Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,601
- 217,992
Hii ndio taarifa iliyotufikia usiku huu, kwamba Mhamasishaji wa BAVICHA Twaha Mwaipaya na Katibu Mkuu wa Bavicha Mh Nusrat Hanje , leo wameachiwa huru na Serikali ya Tanzania , huku ikidai haina haja ya kuendelea na kesi hiyo, hii ni masaa machache kabla ya kusomwa hukumu ya maombi yao ya haki ya dhamana .
Vijana hawa wadogo walishtakiwa kwa kosa la kuimba wimbo wa Taifa lao huku wakipandisha bendera ya chama chao cha siasa ambacho kimesajiliwa kufanya siasa nchini Tanzania , wamekomolewa kinyama kwa kunyima dhamana kwa zaidi ya miezi minne kutokana na roho mbaya za viongozi washamba waliopata madaraka ya nchi na kuyatumia kama silaha ya kuumiza wengine .
Bali kama tulivyosema mara zote ni kwamba HAKUNA MAHALI POPOTE KATIKA DUNIA HII AMBAPO SHETANI ALIWAHI KUMSHINDA MUNGU KWENYE LOLOTE .
Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri .