Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Mbunge Kasulumbay wafikishwa kortini

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
image.jpg Utangulizi.
kuna uchaguzi mdogo unafanyika katika kata ya Ubangwe, Jimbo la Kahama , ni uchaguzi ambao tangu awali mgombea wa Chadema aliwekewa pingamizi kuwa yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ubangwe CCM Hakuwahi kuirejesha kadi ya CCM , ila wanasheria wa Chadema walishindwa hilo pingamizi kwenye ngazi ya rufaa , tume makao makuu kwani Mkurugenzi aliamuru kumwondoa kwa hoja dhaifu kama hiyo.

kata hii kampeni zimekuwa ngumu sana kwa Magamba na hivyo;

Jana usiku majira ya saa saba na robo usiku , viongozi wa Chadema wa kanda ya Ziwa mashariki wakiwa kwenye ngome ya yao ya kampeni ndani ya kata ya Ubagwe, walivamiwa na Polisi wakiwa na magari zaidi ya saba na kuwakamata viongozi wote ambao walikuwa wamekaa kwenye eneo hilo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa kanda ya Ziwa Mashariki Mbunge SYvester Kasulumbay, na kulala za ndani hadi muda huu wa saa saba mchana leo .

baada ya kuwaweka ndani na wananchi kuonekana kuandamana kuelekea Kahama Mjini , polisi wamewafikisha mahakamani kwa MAKOSA mbalimbali yakiwemo ya kupiga na kujeruhi mwili, kuharibu mali nk. Na ndio wanasomewa mashitaka yao katika mahakama ya wilaya ya Kahama .

Hakimu wa mwanzo aliyekuwa amepangiwa kusikiliza Shauri hilo ameondolewa na kuitwa kwa dharura Hakimu mf aidha wa mahakama ya wilaya, sababu bado kujulikana , ila huenda wakanyimwa dhamana kwani inasemekana kuwa jana jioni makada mbalimbali wa CCM walivamiwa na wananchi wakati wakitoka kwenye kampeni baada ya kupaki gari Lao na kuanza kuwashambulia vijana ambao waliku na skafu za CDM ndipo wananchi walijibu kwa kuliharibu vibaya gari Lao baada cha Kuwazidi nguvu, na baadhi ya makada wa CCM pamoja na wananchi waliokuwa eneo la tukio walijeruhiwa , na kuna taarifa kuwa wapo watu sita katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu zaidi.

nitawajulisha hapo baadae , ila hii inaonyesha kuwa IGP mpya kuingia kisiasa kwani mtakumbuka kuwa juzi kule Njombe kiongozi m ja wa Chadema alishambuliwa na makada wa CCM na kuvunja taya na mpaka sasa yupo hospitali ila waliokamatwa ni viongozi na wanachama wa Chadema , .

Ijuliikane kwamba viongozi hawa walifuatwa usiku saa saba na kukamatwa tena wakiwa wamelala na hawakukamatwa kwenye eneo la tukio wala hawakuwa kwenye kijiji tukio lililotokea kwani walikuwa kwenye kampeni kijiji kingine ,

updates.
viongozi wa Chadema walifikishwa mahakamani ni 13 .....

updates ...
wamesomewa mashitaka sita , matano ni ya kujeruhi mwili na moja ni la kuharibu mali , ambalo ni kuharibu gari la CCM .
mwendesha mashitaka ametoa hati ya kiapo ya kuzuia dhamana kwa hoja kuwa majeruhi hali zao ni mbaya sana hivyo watuhumiwa wasipewe dhamana , Hakimu mfawidhi anasubiriwa ili kutoa uamuzi kama wapewe dhamana ama laa.......

UPDATES.
Baada ya maalum nao kuhusu hali za majeruhi kuwa mbaya , Mwendesha mashitaka alitakiwa athibitishe kama wana hali mbaya ama laa, akashindwa kwani hakuwa na Cheti ama taarifa yeyote ya Daktari kuthibitisha hilo.
Kuhusu hoja kuwa wakiachiwa usalama wao utakuwa hatarini,mwendesha mashitaka ametikiwa athibitishe mahakama jambo hilo na ameshindwa ,

Kesi imeahirishwa hadi kesho ambapo Hakimu atatoa uamuzi kuhusu dhamana .........na watuhumiwa wamerejeshwa rumande hadi hiyo kesho.

Updates ...tarehe 6.2.2014

Hati ya mashitaka , nimeshindwa kuiupload ......ila leo Mawakili wameshawasili mahakamani wanasubiria Hakimu ajitokeze

UPDATES
Mahakama imewapatia haki ya kupata dhamana kwa kuwa na masharti ya hati za nyumba , na tayari mchakato huo unaendelea wa kuwatoa wote waliokuwa mahabusu , hii ni baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha kuwa wagon jaw wana hali mbaya baada a kukosa hati au uthinitisho wa daktari, pongezi ziwa ended madaktari waliokataa kuandika hati za uongo .
 
