Viongozi wa CHADEMA mkoani Shinyanga wakosa mvuto bali chama kimebaki mioyoni mwa watu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CHADEMA mkoani Shinyanga wakosa mvuto bali chama kimebaki mioyoni mwa watu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, May 30, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hakuna wakati mgumu sana kama kipindi hiki kwa chama cha CDM kujiimarisha na kujieneza nchi nzima huku kikikabiliwa na changamoto nyingi.Inahitajika umakini wa hali ya juu ili kuzidi kuimarisha nguvu ya chama kwa wanachama wake na wasio wanachama wake ili kupata support ya wananchi katika kushika dola.

  Changamoto alizoziacha hayati Philip Magadula Shilembe mkoani Shinyanga imepelekea wananchi kukatishwa tamaa na aina ya viongozi waliopo hivi sasa.Iko wapi ile CDM ya vitendo katika kumkomboa mwananchi wa kawaida kutokana na lindi la umasikini uliokithiri.

  Hatukupenda nafasi hii ya mwenyekiti wa mkoa wa Shinyanga iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha marehemu Shirembe iendele kukaimiwa kwa muda mrefu bila ya kupata mtu wa kuijaza nafasi hiyo.Uoga wa viongozi waliopo kwa sasa unatia shaka katika harakati za ukombozi ambazo zimeshika kasi nchi nzima.

  Ile imani ya wananchi iliyojaa ndani ya mioyo yao imeendelea kutoweka kutokana na viongozi walioko kushindwa kupatia uvumbuzi wa matatizo yanayo wakabili wananchi.Mbona hatuoni harakati zile alizotuachia marehemu huyu.

  Tuna muenzi vipi Shirembe,ilihali uoga haukuwa itikadi yake.Alikubali kuwafia wananchi kuliko kuona watu wake wananyanyasika bila sababu za msingi.Tunaiomba ofisi kuu ya CDM kulimulika tatizo la kichini chini ambalo linaweza kuwa ni bomu hatari ndani ya CDM kwa siku zijazo.Kuna majungu ya chini chini ambayo chama kisipokuwa makini historia ya vyama vya upinzani kuwa wasindikizaji wa CCM itajirudia.

  Mwisho, mapinduzi ya kweli yataletwa na wale walio kubali kuvua gamba la uoga na kuvaa ujasiri katika kuwatetea wananchi na rasilimali za nchi.Silaha hii ya uoga ndiyo silaha duni iliyotumika kuangamiza vyama ambavyo vilionekana kuwa vyama mbadala wa CCM.Hatutaki CDM hoya hoya shati begani,tunataka chama makini chenye malengo madhubuti wakiongozwa na makamanda makini wasio ogopa dhoruba na rasha rasha za mfumo wa kimangimeza.
   
 2. M

  Molemo JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Jitose mkuu kugombea maana muda si mrefu Filimbi itapigwa
   
Loading...