Viongozi wa CHADEMA wahamasishe vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,052
4,075
Uchaguzi wa mwaka huu umekosa mvuto tofauti na uchaguzi wa mwaka 2015 ukipita mitaani na vijiwe vya kahawa hapa Dar unaweza kuzani hakuna uchaguzi watu wengi wanapiga stori za Simba na Yanga tu.

Vijana wapo wengi kuliko wazee na wamama wa nyumbani vijana hawa ndio mitaji yenu CHADEMA vijana wanaipenda CHADEMA wanahitaji ukombozi lakini nimeona kuna kila dalili uchaguzi huu vijana wengi kutopiga kura.

Nimekuwa nafatilia mikutano ya mgombea wa CHADEMA nashauri viongozi wa chadema na mgombea mwenyewe wa urais Lissu kipindi watarudi kuendelea na kampeni wahamasishe vijana wajitokeze kwa wingi kupigia kura rais, wabunge na madiwani.

Pia watumie media na mitandao ilikuwafikia watu wengi siku ya mwisho watu wajitokeze kuwapigia kura.

Ni jambo jema tukapata wabunge wengi wa mpinzani ambao wataenda kusemea matatizo ya wananchi na sio kupata wabunge watakaoenda kuunga mkono juhudi.
 
Jiwe alitoa kauli mbaya sana juu ya wakurugenzi.

Nimekupa kazi.
Nimekupa Gari.
Nakupa Mshahara.
Nakupa posho.
Nakupa nyumba.

Bado unakwenda kumtangaza mpinzani kashinda iiii?
 
Hamkuenda kuboresha taarifa zenu kwenye daftari la mpiga kura!

Mwaka huu mtafurahia show ya Magu
 
Hamkuenda kuboresha taarifa zenu kwenye daftari la mpiga kura!

Mwaka huu mtafurahia show ya Magu
Na kina Kwame Nkurumah, Nelson Mandela, Nyerere na wengine wengi wangesema kutafuta uhuru ukipigwa Risasi ukafa je, si bora nikae kimya niendelee na shughuli zangu, Africa isinge kuwa hapa, jiongeze wewe kiumbe dhaifu acha mawazo uchwara ya kiccm ccm..
 
Hamkuenda kuboresha taarifa zenu kwenye daftari la mpiga kura!

Mwaka huu mtafurahia show ya Magu
Rais alihamasisha vyama vyote vihamasishe wanachama wao waende CHADEMA wakapinga.Sasa vijana wengi wanajaa mikutano yao zoezi la kuboresha hawakwenda walifurika ofisi za NIDA tu kutafuta vitambulisho vya taifa!!! wengi wana vitambulisho vya Taifa tu na walifurika kwa lazima baada ya kuambiwa simu isiyosajiliwa kwa kitambulisho cha taifa itazimwa

Wengi hawana vitambulisho vya kupiga kura.CHADEMA ilichemka sasa wanakumbuka shuka kukiwa kumekucha.Maafisa wa kuboresha taarifa walikuwa hadi wanasinzia sehemu zingine kwa kukosa watu ukiona wamefurika walikuwa wa CCM waliohamasishwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM kuwa watu wangu wote nendeni mkajiandikishe

Vijana wengi wanaofurika mikutano ya Lissu hawana kitambulisho cha kupiga kura ila cha uraia hapo hapo hata uwaambie wakuonyeshe watakinyanyua juu
 
Kuna vitu huwa nazidi kushangaa tu, kipindi cha kujiandikisha walibeza sana hilo zoezi na kusema hakuna umuhimu wa watu kujiandikisha ikiwa mshindi tayari anajulikana na mwisho kabisa wakafurahi muitikio wa watu kidogo kwenye kujiandikisha.
Sasa hivi watawezaje tena kuwahamasisha wakapige kura ikiwa hawakujiandikisha?
 
Ni kiongozi gani wa CHADEMA aliyebeza watu wasiende kujiandikisha? una uhakika gani watu hawaja jiandisha
 
Hamkuenda kuboresha taarifa zenu kwenye daftari la mpiga kura!

Mwaka huu mtafurahia show ya Magu
Mtu aliyejiandikisha 2015 anaenda katika kituo alichojiandikishia na kupiga kura. Sio lazima awe ameenda kuhakiki.
Yule aliyehama eneo ndiye hasa alipaswa kwenda kuhakiki na kubadili kituo.
Kwa hiyo wenye kadi ya mpiga kura 2015 wataenda kituo walichopigia hata kama hawakuhakiki

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Rais alihamasisha vyama vyote vihamasishe wanachama wao waende CHADEMA wakapinga.Sasa vijana wengi wanajaa mikutano yao zoezi la kuboresha hawakwenda walifurika ofisi za NIDA tu kutafuta vitambulisho vya taifa!!! wengi wana vitambulisho vya Taifa tu na walifurika kwa lazima baada ya kuambiwa simu isiyosajiliwa kwa kitambulisho cha taifa itazimwa

Wengi hawana vitambulisho vya kupiga kura.CHADEMA ilichemka sasa wanakumbuka shuka kukiwa kumekucha.Maafisa wa kuboresha taarifa walikuwa hadi wanasinzia sehemu zingine kwa kukosa watu ukiona wamefurika walikuwa wa CCM waliohamasishwa na wajumbe wa nyumba kumi wa CCM kuwa watu wangu wote nendeni mkajiandikishe

Vijana wengi wanaofurika mikutano ya Lissu hawana kitambulisho cha kupiga kura ila cha uraia hapo hapo hata uwaambie wakuonyeshe watakinyanyua juu
Bado wengi hawana kitambulisho cha uraia na wengi wana cha mpiga kura. Ugumu wa kupata kitambulisho cha uraia uliwafanya vijana watafute cha mpiga kura.
Hivyo wakapige kura walikojiandikisha 2015

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom