Viongozi wa CCM na Serikali sasa jino kwa jino kuonyeshana Ubabe

kanga

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
1,025
493
CCM yapinga maagizo ya DC


na Victor Eliud, Geita


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, Joseph Musukuma, amepiga marufuku utaratibu wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Omary Mangochie, wa kuwazuia wafanyabiashara kufunga maduka siku ya Alhamisi na kuyafungua saa nne asubuhi kwa ajili ya kufanya usafi katika maeneo yao.

Musukuma alitoa agizo hilo jana wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali na kuwawajibisha viongozi wanaokosa uadilifu kwa kula fedha za umma ambapo alitoa ruhusa kwa wananchi wa mkoa huo kufungua biashara yao siku hiyo.
"Kuanzia leo mimi kama Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita na kwa rungu nililopewa na chama natangaza rasmi kuanzia leo hakuna cha ‘Mangochie Day' hapa, hiyo kazi waachiwe mabwana afya tumewaajiri kwa kazi hiyo… mtu akikusumbua kwamba umefungua duka leo siku ya usafi nipigie simu nidili naye," alisema.
Kauli hiyo ilionekana kuwafurahisha wananchi wengi hivyo walijikuta wakishangilia kwa kumuita ‘jembe…..jembe…'
Kwa upande wake, mkuu wa wilaya hiyo, alilaani kitendo cha mwenyekiti huyo kuingilia madaraka hayo bila makubaliano na kusema huo si uongozi bali ni ubabe, kwani hatua hiyo ililenga kuhakikisha mji wa Geita unakuwa katika mazingira safi.
"Nimeshangazwa na taarifa hiyo; huyu mwenyekiti anasumbuliwa na utoto, hiyo siyo akili ya kiongozi mwadilifu. Wewe utazuiaje mipango ya serikali kwa katiba ipi na utaratibu upi, kwa mujibu wa katiba kwa nafasi yake hana mamlaka ya kuzuia huo mpango," alisema Mangochie.

MY TAKE:CCM kusimamia serikali bila busara italeta madhara makubwa kama juhudi makusudi ya Mwenyekiti wao Kikwete hatachukua kuwadhibiti hawa wenyeviti wa CCM.

 
wanaanza kujikanyaga wenyewe! DC kilaza, mwenyekiti kilaza!! what next kama siyo kukwaruzana kusiko na msingi? kila mtu anataka ajione yupo juu...poor ccm!!
 
DC ni mwenyekiti wa kamati ya CCM wilaya..haya ndio matatizo,mtu ni mtumishi wa serikali hapohapo ana cheo cha kichama.
 
Patamu hapo ngoja hao makatibu wa mikoa wa CCM walioitwa Dar na Muuzaji wa Pembe za Ndovu wetu aka Kinana watakapenda kuanzisha zari,badala ya kutumia muda mdogo kupiga hatua tutajikuta tunarudi hatua ishirini nyuma nyuma
 
kila mtu ni mbabe kwenye nafasi yake,lakini tutafika tu!.......

Huyo kiongozi wa CCM hatumii akili maana alitakiwa azungumze na mkuu wa wilaya kwanza hata kama alichokuwa anafanya mkuu wa wilaya si sahihi au alikuwa anataka zsifa za kijinga.
 
kwa ni ni unasema mkuu wa wilaya ni kilaza?

Swala la usafi kwenye mamlaka za miji au halmashaur zipo chin ya mamlaka husika na naamin kila halmashaur zina by law zao, so hapo dc alikuwa anatafuta tu umaarufu wa bure
 
swala la usafi kwenye mamlaka za miji au halmashaur zipo chin ya mamlaka husika na naamin kila halmashaur zina by law zao, so hapo dc alikuwa anatafuta tu umaarufu wa bure
kwa hiyo mkuu wa wilaya kwa mujibu wa sheria hawezi kusimamia na kuweka utaratibu wa kuhakikisha mazingira ni safi kwenye wilaya yake?
 
Afu mambo mengine ya kizamani kweli kweli, yani siku za alhamis maduka yafunguliwe saa nne asubuh kisa usafi? kwa hyo kuanzia j3 hadi j5 hakuna kufanya usafi? unaambiwa hayo kaamua mkuu wa wilaya mwenye akili timamu, watu wafungue maduka saa nne? duh
 
kwa hiyo mkuu wa wilaya kwa mujibu wa sheria hawezi kusimamia na kuweka utaratibu wa kuhakikisha mazingira ni safi kwenye wilaya yake?

Kwa hyo unamuunga mkono? usafi ni kila siku bana bila kujali ni alhamis au lah
 
kwa hyo unamuunga mkono? Usafi ni kila siku bana bila kujali ni alhamis au lah......

kila siku ila mimi naona ni sahihi tu kutenga siku moja masaa labda mawili kwa ajili ya usafi mkuu.kwa mfano hata mimi nyumbani nafanya usafi kila siku ila jmosi nafanya zaidi.
 
kazi ya mkuu wa wilaya ni kubuni sera na kutekeleza sera na majukumu yaliyotolea na serikari kuu, mwenyekiti wa CCM hafahamiki hata kikatiba.ukilaza wa mwenyekiti huyo wa wilaya wa CCM ndio aliouchukua mr. Nape na kuingilia vyombo vya dola kama alivyo fanya kwa kuamrisha jeshi la magereza kuondoa kizuizi kilichokuwa kimewekwa na jeshi hilo kwa sababu maalum.enyi viongozi wa chama wa CCM acheni kulewa madaraka.huu ni mfumo wa vyama vingi na wala cio mfumo wa chama kushika hatamu.

Mnafaa kushitakiwa.m uwe mnasoma mno katiba ya nchi na sio katiba ya chama chenu na matokeo yake mnagombania fito kwa kujenga nyumba moja na mwisho ni kuabishana bana.
 
kila siku ila mimi naona ni sahihi tu kutenga siku moja masaa labda mawili kwa ajili ya usafi mkuu.kwa mfano hata mimi nyumbani nafanya usafi kila siku ila jmos .

mkuu hayo masaa 4 utayafidiaje kibiashara?
 
hakuna cha kufidia.nani kakuambia muda ukishapita unaweza kuufidia? nadhani unajua wabongo tulivyo wa bishi kufanya mambo hadi tusukumwe!......

Mbona maeneo mengine usafi unafanywa bila kufungwa maduka na mambo yanaenda?
 
Back
Top Bottom