Viongozi wa ccm mbona mnahangaika kwenye chaguzi za vyu vikuu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa ccm mbona mnahangaika kwenye chaguzi za vyu vikuu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by PAMBANA, May 20, 2011.

 1. P

  PAMBANA Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF naomba kuchukua nafasi kuwauliza viongozi na wapenzi au washabiki wa CCM walioko humu ndani " Kwa nini viongozi wa CCM wakiongozwa na Nape wanahangaika sana kwenye chaguzi za serikali za wanafunzi vyuoni? " maana ni ukweli usiopingika kwenye vyuo ambako uchaguzi umeishafanyika tumeshuhudia wagombea ambao ilifahamika kuwa ni wanachama wa CCM walitumia gharama kubwa sana kwenye kampeini zao lakini mwisho wameambulia kushindwa. Kwa mfano tumesikia kilichotokea kule UDOM jinsi ambavyo hawa jamaa walitumia gharama kubwa sana (millions of shillings), vivyo hivyo pale RUCO-Iringa, CBE-DSM. Hata hapa TUMAINI-Iringa katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi iliyopita mgombea mmoja ambaye anajulikana kuwa ni mwanachama wa CCM alipewa fedha millioni kadhaa na kada wa chama hicho hapa mkoani za kutumia kwenye kampeini zake, kama kawaida ya CCM baada ya kijana huyu kutokubalika alifikia hatua ya kwenda kukodi vijana kutoka sehemu nyingine kwqa kuwanunulia pombe ili waje kumpigia kampeini lakini pamoja na hayo yote aliangukia pua vibaya sana.Hivi sasa nimesoma thread moja humu jinsi ambavyo CCM imetumbukiza sh.10,000,000/= kwenye uchaguzi wa serikali ya wanafunzi pale Chuo cha MIPANGO Dodoma.

  MY TAKE:
  Vijana wa vyuo vya elimu ya juu ni nguvu ya mabadiliko hapa nchini hivyo naomba tusirubuniwe na wahuni,sisi ndio watu wa kuwasaidia kuwatoa ndugu zetu ambao bado wapo gizani na wengi wao wapo vijijini ambako tulio wengi tunatokea huko. Fedha wanazowapa chukueni maana ni kodi za wazazi wetu.Kumbukeni vijana hasa wa vyuo vikuu ndo wamekuwa chanzo cha mabadiliko katika nchi zao kwa mfano angalia kilichotoke pale Tunisia, Misri na kinachoendelea kule Syria, hivyo naomba wenzangu tubadilike maana ukombozi wa kweli wa taifa letu upo mikononi mwetu vijana.

  " YOUTH LET US THINK CRITICALLY AND ACT GLOBALLY"
   
 2. H

  Honey K JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rafiki angu Pambana,
  Kuzusha mambo hakufai hasa unaposema wanaongozwa na Nape hao unaowaita viongozi wa CCM, nakushauri sema ukweli badala ya kuzusha kwa lengo la kufurahisha na kuchafua watu hapa... Sijawahi kujihusisha na uchaguzi WOWOTE wa vyuo wala shule, haya ni majungu ya aibu kwa aliyeyazusha....achani...
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  nice to see you nape coming up openly respond to those accusations this is how politicians are supposed to be
   
 4. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nape
  Nimeipenda style hii nape ya kujitokeza na kujibu hadharani haraka kiasi hiki, safi sana. Lakini nijuacho mie kuhusu uchaguzi wa vyuo vya elimu ya juu ni kwamba pale UDOM kampeni zilitawaliwa sana na UDINI, ukristu na uislamu na hatimaye upande mmoja ukashinda. Hata hivyo udini huo ulikuwa na msukumo wa vyama vya siasa tena vyama vikuu hapa Tanzania. Fanyeni uchunguzi mtagundua hili.

  Juzijuzi ukafuata uchaguzi katika chuo kikuu cha Ardhi hapa Dar es salaam. Kama ilivyokuwa UDOM, ARDHI napo kukatawaliwa na udini, lakini wale walioshinda dodoma hapa ARDHI wakajikuta wakidondoka na hivyo upande wa pili kushinda kuanzia nafasi ya uraia na makamu wake. Mbaya zaidi hapa Ardhi Rais akafanya uteuzi wa WAZIRI MKUU na bahati mbaya akamteua mfuasi wa dini yake pia. kuona hivyo bunge la ARDHI likakataa kumuidhinisha waziri mkuu huyo na hadi ninapoandika post hii waziri mkuu huyo alikuwa hajaidhinishwa na bunge limeweka ngumu kwa kisa cha UDINI.

  ONYO: Uchaguzi wa DARUSO uko kwenye maandalizi makali sana kwa sasa na wanasiasa wameshavamia kambi huko tayari. Pia UDINI umeingia huko. Sie wenye mapenzi mema na nchi yetu ambao hatuna mrengo wa chama chochote na TUCHUKUE HATUA!
   
 5. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Vipi ile kauli kuhusu CHADEMA ni chama cha wachaga unayodaiwa kuitoa hivi karibuni unaweza kuitolea ufafanuzi maana imechafua hali ya hewa ya kisiasa hapa nchini!!
   
 6. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  wachaga wanakusubiri ili wakukabidhi kadi za chama chako na waende katika kile chama ulichosema ndio cha kwao.
   
 7. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  thx my doctor kuchokonoa, i would love to hear his comment on ths..if he regretts or if it is jst okay with hm
   
 8. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Lakini hata tuki-assume kwamba ni kweli ulifanya hivyo kwani ni dhambi? Mbona akina Lema wanahangaika huko UDOM na vyuo vingine. Anatafuta nini. Hii mijitu ni kulia lia na kulalamika kila wakati! We are sick and tired of this hopelessness!
   
 9. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mbona hilo limejadiliwa sana. Hivi Dr. hilo ukiluliza humu utapata jibu tofauti na lile lililoko kwenye zile thread?
   
 10. Fungo N.

  Fungo N. JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  to be what?ask the UDOMU'S what was going on here during the udoso election and hw the students responded.
   
Loading...