Viongozi wa CHADEMA Taifa mna uhakika kesho ofisi za Tume ya Uchaguzi zitafunguliwa?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,379
2,000
Kwakuwa kesho ni sikuku ya Nanenane (Public holiday), ofisi za serikali/ umma huwa hazifunguliwa isipokuwa kwa baadhi tu ya ofisi au Taasisi ambazo kulingana na nature ya kazi zao,ofisi zao huwa hazifungwi.

Kwa msingi huo, NEC kesho watafungua ofisi zao?

Au katika ratiba waliyotoa ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu(kama ipo) ,siku ya kesho ni moja ya Siku za kutoka na kupokea fomu za wagombea?

Nawashauri CHADEMA watoe maelezo au ushahidi walionao kabla ya kesho unaoonyesha kuwa NEC kesho watafungua ofisi/wamepanga/wanapaswa kufungua ofisi ili lolote likitokea,tuwe na hoja za kusema /kujibu vinginevyo itakuwa vivyo sivyo.

Sitaki kuamini CHADEMA watakuwa wame-overlook hili jambo, bali naamini watakuwa wana uhakika kuwa kesho NEC wanatakiwa kuwa ofisini, ila kutokana na siasa zetu , lolote bado linaweza kutokea, hivyo ni bora kuwawahi kwa kuweka hadharani maelezo /ushahidi wa Tume kesho kutakiwa kufungua ofisi either kwa mujibu wa sheria na taratibu za NEC au kulingana na NEC wenyewe walivyopanga.

Wanaweza kupanga kufungua ofisi hiyo kesho, ila bado wanaweza kusema walipitiwa kuwa kesho sio siku ya kazi alafu tukajikuta tunaanza mjadala mpya juu ya tukio hilo.

In short,hapa na-suggest tufanye kitu ambacho ni pre-emptive, ili lolote likitokea,tuwe kwenye safe side.
 

Ngatele

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
712
1,000
Nafikiri walitoa utaratibu na tarehe za kuchukua form na pia kama sikosei vyama vilitakiwa kufanya bookings za tarehe wanazotarajia kwenda and therefore hiyo siku iko kwenye mpango wa uchaguzi.

Ila CHADEMA wanapaswa kuzikagua hizo forms ktk bag kama zipo copies zote wanazosema na kama zina pages kamili. Sina hakika kama ukizikuta zina makosa au pages hazijatimia inakuwaje na kama zina initials za viongozi wa Tume kwa kila page!?
 

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
3,299
2,000
Mi naamini ni mipango, siasa ni kutengeneza matukio ili uendelee kupigiwa promo na kuzungumzika.

So, kwa mimi bado nawasifu. Wanaendelea kucheza karata zao vema.

Ningetegemea tume ya uchaguzi kusema kwamba hawatakuwepo, ila kukaa kwao kimya ina maana wamepoteza mpambano kwenye hii issue.

Bado naamini CHADEMA ni chama makini kimkakati
 

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
8,877
2,000
tokea walipotangaza tarehe 8 mwezi wa 8 ndio wataenda kuchuka fomu nikajua fika kabisa hiki chama menejiment yao iko very week, 88 ni public holly day na ofisi ya tume ni ofisi ya umma.
Huenda wana uhakika siku hiyo NEC watafanya kazi kama kawaida.
CHADEMA watakuwa wamefanya hivyo kwa kulenga kupata watu wengi ambao wataenda kuhudhuria tukio sababu watakuwa mapumziko hawaendi kazini.

Mwajiriwa wa mkoa wowote anaweza kuwahi tukio DOM.
 

Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
8,165
2,000
Mi naamini ni mipango, siasa ni kutengeneza matukio ili uendelee kupigiwa promo na kuzungumzika.

So, kwa mimi bado nawasifu. Wanaendelea kucheza karata zao vema.

Ningetegemea tume ya uchaguzi kusema kwamba hawatakuwepo, ila kukaa kwao kimya ina maana wamepoteza mpambano kwenye hii issue.

Bado naamini CHADEMA ni chama makini kimkakati
Tume ya taifa ya uchaguzi haifanyi hiyo michezo ya kitoto
 

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
2,986
2,000
Huenda wana uhakika siku hiyo NEC watafanya kazi kama kawaida.
CHADEMA huenda wamefanya hivyo kwa kulenga kupata watu wengi ambao wataenda kuhudhuria tukio sababu watakuwa mapumziko hawaendi kazini.

Mwajiriwa wa mkoa wowote anaweza kuwahi tukio DOM.
maybe naomba iwe hivyo maana kiw kinyume ofisi zisipokuwa wazi hapata tosha hapa kesho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom