Viongozi wa Bunge na wabunge someni hii kisha mtafakari "Bunge la Hoja Vs Bunge la Kanuni" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Viongozi wa Bunge na wabunge someni hii kisha mtafakari "Bunge la Hoja Vs Bunge la Kanuni"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chaimaharage, Jul 29, 2012.

 1. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni makala iliyo andaliwa na Dr.Kitila Mkumbo(Jembe) kwenye gazeti la Raia Mwema, Toleo la 251, 25 July 2012.


  KATIKA siku za hivi karibuni majadiliano katika Bunge letu yamepata ufuasi mkubwa kutoka kwa wananchi wanaofuatilia kupitia luninga na redio. Kuna Mwalimu mwenzetu mmoja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa muda sasa amekuwa akirudi nyumbani kila ifikapo saa nne asubuhi na saa kumi na moja, jioni kwenda kutazama kipindi cha Bunge. Imefika mahala anamshindwa kuacha kwenda kutazama majadiliano bungeni na anaporudi hutusimulia yaliyojiri kwa furaha na hamasa kubwa.

  Hata hivyo, katika siku za karibuni ameacha kwenda kutazama Bunge kama ilivyo kawaida yake, kwa sababu anazodai kuwa Bunge letu limegeuka kuwa Bunge la Kanuni badala ya Bunge la Hoja ! Kwamba Bunge letu limekuwa likitumia muda mwingi kulumbana juu ya matumizi ya kanuni za Bunge, badala ya kujadiliana hoja zinazohusu maisha ya wananchi na taifa kwa ujumla. Na kuna wabunge ambao wameamua kubobea katika kutoa miongozo kiasi cha kupachikwa jina la ‘Mbunge wa Mwongozo' mitaani.

  Kwa mujibu wa maoni ya wananchi yaliyochapishwa katika magazeti ya Jumapili iliyopita, ni wazi kwamba wananchi wengi wameanza kukosa hamasa na hamu ya kutazama majadiliano bungeni kama ilivyo kwa mwalimu mwenzangu niliyemtaja. Maoni ninayoyatoa katika makala haya yana lengo la kujaribu kuwakumbusha wabunge, na hasa viongozi wa Bunge, juu ya wajibu wao ili warudi katika mstari na kuwapa wananchi kile wanachokitarajia kutoka kwao.
  Katika Jumuiya ya Madola, Bunge lina kazi kubwa nne za msingi. Kazi ya kwanza ni kujadili, kutathmini na kusimamia utendaji wa serikali. Kazi ya pili ni kujadili na kupitisha sheria mbalimbali. Kazi ya tatu ni kuiwezesha serikali kupandisha kodi kupitia bajeti za kila mwaka. Kazi ya nne ni kujadili na kutoa mwelekeo juu ya jambo lolote zito lililotokea katika nchi ambalo linaweza kuchukuliwa kama dharura.

  Ukiwa mfuatiliaji wa Bunge letu utakubaliana nami kwamba Bunge letu limefanya kazi nzuri sana katika maeneo mawili, ambayo ni kupitisha sheria na kuiwezesha serikali kupandisha kodi mbalimbali kupitia bajeti za kila mwaka. Kwa maoni yangu, Bunge letu halijafanya kazi yake sawa sawa katika kujadili, kutathmini na kusimamia utendaji wa serikali. Hata lugha ambazo wabunge wetu wanazitumia bungeni ni kielelezo cha kutosha juu ya wao kupwaya katika kuelewa au kuzingatia uzito wa mamlaka yao dhidi ya serikali ambayo yapo wazi kikatiba. Kwa mfano, wabunge wengi wanapowasilisha maoni au mahitaji yao kuhusu jambo fulani wana tabia ya kusema kwamba ‘ninaiomba au ‘ninaishauri' serikali. Sasa hata kama mimi nilikuwa ndiye serikali ukishaniambia ‘unaomba' au ‘unanishauri' ni wazi kwamba nina hiari ya kukubali au kukataa ombi au ushauri wako. Serikali ina washauri chungu nzima ambao wameajiriwa kwa ajili hiyo wakifanya utafiti na uchambuzi kwa ajili ya kuishauri serikali kitaalamu, ambao ni muhimu zaidi kuliko ushauri wa mbunge unaotolewa katika dakika 10 anaposimama bungeni.

  Kwa sababu wabunge wetu wamekaa kiushauri zaidi kuliko kiuwajibikaji, wamefika mahala hawawezi kujadili jambo lolote zito hadi serikali ikubali kushauriwa. Na ni bahati mbaya kwamba viongozi wa Bunge wanaisikiliza serikali zaidi kuliko wanavyowasikiliza wabunge. Na serikali nao wamebuni mtindo unaowasaidia kukwepesha mijadala mizito kwa kutumia kanuni. Kwa hivyo serikali, badala ya kujiandaa kujibu hoja, inajiandaa kwa kutafuta kanuni ya kukwamisha mjadala ! Matokeo yake ni kwamba Bunge letu lipo ‘busy' kulumbana juu ya kanuni badala ya kulumbana juu ya hoja, na hatimaye upande wa serikali hushinda-kwa kukwamisha mjadala. Ndivyo ambavyo mijadala mizito kama ya utekwaji wa Dk. Steven Ulimboka na kuzama kwa meli ya MV Skagit ilivyozimwa. Kwa kutumia kanuni za Bunge, viongozi wa Bunge wametukosesha fursa muhimu na adimu ya kujua kilichomkumba Dk. Ulimboka na sababu hasa za matukio yanayofuatana ya kuzama kwa meli huko Zanzibar. Bunge letu limeingia katika historia isiyotukuka kwa kukubali kukatazwa kutekeleza kujadili mambo mazito katika jamii.

  Ni muhimu viongozi wa Bunge wakazingatia kwamba watazamaji na wasikilizaji wa vipindi vya Bunge hawapo kwa ajili ya kushuhudia umahiri wa kuzijua kanuni za Bunge. Wana hamu na hamasa ya kutazama na kusikiliza jinsi ambavyo wabunge wao wanaibua hoja zinazohusu maisha yao na nchi yao. Na hili ndilo lililoleta hamasa kubwa kwa wananchi kupenda mijadala ya Bunge. Kama viongozi wa Bunge wataendelea kuikumbatia serikali kwa kuiruhusu itumie kanuni kuzima mijadala yenye maslahi mapana kijamii, Bunge litapoteza mvuto na maana katika jamii. Na ikifika hapo Bunge letu litasuswa sio tu na watazamaji/wasikilizaji ,lakini pia hata na wabunge wenyewe kama tulivyoshuhudia hivi karibuni. Tunamshauri Spika wa Bunge atumie kanuni za Bunge katika kufanikisha badala ya kukwamisha mijadala ya wabunge. Tunataka Bunge la Hoja na sio Bunge la Kanuni!

   
 2. T

  Technology JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  hivi huwezi kuandika kwa kifupi na ueleweke mpaka ujaze pumba nyingi? hao wanafunzi mnawaeleweshaje sasa?
   
 3. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi unajua kipi ni pumba na kipi siyo? jipi jema, kuandika kwa kirefu watu wakapata ujumbe husika au kuandika kwa kifupi bila kutoa majibu na ufafanuzi wa kile ulicho dhamiria kuwafikishia ujumbe?
  Acha uvivu wa kusoma na kufikiri, nyie ndio watanzania tulionao siku hizi na matokeo yake bado tumezidi kukwama kwenye lindi la umaskini na fikra mbovu kama zako. Ili tuendelee inabidi kizazi kama chako kitoweke. Dr kaongea mambo ya msingi lakini mbumbumbu kama wewe bado umeshindwa kuchambua hizo pumba na kuziainisha hapa kwamba hiki na niki ni pumba.

  Uvivu huleta umaskini na mwisho wa yote ni wivu kwa kuona wenye fikra za kimaendeleo wakitoa mchango wao kwenye jamii. Jana umelala na hangover nini? make walevi kama wewe ni wengei sana..kodi kwenye kinywaji ndio kiboko yenu.
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Kama mwalimu uchambuzi wake ni dhaifu, umejaa hisia za kishabiki na propaganda za kuomba huruma.
  Kama mwanasiasa amefanikiwa kuonesha picha halisi ya kinachoendelea bungeni, kukigeuza kwa manufaa yake kisiasa na kushambulia mpinzani wake. Inategemea unaitazama kwa jicho lipi.
   
