Viongozi wa CHADEMA chukueni hatua, acheni kupuuzia haya mambo kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CHADEMA chukueni hatua, acheni kupuuzia haya mambo kabisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JATELO1, Oct 23, 2012.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Habari ya ADC kutumia bendera yenye rangi karibia sawa na CHADEMA si jambo la kupuuzia hata kidogo. Hili jambo viongozi wetu wa CHADEMA wanalichukulia kimzaa mzaa kweli na kejeli nyingi sana bila kujaribu kufikiria madhara ya MUDA MREFU ya Bendera ya ADC na hizo alama sasa wanazotumia kama CHADEMA. CHADEMA tunasahau kitu cha msingi sana kwamba Chama ili kishindi ni lazima kiwe kimejijenga hasa maeneo ya VIJIJINI. Na unapofikiria hilo la kujijenga vijijini, huna budi kufikiria aina ya watu wanaoishi kwenye mazingira husika. Je ni watu ambao uelewa wao uko kwa kiasi gani? je wana access na TV ili kuweza kutofautisha vyama kwa kiasi gani? Je, ni wangapi wenye uwezo wa kusoma vizuri?

  Nikirudi nyuma kidogo, nakumbuka moja kati ya malengo ya OPERESHENI SANGARA na sasa tuna M4C ni kuwafikia wananchi katika maeneo yale hasa ya vijijini ambapo chama chetu cha CHADEMA kilikuwa hakijafika. Ndiyo maana kila M4C inapofanya mikutano yake, wanachama wanapokelewa, Ofisi zinafunguliwa, na Viongozi wa muda wa tawi wanachaguliwa. Lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kwamba chama kinasimama maeneo ya vijijini ili kuweza kuipa chama uwezo wa kuja kuchukua nchi hapo 2015.

  Sasa basi ili malengo hayo yafanikiwe, ni lazima CHADEMA ifikie kipiindi itambue hali ya watu ambao chama kinataka kuwekeza kwao, ili chama kiweze kupanga mikakati/strategies sahihi kwa ajili ya shughuli hiyo. Mimi naamini kwamba kadri CHADEMA wanavyojipanga kwa mikakati mbalimbali ili kuweza kujijenga, ni wazi kwamba CCM nao wanajipanga kwa mikakati mbalimbali ili kukimaliza au kukipunguza nguvu CHADEMA. Na katika mikakati hiyo mingi ya CCM, ADC ilianzishwa tena haraka sana na kuna taarifa zisizo rasmi kwamba viongozi wa CCM waliwahamasisha wanachama wao katika mikoa mbalimbali wajiunge na ADC ili kufanikisha usajili wake mapema.

  Naomba niwaambie viongozi wangu wa juu wa CHADEMA kwamba,
  1. Rangi ya bendera ADC siyo bahati mbaya kama mnavyoendelea kupuuzia jambo hili siku zote, japo msajili wa vyama alikwisha weka wazi kwamba iwapo CHADEMA italalamika, basi ADC watalazimika kubadili rangi yao. Pamoja na Msajili kusema hilo jambo, mpaka sasa hatujasikia hatua yoyote iliyochukuliwa na CHADEMA juu ya rangi ya bendera ya ADC. Wengi wetu, tena wale wenye access ya internet na media mbalimbali tukiendelea kuwadanganya viongozi wetu kwamba hakuna haja ya kuchukua hatua kwani CHADEMA ipo kwenye mioyo ya watu. Nasema huku ni kujiliwaza katika mapungufu bila kuchukua hatua, kwani kushindwa kuchukua hatua sasa, itakuwa na madhara makubwa sana kwa CHADEMA na hatima yake hapo mwaka 2015.

  CHADEMA lazima tufikie kipindi tuelewe kwamba rangi ya bendera ya ADC na hata sasa alama ya V wanyaotumia vimelenga tu kuwachanganya wananchi hasa wale wa vijijini ambao wengi wao wanaangalia rangi ili ADC waweze kugawa kura za CHADEMA hasa maeneo ya vijijini wakati CCM ikipeta.