Asante mkuu japo umeandika haraka.
Ukitulia tupe mkasa kamili kwa usahihi zaidi
 
Kumbe IGP mpya kaingia na Sera ya Said mwema ya kuangamiza upinzani???

nadhani tunahaki ya kuanza kujitetea
 
Policcm pamoja na kubadilishiwa lGP na waziri bado mnaendelea kutumika na maCCM?

Naomba HQ CHADEMA mwahi na CHOPA fasta hapo kahama na Njombe na wanasheria wetu wote!

MaCCM pamoja na yote ushindi ni lazma CHADEMA
 
HII nchi KIkwete ataiacha vipande vipande ni kwa nini CCM wanadhani vitisho vinaweza kurudisha nyuma hamasa ya mageuzi duh hasara tupu
 
Kumbe IGP mpya kaingia na Sera ya Said mwema ya kuangamiza upinzani???

nadhani tunahaki ya kuanza kupambana mitaani na polisi, kimya kimya tukiwashughulikia ipasavyo watatuheshimu na kuheshimu haki zetu.

Ni vema kuanzisha malipizi kwa kuwashughulikia polisi wanaporudi majumbani kwao.

ndio itkad y chama chko hYO?
 
mnazidi kutupandisha daraja chadema haki ya mtu hatapotea hawa police wa ccm wanafanya kazi kiccm wote machizi ccm hakuna msafi wote wezi wakubwa ...
 
Ajabu juu ya Ajabu............. juzi usiku vijana wa ccm walichoma nyumba ya mgombea diwani wetu, hakuna hatua zilizochukuliwa na polisi.

Nimeamini kwamba ni rahisi sana polisi kuwakamata wanasiasa wanaotokana na chadema, lakini ni vigumu sana polisi kuwakamata hata vibaka wenye element za ccm.
 
Ccm hila zenu azita wasaidia polisi tendeni haki hasa IGP usilete siasa maana watu wanazidi kuumia
 
Kwa jinsi hali inavyoanza kujionesha, utawala wa IGP Mangu unaweza ukawa mbaya na wenye maafa makubwa kuliko ilivyokuwa kwa Said Mwema. Kuna harufu na dalili za wazi za kujipendekeza, kutumiwa na kutekeleza amri za watu ama kikundi fulani ndani ya jamii yetu jambo ambalo ni la hatari sana kwa mustakabali wa Taifa na jamii kwa ujumla.
 
Ccm hila zenu azita wasaidia polisi tendeni haki hasa IGP usilete siasa maana watu wanazidi kuumia

Miaka michache iliyopita vijana wa ccm walifanya "mafunzo" Singa Chini kule Moshi. Walihutubiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa ccm, Yusufu Makamba, na Mwenyekiti wa ccm, JK.

Viongozi wote wawili waliwaambia vijana kuwa ccm lazima ishinde uchaguzi uliokuwa unakuja "kwa gharama yoyote", na hakuna wa kuwauliza "kwani serikali ni yao". Walipomaliza mafunzo walipitia KCMC. Kuna mtu alitumia uhuru wake barabarani akafanya ishara ya vidole viwili. Hao vijana walikwenda hospitalini wakapiga wafanyakazi na wagonjwa, na hakuna aliyewauliza.

Huu ndiyo msimamo wa ccm. Pale wanapozidiwa hoja hutumia fujo na mauaji, na wanasingizia wengine. Polisi hawawezi kuwauliza "kwani serikali ni yao". Tukumbuke fujo na mauaji waliyofanya ccm Arusha, Morogoro, Igunga na kwingineko "hawajaulizwa kwani serikali ni yao".

Inabidi kujiuliza kwa dhati kabisa: katika hali hii, mabadiliko ya amani yanawezekana Tanzania? Mabadiliko ni lazima; swali lililopo ni kama yanaweza kuwa ya amani kama ilivyotokea Zambia, Ghana na kwingineko.

Polisi wanaelekezwa vibaya. Ni tegemeo langu kwamba kuna siku watachoka kuonea Wananchi wenzao.

Inaweza ikawa ndoto kudhani kwamba ccm inaweza kuachia madaraka kwa mfumo wa demokrasia na amani.
 
Ajabu juu ya Ajabu............. juzi usiku vijana wa ccm walichoma nyumba ya mgombea diwani wetu, hakuna hatua zilizochukuliwa na polisi.

Nimeamini kwamba ni rahisi sana polisi kuwakamata wanasiasa wanaotokana na chadema, lakini ni vigumu sana polisi kuwakamata hata vibaka wenye element za ccm.

Mkuu Mungi hawa wanadekezwa na sisi wenyewe CHADEMA sasa nadhani inatakiwa kufika wakati tukatae kutiii amri zao,kujibu mashataka yeyote mbele ya Mahakama zao,Tukatae kuweka chini ya Ulinzi wa Jeshi la Polisi la CCM mpaka Jeshi jipya litakapoundwa na wakija kwa moto tuwajibu kwa moto jino kwajino na jicho kwa jicho kama ni ukibogoyo tufike 2015 wote tukiwa vibogoyo na kama ni upofu potelea mabali tufike 2015 wote tukiwa vipofu.Tatizo tumekuwa tuna mpa -------- jibu la kiuerevu na ndo maana wanavimba vichwa.
 
Back
Top Bottom