazishi mpona watanzania tunashusha uwezo kufikri hivyo, kwani CDM ndo waliimua huyo mama.
 
Back
Top Bottom