Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Viongozi na wanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Pwani wamezuiwa na jeshi la polisi kwa saa kadhaa wakati wakielekea mkoani Morogoro kuhudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuimarisha chama.
Viongozi hao kutoka mkoani Pwani wakiongozwa na katibu wa kanda ya Pwani wa chama hicho wamesema wamelazimika kusimamishwa na jeshi la polisi na kuhojiwa kwa saa kadhaa huku wakisindikizwa na jeshi hilo kutoka mkoani Pwani hadi Morogoro.
Akizungumza na wajumbe wa mafunzo hayo, mjumbe wa kamati kuu taifa ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Morogoro Suzan Kiwanga amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakiwadharau wanachama na kwamba kufanya hivyo kunahatarisha safari yao ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.