Viongozi wa CHADEMA 'wadanganya': Mh. Lissu atofautiana na 'uongozi' wa CHADEMA Singida.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Uwongo hata siku moja hauwezi kupambana na ukweli pamoja na kwamba uwongo hupanda lift na ukweli hapanda ngazi.

Maelezo ya Mh. Lissu yalipanda lift na kutuaminisha mapema kuwa alichokisema kilikuwa ni kweli lakini ukweli baada ya kupanda ngazi umetufikia na sasa tunaweza kwa uhakika kusema, baadhi ya hawa viongozi wa CHADEMA ni waongo na wazandiki kama maelezo yao yalivyotofautiana.

Ni nani hapa anasema ukweli?.

Maelezo ya hoja ya ofisi ya CHADEMA Mkoa.
Wilfred N. Kitundu
Nimekuwa nikijitolea vya kutosha nguvu, muda na akili zangu nyingi kukijenga na kukilinda chama hiki mpaka sasa mkoa wetu wa singida umepata wabunge watatu mmoja wa kuchaguliwa na wawili wa viti maalum.
Tangu mwaka 1992 mpaka 2011, chadema imekuwa ikitumia nyumba yangu kama ofisi, nimekuwa nikifanya hivyo kama kielelezo change cha kudai na kupigania demokrasia ya kweli ndani ya nchi kwa kuijenga CHADEMA imara.

Mh. Tundu Lissu.
Wilfred Kitundu is probably the longest serving regional chairman wa CHADEMA katika nchi hii. Na ni kweli, Kama anavyosema, kwamba kwa muda wa karibu miaka ishirini ya uenyekiti wake, sebule ya nyumba yake ilikuwa ndio Ofisi ya chama ya Mkoa. Which is another way of saying, kwa miaka yote hiyo, chama hakikukua.
On the other hand, zaidi ya kutuwekea Ofisi ya Mkoa sebuleni kwake, sidhani kama Mzee Kitundu ametoa mchango mwingine wowote katika mafanikio haya.

Shaban Lyimo (Kaimu Mwenyekiti wa Mkoa) na Patrick Msuta (Katibu wa Mkoa)
Ndugu waandishi wa habari, wanachama na viongozi wa CHADEMA, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amedai kuwa tangu mwaka 1992 hadi 2011 chama kimekuwa kikitumia nyumba yake kama ofisi ya chama. Jambo hili si la kweli kwani kumbukumbu zetu zinatunyesha kama ifuatavyo:-
1.Mwaka 1992 hadi 2000 ofisi ya CHADEMA ilitolewa na Mzee KALALU ambaye kwa sasa ni marehemu. Wakiti huo mzee Wilfred Kitundu alikuwa Mwenyekiti.
2.Mwaka 2000 hadi 2004 ofisi ya chama aliitoa mwanachama wetu alimaarufu MAMA VERO. Kwa kipindi hiki chote yeye hakuwa mwenyekiti wa chama bali mwenyekiti alikuwa ndugu NATANIEL MPANYA. Kwa hiyo sikweli kwamba yeye amekuwa mwenyekiti toka 1992-2013.
3.2000 aliondolewa kwenye uongozi kutokana na kudharau kikao cha uongozi mkoa hivyo aliondolewa kwenye uenyekiti kabla ya kuomba kugombea tena mwaka 2004.
4.2004 aliomba kugombea uenyekiti akapitishwa bila kupingwa kwani hakuwa na mpinzani na mwaka 2009 akagombea tena ambapo muda wake ulipaswa kuisha mwaka 2014 mwaka kesho. Kwahiyo kuanzia mwaka 2004 – 2011 ndipo ofisi ilihamia kwenye chumba cha sebule yake.

Kwahiyo si kweli kwamba yeye amekuwa ndiye mwenyekiti tangu 1992 – 2013 kama alivyosema kwenye taarifa yake.

Kufanya kampeni na mikutano.
Wilfred N. Kitundu
yeye ni kinara sana wa kumshambulia zitto kwenye hili, lakini ninasikitika kusema kuwa Tangu nimekuwa mwanachadema na Tangu nimemfahamu Lissu alipohamia CHADEMA hajawahi kufanya mkutano hata mmoja wa kujenga chama ndani ya mkoa wa SINGIDA ukiondoa jimboni kwake. Tumemuona Zitto akitoka bungeni na mara nyingine hata kigoma kuja kufanya mikitunano maeneo mbali mbali hapa singida ikiwemo iramba, singida mjini na kwingineko, na mtakumbuka zitto amewahi kukamatwa na polisi mkoni singida akikinadi chama, hakuwa lissu. Sasa leo anapotoka mbele na kujinadi kuwa ana mapenzi mazuri na chama kushinda zitto kabwe ni upuuzi unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa sana.

Mh. Tundu Lissu.
CHADEMA imekuwa sana katika Mkoa wa Singida tangu 2010. Kwa kiasi kikubwa, pengine kuliko mtu mwingine yeyote katika Mkoa wetu, ni mvamizi na mhamiaji Tundu Lissu. I can say with a straight face kwamba Jimbo pekee ambalo sijawahi kufanya mikutano ya hadhara ni Iramba Magharibi. Mengine yote nimefanya mikutano ya hadhara hata kabla sijawa Mwenyekiti wa M4C Kanda ya Kati.

Shaban Lyimo (Kaimu Mwenyekiti wa Mkoa) na Patrick Msuta (Katibu wa Mkoa).
1. Mh Lissu alianza kazi ya ujenzi wa chama mkoani Singida tarehe 4,January 2008 katika jimbo la SINGIDA KUSINI likiwa na jumla ya kata 26 na vijiji 104 kabla ya kugawanywa na kupata majimbo ya
(i) SINGIDA MASHARIKI
(ii) SINGIDA MAGHARIBI

Maelezo yote yanapatikana katika thread hizi hapa,
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ida-ajiuzulu-adai-kamati-kuu-ni-wanafiki.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ibu-aliyekuwa-mwenyekiti-mkoa-wa-singida.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ililotolewa-na-aliyekuwa-mwenyekiti-mkoa.html
 
Chadema ni chama cha ulaghai pamoja na magumashi siwezi kulaumu hawa wanafuata Dr.Slaa.
 
Vipi mkuu, hii ajira yenu inalipa kweli? Maana naona mnataka kufia kwenye mitandao wewe na mkeo Simiyu na ZeMarcopolo!! Msalimieni mwajili wenu Mwanadiwani..
 
Maelezo yana tija gani kwa taifa
Huwezi kufahamu kama huyafahamu uwongo na uzandiki una maana katika mstakabali wa taifa.

Taifa linaloongozwa na viongozi waongo na wazandiki ambalo wanaongopa ili kutimiza matamanio yao ya kupewa dola ni kama taifa linalojongea kifo katika nyanja za kisiasa, kiuchumu na kijamii.
 
Mfanye nini wewe na nani?. Jisemee mwenyewe!.

Inaonyesha wewe naye umechoka kweli kama sura ya bibi yako, ona maelezo kibao hayAna hata tija: Badala ulete uchambuzi makini ya kuhusu rasilimali zA taifa letu zinavyotapanywa na mafisadu wewe unaleta umbea usiokuwa na madhara yoyote hapa.shenzi sana wewe
 
Tunashukuru sana kwa uchambuzi huu ambae msomi yeyote mwenye kutaka uchambuzi makini ataukubali. Tatizo ni kwamba wa Tanzania wengi siku hizi wanapenda kudangnywa na propaganda. Simfahamu aliyechambua hizi documents lakini anaweza kuwa mwanasheria mzuri
 
kwa kweli kupenda ni upofu_maelezo (information) havina tija kwa Taifa? vikao ni kwa ajili ya nini sasa? usichangie kama muda na ufaham wako havijawa sawa

Hiki chama hakina mikutano ya ndani? Mambo ya kusema ofisi ilikuwa sebule ilitakiwa kuzungumzwa kwenye vikao vyao..sisi wanatakiwa kutupa reports za maendeleo, plan(s) kwa kile wanacjopanga kufanya miaka ijayo pia wakipewa nchi leo hii nini watafanya....wananchi tunahitaji sana information lakini sio kila information inatakiwa kuwa published.

Mfano mzuri ni ukiwa na familia yako, watoto gawahitaji kusikia nini mnafanya chumbani, wanataka kujua mnatimizaje mahitaji yao...same apply kwa taifa..wananchi wanahitaki kujua viongozi wao wanawajibikaje katika nyadhifa walizowakabidhi
 
Inaonyesha wewe naye umechoka kweli kama sura ya bibi yako, ona maelezo kibao hayAna hata tija: Badala ulete uchambuzi makini ya kuhusu rasilimali zA taifa letu zinavyotapanywa na mafisadu wewe unaleta umbea usiokuwa na madhara yoyote hapa.shenzi sana wewe
Jadili hoja na siyo kujadili mleta hoja.

Kama huna hoja ya kuandika basi hata kutokuandika chochote nayo ni aina mojawapo katika kujadili hoja.

Are you fighting internal multi-inferiority complex?. Dawa yake ni kujenga hoja mbadala!
 
Hiki chama hakina mikutano ya ndani? Mambo ya kusema ofisi ilikuwa sebule ilitakiwa kuzungumzwa kwenye vikao vyao..sisi wanatakiwa kutupa reports za maendeleo, plan(s) kwa kile wanacjopanga kufanya miaka ijayo pia wakipewa nchi leo hii nini watafanya....wananchi tunahitaji sana information lakini sio kila information inatakiwa kuwa published.

Mfano mzuri ni ukiwa na familia yako, watoto gawahitaji kusikia nini mnafanya chumbani, wanataka kujua mnatimizaje mahitaji yao...same apply kwa taifa..wananchi wanahitaki kujua viongozi wao wanawajibikaje katika nyadhifa walizowakabidhi

wakataze sasa viongozi wako, kaka!
 
Huwezi kufahamu kama huyafahamu uwongo na uzandiki una maana katika mstakabali wa taifa.

Taifa linaloongozwa na viongozi waongo na wazandiki ambalo wanaongopa ili kutimiza matamanio yao ya kupewa dola ni kama taifa linalojongea kifo katika nyanja za kisiasa, kiuchumu na kijamii.

uwongo si jambo jema lkn tunatafuta uwongo ktk very cheap things, tupeni taarifa za uwongo zinazotolewa na watawala kama kuambiwa elimu bure, afya bure mapato kwenye raslimali za nchi n.k
 
Back
Top Bottom