Viongozi wa CCM mbona mnahangaika kwenye chaguzi za vyuo vikuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa CCM mbona mnahangaika kwenye chaguzi za vyuo vikuu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PAMBANA, May 20, 2011.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF naomba kuchukua nafasi kuwauliza viongozi na wapenzi au washabiki wa CCM walioko humu ndani " Kwa nini viongozi wa CCM wakiongozwa na Nape wanahangaika sana kwenye chaguzi za serikali za wanafunzi vyuoni? " maana ni ukweli usiopingika kwenye vyuo ambako uchaguzi umeishafanyika tumeshuhudia wagombea ambao ilifahamika kuwa ni wanachama wa CCM walitumia gharama kubwa sana kwenye kampeini zao lakini mwisho wameambulia kushindwa. Kwa mfano tumesikia kilichotokea kule UDOM jinsi ambavyo hawa jamaa walitumia gharama kubwa sana (millions of shillings), vivyo hivyo pale RUCO-Iringa, CBE-DSM. Hata hapa TUMAINI-Iringa katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mgombea mmoja ambaye anajulikana kuwa ni mwanachama wa CCM alipewa fedha millioni kadhaa na kada wa chama hicho hapa mkoani za kutumia kwenye kampeini zake, kama kawaida ya CCM baada ya kijana huyu kutokubalika alifikia hatua ya kwenda kukodi vijana kutoka sehemu nyingine kwqa kuwanunulia pombe ili waje kumpigia kampeini lakini pamoja na hayo yote aliangukia pua vibaya sana.Hivi sasa nimesoma thread moja humu jinsi ambavyo CCM imetumbukiza sh.10,000,000/= kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi pale Chuo cha MIPANGO Dodoma.

  MY TAKE:
  Vijana wa vyuo vya elimu ya juu ni nguvu ya mabadiliko hapa nchini hivyo naomba tusirubuniwe na wahuni,sisi ndio watu wa kuwasaidia kuwatoa ndugu zetu ambao bado wapo gizani na wengi wao wapo vijijini ambako tulio wengi tunatokea huko. Fedha wanazowapa chukueni maana ni kodi za wazazi wetu.Kumbukeni vijana hasa wa vyuo vikuu ndo wamekuwa chanzo cha mabadiliko katika nchi zao kwa mfano angalia kilichotoke pale Tunisia, Misri na kinachoendelea kule Syria, hivyo naomba wenzangu tubadilike maana ukombozi wa kweli wa taifa letu upo mikononi mwetu vijana.

  " YOUTH LET US THINK CRITICALLY AND ACT GLOBALLY"
   
 2. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Ha ha ha. Kaka ina maana huyo kijana wa bacd alimwaga pesa?
   
Loading...