Viongozi wa Bunge wanaweza kuwa tatizo lakini KUB ni tatizo Kubwa

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
Juzi Wanafunzi Takribani 7000 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) waliamriwa na uongozi wa Chuo kurejea Majumbani mwao wakati tatizo la mgomo wa Wakufunzi wao likitafutiwa ufumbuzi.

Baada ya tukio hilo, bunge liliingia kati kutaka kujua hatma ya Wanafunzi hao. Alikuwa ni Mbunge wa Chemba(CCM) , JUMA NKAMIA aliyeomba muongozo kutaka shughuli za Bunge zisitishwe ili waheshimiwa Wabunge waweze kujadili suala hilo la UDOM. Hata hivyo hoja ya NKAMIA ilikataliwa baada ya kukosea kanuni. Ndipo Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipofuata vizuri kanuni za Bunge na Muongozo wake kusikilizwa.

Naibu Spika wa Bunge, Tulia Akson kwa kutumia kanuni hizohizo za Bunge alisema Bunge litaendelea kama kawaida na hazitasitishwa ili kujadili tukio la UDOM kama suala la dharura.

Uamuzi huo wa Naibu Spika haukuwafurahisha Wabunge bila kujali itikadi zao waliamua kutoka nje Ukumbi wa Bunge kama ishara ya kupingana na maamuzi ya Naibu Spika.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani, Freeman Aikaeli Mbowe wakati akitolea maamuzi yake alisema ANAWAOMBA WABUNGE WOTE KUSUSIA VIKAO VYOTE vitakavyoongozwa na Mh. Tulia Akson akiwa kama Naibu Spika au Mwenyekiti.

Kauli hii ya MBOWE imekuja baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kupendekeza baadhi ya Wabunge kuadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni za Bunge kutokana na kwenda kwao kinyume na kanuni za Bunge wakati wakijadili suala Televisheni ya Taifa TBC1 kutoonesha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge.

Kauli ya Mbowe ya kutaka Wabunge kususia vikao vyote vitakavyoendeshwa na Mh. Tulia Akson nayo imezua mjadala huku mitaani huku wengine wakisema Mbowe amehofu kama Bunge linaweza kuwa na nguvu tena baada ya Wabunge ambao wanaonekana kuwa ndiyo wasemaji wazuri kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge, adhabu ya kuanzia kutohudhuria vikao 10 hadi mikutano 2.

TAFAKURI YANGU: Vyovyote vile kwa sababu gani Mbowe ametoa kauli ya kuwataka Wabunge wasusie vikao vitakavyoendeshwa na Naibu Spika, Dr. Tulia Akson, iwe ni kwa sababu hatendi haki au kwa sababu tu ya kuogopa akina nani wataweza kukabiliana na kanuni za Bunge baada ya Wabunge Machachari kuadhibiwa, binasi naona MBOWE ni TATIZO kubwa sana. MBOWE ameshindwa kabisa kuwa KIONGOZI WA UPINZANI na badala yake amekuwa ni KIONGOZI wa MIGOMO BUNGENI. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani anatakiwa awe kiungo kati ya Wabunge wa chama tawala na wale wa Upinzani katika kuisimamia Serikali.

Kauli za MBOWE zimekuwa ni kauli za Mwisho kwa Wabunge wa Upinzani wachukue hatua gani. Kuanzia Bunge la Katiba, sakata la TBC1 kuonesha vikao vya Bunge na hata hili la UDOM , wabunge wamefuata kauli za Mbowe, hii ni hatari sana. Siku Mbowe akisema Wabunge wote wampige kiongozi wa Bunge aliyeko meza ya Spika watafanya hivyo.

Siamini kama kuongoza Wabunge kutoka nje au kugomea vikao vya Bunge ni suluhisho la tofauti zinazojitokeza kati ya kiti cha Spika na Wabunge.

Misimamo isiyo na tija ya KUB ndiyo inayopelekea Serikali isisimamiwe vyema. Leo Wabunge wamesimamishwa kuhudhuria vikao wakati wa kipindi ambacho wanahitajika sana, kipindi cha kujadili bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Katika sakata la UDOM wabunge wametoka nje, je hilo limekuwa suluhisho la tatizo hilo? Waligomea kujadili hotuba ya rais kwa sababu tu Bunge halikuoneshwa live, hilo lilikuwa ni suluhisho? Leo Bunge linaoneshwa live?