 5. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni makala iliyoandikwa gazetini na Dr.Kitila Mkumbo na mleta thread ni Kimbweta ambaye siyo mwalimu sasa kwanini unasema hao wanafunzi mnawaeleweshaje. Uwe makini unapochangia hoja ndugu yangu Technology.
   
 6. T

  Technology JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  kuandika saaana haimaanishi mantiki, wako wabunge wanaongea saana hata zaidi yako lakini mwenyewe unashuhudia kinachotokea leo bungeni. kama wewe ni mwalimu
   
 7. T

  Technology JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 733
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Kwani Dr.Mkumbo sio Mwalimu? hawezi kaundika kwa kifupi??? umakini upi zaidi ya huo. au umakini kwako ni NSSF kutulipa jasho letu baada ya miaka 55?
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  wewe una technology ya mafunzo ya mbwa, kwani mbwa haambiwi sentesi ndefu, (kama, kula, acha, lala n.k) na kwa mtazamo huo upo kitengo kimoja na "rama" kwenye kile kitengo wahusika hurandaranda magogoni kusubiri maelekezo ya jack zoka.
   
 9. m

  muafaka Senior Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dr. kitila nadhani kubeza kanuni si sahihi, masuala mengine umezungumza yana mashiko kiasi. Nadhani ngezungumzia Bunge kuwa la HOJA NA LENYE KUFUATA KANUNI, kama mtaaluma ningekupa Bigup.

  Unaniacha hoi pale unapo refer kwenye magazeti, nilitegemea uzungumzie matokeo ya utafiti nadhani ingesaidia zaidi kuongeza makali ya hoja.
   
 10. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Niliwahi kutoa tahadhari juu ya mwenendo wa bunge letu na haliya kukosa meno kiasi cha kushindwa kufanya kazi yake barabara katika kuisimamia serikali,nilifika mbali zaidei kwa kutaka kama inawezekana tulivunje bunge na kufanya uchaguzi ambao utawapeleka wabunge makini wenye kuweza kujua majukumu yao ya kibunge.

  Naweza kusema bunge limehongwa na serikali ndiyo maana serikali imekuwa juu ya bunge na wabunge wameamua kuisadia serikali kujibu hoja kali za baadhi ya wabunge ambao wamekosa mshikamano toka kwa wabunge wenzao.Ndo maana nimeiunga hoja yako mkono tena umeileta wakati muafaka.

  Nasisitiza kuna rushwa ya mazingira kati ya bunge na serikali ndo maana hata wabunge wetu wameona upuuzi wameaamua kula mlungula na kuingiza nchi kwenye giza pasi na sababu za msingi
   
 11. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Acha Uvivu.
   
 12. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #12
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama haya unayaona ni pumba basi wewe ufahamu wako una mushikeli au magamba wamekuharibu uwezo wako wa kufikiri.
   
 13. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #13
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na mtoa hoja 100%. kwangu mimi wanaoliharibu bunge ni spika na wenyeviti wake kwa kuendesha bunge kwa matakwa ya serikali.Ndio maana hoja yoyote ambayo serikali haitaki ihojiwe bungeni spika et al hawawezi kuruhusu ihojiwe hata kama mbunge atatumia kanuni kwa usahihi wote. mfano, kanuni alivyoitumia Tundu Lisu kutaka uwepo mjadala kwa tukio la kuzama mv skagit na namna jobu ndugai alivyozuia, mpaka unaona aibu jinsi wanavyotumiwa vibaya na serikali.
  Kwa suala la DR Ulimboka, serikali ikamtafuta mkenya feki haraka-haraka ikampeleka mahakani ili bunge lifyate mkia, na kweli ikawa hivyo, basi serikali inaendelea na uovu wake bila wasiwasi, huku ikiwa na uhakika wa utetezi wa spika na wenyeviti wake. Kwangu mimi spika et al ni janga la taifa
   
 14. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenena. Kizazi hiki ni cha "Multiple choice" kwenye mitihani yao. Mambo ya "discuss", "compare", "define" hayapo tena kwenye syllabus zao!
   
Loading...