Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,130
Hivi leo huko Kenya wananchi wa Kenya wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ikiwemo kumchagua Rais wa nchi hiyo atakayedumu kwa kipindi cha miaka 4 hadi mwaka 2021.
Katika uchaguzi huo kuna mchuano mkali sana kati ya Uhuru Kenyatta wa Jubilee na Raila Odinga wa NASA.
Hata hivyo kuna kitu nilichokishuhudia leo ambacho huwa hakitokei huku kwenye uchaguzi wetu huku Tanzania.
Katika hotuba aliyoitoa asubuhi ya leo, Rais anayemaliza muda wake Uhuru Kenyatta alitoa hotuba ya hekima mno alipowahamasisha wakenya wote wenye haki ya kupiga kura wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kuwachagua wagombea watakaowaona wanafaa kuliongoza Taifa lao kwa kipindi cha miaka 4 ijayo,na kilichoonyesha kuwa demokrasia ya Kenya imekua sana ni pale Uhuru Kenyatta aliposema kuwa atayapokea kwa mikono miwili matokeo yoyote yatakayopatikana kwenye uchaguzi wa leo, hata kama atakayeshinda ni mgombea toka chama cha NASA, Raila Odinga.
Vile vile nilimsikia pia Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto naye wakati anapiga kura kwenye kituo chake cha kuoigia kura, alipohojiwa na waandishi wa habari naye akasema atayapokea matokeo yoyote ya leo kutokana na matakwa ya wapiga kura wa Kenya, hata kama wananchi watakuwa wameamua kuchagua Muungano wa NASA.
Nasema hizo kauli za wagombea hao 2 kutoka chama kilichoko madarakani hivi sasa, ni lazima ziwe mfano na kuigwa na wenzao wa CCM.
Tulishuhudia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wagombea wote 2 wa nafasi ya Urais, JPM na mwenzake
Shein wa Zanzibar, walipohojiwa na waandishi wa habari ili kueleza msimamo wao ikiwa watakubali matokeo iwapo watakuwa wameshindwa uchaguzi huo, waligoma kujibu kuwa watakubali matokeo hayo na badala yake wakasema wao ni lazima watashinda!
Tujuavyo ni kuwa watu wawili mnaposhindana ni lazima atapatikana mshindi na mshindwa.
Na vile vile kuna msemo unaosema asiyekubali kushindwa siyo mshindani.
Kwa hiyo kwa kitendo cha wagombea wote 2_kwa tiketi za CCM yule wa Urais wa Jamhuri na yule wa Zanzibar, kugoma kukiri kuwa watayapokea matokeo hata kama ikiwa wao watashindwa ni dhahiri kuwa kumbe CCM huwa wanashinda kwa goli la mkono kwa maana ya kuwa kura zinapokuwa hazijatosha huwa wanalazimisha zitoshe!
Ni vyema kwa mfano ulioonyeshwa leo na wagombea,wa Jubilee, Uhuru Kenyatta na Wiliiam Ruto kwa kutamka hadharani kuwa iwapo watashindwa kwenye uchaguzi wa leo watskabidhi kwa amani kwa viongozi watakaoshinda, mfano huo pia uonyeshwe na viongozi wa CCM watakaosimama kwenye uchaguzi wa 2020, yaani kwa Urais wa Jamhuri ya Tanzania na yule wa Zanzibar wakatamka kabla ya siku ya kupiga kura kuwa matokeo yoyote yatakayotokea watakuwa tayari kuyapokea na watakabidhi kwa amani kwa viongozi watakaokuewa na kupewa riidhaa na wananchi kuliongoza Taifa letu.