Ni lazima MBOWE ajitathmini kama anafaa kuendelea kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni(KUB), la sivyo Bunge litaendelea kuwa Bunge la vurugu na siyo la kutetea Wananchi. Binafsi nilitegemea Wabunge wang'ang'anie kuomba suala la Wanafunzi wa UDOM lijadiliwe kama suala la dharura kuliko kukimbia na kutangaza kususia vikao, haya wamekimbia na watasusia vikao, nini mchango wao katika hatima ya wanafunzo hao?
 
Eti "Bunge linaweza kuwa na nguvu tena". Kwa hiyo unaamini kwamba kuna kipindi lilikosa nguvu? Yaani vikaragosi vya umagambani vinakera kweli kweli.
 
Huwezi kumchagua mtu ambaye ni failure wa form six awe mwenyekiti wako dheni ukategemea matokeo mazuri. Wana CHADEMA wamevuna walichopanda
Mwenyekiti wako nae ali disco chuo ila sbb vice wa wakati huo ndo alikuwa katibu mkuu wa chama wakambeba.
 
Mwenyekiti wako nae ali disco chuo ila sbb vice wa wakati huo ndo alikuwa katibu mkuu wa chama wakambeba.
Huna ushahidi wa hilo. Hili la Mbowe linafahamika hata kwa watoto walio tumboni
 
Nilisoma mahali huko Dodoma wanahoji itakuwaje ikiwa Naibu Spika akiongoza vikao vyote vilivyobaki?Upuuzi kabisa.
 
Eti "Bunge linaweza kuwa na nguvu tena". Kwa hiyo unaamini kwamba kuna kipindi lilikosa nguvu? Yaani vikaragosi vya umagambani vinakera kweli kweli.
downloadfile-23.jpeg


swissme
 
Mbowe anawaharibia wabunge wake. Wabunge wanaweza kuwa na hoja za msingi za kuwasaidia wanancbi lakini zikapotea kwa sababu ya Kauli za mihemuko za KUB kwa sababu tu ya kutafuta appreciation ya Wananchi. 2020 bado mbali nani atakuja kukumbuka kuwa Mbowe aliongoza migomo ya Udom na Bunge live? Sasa Wanafunzi wa UDOM wako wapi?
 
Huwezi kumchagua mtu ambaye ni failure wa form six awe mwenyekiti wako dheni ukategemea matokeo mazuri. Wana CHADEMA wamevuna walichopanda
KILAZA KTK UBORA WAKO,UNAONA WANAFUNZI 7000 KUKATISHWA MASOMO NI SAWA?KUMBUKA HAWA WALIDAHILIWA NA SERIKALI YA CCM.UJINGA NI MZIGO.UPUMBAVU HAUTAKUSAIDIA KIJANA,UTAJITAMBUA LINI?SHAME OF U.
 
Huwezi kumchagua mtu ambaye ni failure wa form six awe mwenyekiti wako dheni ukategemea matokeo mazuri. Wana CHADEMA wamevuna walichopanda
Wewe Lizabon acha bwana!! Utaka kutuaminisha pamoja na kujiamini kwake kote huko hakuweza kupata hata Div.4? Siamini, hahahahahah
 
Wewe Lizabon acha bwana!! Utaka kutuaminisha pamoja na kujiamini kwake kote huko hakuweza kupata hata Div.4? Siamini, hahahahahah
Watuwekee hata matokeo yake bwana, this is too much. Anakurupuka sana. Hivi leo Magufuli akaamka akasema maeneo yetu tususiane pale tunapotofautina nchi itakalika kweli? Kiongozi lazima awe na busara na staha.
 
Mbowe ndio amewaambia wale Waadhiri wa UDOM wagome?
hajawaambia lakini kama kiongozi wa Mbunge aliyetoa hoja alitakiwa ahakikishe hoja inajadiliwa ili kuwasaidia wale vijana , sasa amekimbilia kusema wanagomea vikao, so what next?

Hivi Wabunge wakikomaa Bungeni wanataka hoja ijadiliwe Spika atafanya nini zaidi ya kukubaliana na hali halisi? Tatizo la Mbowe anataka sifa kwa watu kama wewe. Ni hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom