Viongozi wa CCM hiki mnachofanya sio sawa

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Bado najiuliza hofu ni ya nini? 2025 itafika mtampitisha mnayemtaka na mtampigia kampeni kwa kadri mtavyotaka.
Hata mkiamua kumpitisha kibajaji ni sawa tu, maana yatakua maamuzi ya chama chenu.
Nimesoma maoni(comments) kwenye media zote na viongozi waliopost Hilo suala, nimeona asilimia kubwa bado hawamkubali kabisa mama. Na hata mtaani hali ipo hivyo.
Lakini hii sio issue sana kwa kuwa mama ana muda wa kurekebisha na kuweka mambo sawa na watu wengi wakamkubali kuliko kuanza kuja na hizi kampeni.
Wenyewe mmekiri kuwa uchumi umeshuka sana, kwa nini msitumia nguvu kubwa kupambana ili uchumi uinuke?
Mnapaswa kujikita kuinua uchumi, uchumi ukishainuka na watanzania kunufaika Wala hakutakua na sababu ya kutumia nguvu kunadi mgombea wenu kwa kuwa kila mmoja ataona mambo yaliyofanyika
Mfano; msimu huu mbolea imeongezeka Bei Mara mbili, mkapiga blahblah lakini hadi sasa bei bado haijashuka. Watanzania walio wengi (zaidi ya mil 40) wanategemea kilimo. Kwa nini msije na mbinu kuwasaidia sasa hivi waweze kumudu hizi gharama kubwa za mbolea?
Au mngeweza kuweka ruzuku kwenye mbolea ili hawa mamilioni ya watanzania waweze kumudu bei.
Hiki mnachofanya sio sawa kabisa.

Screenshot_20210919-103036_1.jpg
20210918_150949.jpg
 
Athari za kutangaza kugombea mapema ni kubwa kuliko asingetangaza, kwa sasa itabidi aishi kwa makini sana maana mistake yoyote hata iwe ndogo itazidi kumshushia ukubalikaje wake.
 
Back
Top Bottom