  2. Rejea kauli ya kwanza ya viongozi wa ADC baada ya kupata usajili wa muda kwamba ADC imelenga kuvunja nguvu ya CHADEMA. Hii kauli iliyoletwa hapa JF na ndugu Hasan124 na hata kwenye media iliandikwa haikutoka kwa bahati mbaya kama viongozi wetu wa CHADEMA wanavyotaka tuamini tu kwamba huu ni upepo utapita na hauna madhara kwa CHADEMA. Kwanini tusijulize ni kwanini chama kipya cha siasa kianzishwe tena kwa muda mfupi na kitangaze vita na chama kingine cha upinzani, tena ambacho hakina Dola na kina wabunge wachache wa kuchaguliwa? Kwanini ADC ilenge kuvunja ngome ya CHADEMA ambacho hakina dola na hakina habari na CCM chenye Dola? Naomba niwaambie viongozi wangu wa CHADEMA kwamba ADC ni moja ya mikakati ya CCM kama ilivyo kwa V4C ya CUF ili kuweza kuwachanganya wananchi na kupambana na CHADEMA na si chama tawala CCM. ADC na CUF kupitia V4C kwa pamoja vinafadhiliwa na CCM kwa ajili ya kukipunguza nguvu CHADEMA ili CCM iweze kushinda uchaguzi mwaka 2015.

  3. Jana kuna mtu mmoja kasema hapa kwamba ADC katika jimbo la Kigoma Kaskazini kuna bendera nyingi sana karibia kila mahali. Hivi ni kwanini katika Jimbo la Mbunge wa CHADEMA kuwe na bendera nyingi sana? Hapa kuna maswali ya kujiuliza na ukirejea matamshi yaliyotolewa na mbunge wetu kuhusu nafasi ya kugombea mwaka 2015. Lakini pia rejea makala ya kwenye magazeti na facebook ya wale wote ambao kwa kiasi fulani hawako na uongozi wa juu wa CHADEMA pamoja.

  Katika haya mazingira, ni lazima viongozi wetu wa CHADEMA wachukue hatua hasa Rangi ya bendera ya ADC na mengineyo. Vinginevyo, asijetokea mtu wa kulaumiwa baadaye wakati mambo yako wazi mapema na bado kuna nafasi ya kuyarekebisha.

  WITO WANGU KWA VIONGOZI WA CHADEMA ni kuchukua hatua na kuacha kupuuzia hii mianya ambyao inadhoofisha chama hasa maeneo ya vijijini. Na hapo ADC haijaenda mikoa mingine kama Lindi, Mtwara, n.k.
   
 2. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Team nzima ya CHADEMA ninaiamini. Wanafanyia kazi suala hili. Si watu wa kukurupuka.
   
 3. S

  Shamwile Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja hili si jambo la kupuuzia ni vizuri hoja hii ikajadiliwa ktk vikao vya juu vya chama.
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  John tendwa ndio wa kulaumiwa kwa hili!
   
 5. commited

  commited JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2012
  Joined: Feb 27, 2012
  Messages: 1,617
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jambo la muhimu sana hili, kamanda mbowe, slaa, mnyika, mwanasheria tundu lissu, mabere malando na prof safari tafadhali lifanyieni kazi hili, msipuuze mabo tafadhali, hivi kwanini hapo kigoma kaskazini hizo bendera zipo kibao... Timueni huyo zana za kilomo mapema, wanachi watamsahau mapema tu hata kabla ya 2013 kwisha, tuanze upya jamani huo jamaa hajifunzi ni karoho ka madaraka na masifa tu, sasa kazi hakafanyi kenyewe kako bizo na misafara ya jk, kanawaza uraisi, sijasikia hata kapo kata yoyote ambako uchaguzi unafanyika, kameshalewa pesa za barrick hako fukuzia mbali pllllzzz
   
 6. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  kwa nini ..wakati keshatoa fursa mwenye malalamiko ayafikishe kwake naye atayafanyia kazi
   
 7. s

  swrc JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sidhani kuwa ipo haja ya kumuandama sana huyo mbunge wa cdm ambaye bendera za adc ziko nyingi kwake. Tuache demokrasia ifanye kazi yake. KUmuandama kiasi hiki ni kuzidi kumpa umaarufu ambapo ni sawa na kumpiga teke chura. Ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kuvumiliana.
   
 8. m

  mbayaaa Senior Member

  #8
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lisemwalo lipo kama halipo lipo njiani linakuja. Makamanda fungueni macho.
   
 9. M

  Molemo JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja,viongozi wachukue hatua sasa.
   
 10. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  angalizo zuri saana tena linahitaji umakini mkubwa chadema kuweni macho na hili
   
 11. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133
  Ukweli ni kuwa lengo lao kubwa ni kutaka kuwachanganya wananchi kwani Rangi zile zinafanana kabisa kwa mtu wa kijijini ni vigumu kuzitofautisha. Viongoozi chukueni hatua HARAKA.
   
 12. o

  okon JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2012
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 305
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wewe ni genius wa masuala ya siasa!
   
Loading...