viongozi wa aina hii ya Sumaye ni hatari sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

viongozi wa aina hii ya Sumaye ni hatari sana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Danniair, May 29, 2012.

 1. D

  Danniair JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 361
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [h=2]Mtanzania
  ''Sumaye aibomoa Takukuru [/h]Jumatatu, Mei 28, 2012 08:39 Na Arodia Peter


  *Adai wakiitegemea mapambano ya rushwa yatakuwa magumu
  *Awataka Watanzania wawe na usajiri wa kukataa ufisadi
  *Asema viongozi wanaoingia madarakani kwa rushwa hawafai
  WAZIRI Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, amesema Watanzania wasitarajie
  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ndiyo iwasaidie
  kupambana na vitendo vya rushwa, kwani watakuwa wanapoteza muda.

  Akizungumza katika ibada ya kuombea taifa, iliyoandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima, Kawe mjini
  Dar es Salaam jana, Sumaye alisema kama Watanzania wasipokuwa na ujasiri wa kupambana na vitendo
  vya rushwa na ufisadi, nchi itaangamia. ''

  Sikutetemea mwanzilishi wa chombo hiki leo akipige mateke, chombo ambacho akiwa waziri mkuu
  alikitetea kwa nguvu zake zote. Nadhani Hosea wakati umefika uibue yale madudu yao hata watakapoona
  kuwa chombo kinafaa. Kwani walikunyima meno ili usiwakamate. Sasa Hosea lilia meno ili wakuheshimu.
   
 2. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sumaye amesema ukweli mtupu, kuna watu waliingia madarakani kwa rushwa sasa tunaona serikali inawashinda kuiendesha maana hela za watu zilitumika, hujui hilo??? Pili unataka Sumaye awambie watz kuwa woga mbele ya mafisadi???

  Tatu hadi sasa mapambano ya rushwa ni magumu, ulitaka aseme ni mepesi wakati hata presida kanywea, hudhani ni magumu???

  Maige anaposema majangiri wananguvu hata ya kumng'oa mtu uwaziri, huelewi maana yake??? waziri anateuliwa na rais, leo jangiri ananguvu ya kumtoa waziri, huelewi Maige anasema nini??? rais anaushirika wa karibu na jangiri kuliko waziri wake, funguka kichwani sio mdomoni.:israel:
   
 3. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Serikali ya mazimwi, yameanza kulana yenyewe.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu Danniair sasa hapo Sumaye kakosea wapi? Ukweli wote kuhusu utendaji wa takukuru wote tunaujua sasa kuwataka takukuru kuibua madudu ya Sumaye na wenzake leo ni uzandiki ambao hauwezi kuisaidia takukuru wala yeyote. Kama akina Sumaye waliinyima meno takukuru hao waliofuata wameipa meno kiasi gani? Acheni ukweli usemwe.
   
 5. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Hivi unafikiri wao hawayajui madudu ya Hosea?
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,137
  Trophy Points: 280
  ukweli unauma wewe
   
 7. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  ngoja wamalizane, sisi ni M4C tuu
   
 8. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni lini anasema chochote kuhusu hili(soma attachment) lilioweka mizizi ndani ya eneo ambalo yeye alikuwa mbunge kwa muda mrefu? Mungu hakejeliwi siku moja Mwenyezi Mungu atasikia sala na maombi ya watu walioshikiwa chini under his watch! Aache kujifanya mzalendo kanisani wakati nje ya kanisa dunia inamjua vizuri.

  :evil:


   

  Attached Files:

 9. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,394
  Likes Received: 6,578
  Trophy Points: 280
  Out of topic kidogo..this guy like a month ago alikuja kanisani kwetu kaita ufunguzi wa jengo kama mmoja wa wageni rasmi...by that time jumapili hiyo nadhani mchana kulikuwa namechi ya simba na alikuwa mgeni rasmi pia katika mechi hiyo..sasa ili kupata mwanya wa kwenda kwenye mechi akadangaya umma wote bila kujua pia kuna waumini wengine wenye ufahamu wa hayo mambo eti ana ratiba nyingine katika kanisa jingine , kwahiyo hataweza kukaa sana hapo church..akaaga..mdau na mimi nikajitosa uwanjani..namkuta kama mgeni rasmi..nikasema kulikuwa na haja gani kwa kiongozi mkubwa kama yeye kuwadangaya waumini kuwa anakwenda kanisa jingine kumbe anakwenda uwanjani??
   
 10. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  unajuaje mechi ya Simba ilikuwa ni part ya ibada zake?
   
 11. franktemu123

  franktemu123 JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 775
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 80
  Kiukweli pale kwa Hosea inabidi kufumuliwe upya kuanzia juu mpaka chini lakini najua Ba Riz hawez maana Hosea ni Mshkaji wake. Labda tusubiri Rais ajaye kama akitokea chama kingine. Jiulize Kesi ya Mengi vs Mafisadi Papa amabyo jamaa walisema wanaishughulikia imeishia wapi?lo wasa na richmond? bongo kwa awamu hii ya uongozi ni tambarare. vyeo vinapewa kishkaji so mtu akiingia hana wasi wasi anakulaaaaa ila akizidisha sana anatolewa kafara ili kutuliza umma (CHADEMA) halafu wanaendelea kula kama kawa.
   
 12. wagaba

  wagaba JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 829
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  na angesema ukweli wake hapo kanisani, mgesema huyo ni freemason
   
 13. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Inaelekea Dannair ndio Hosea mwenyewe!
   
 14. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hamieni Airtel tumalize kazi. Wa zee wa anga M4C. Tuko Mtwara saizi. Msipoteze muda kusikiliza uozo wa CCM na makada wake.
   
 15. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kanyaga twende.
   
 16. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Yeye alikopa mamilioni NSSF wakati sio mwanachama na alinunulia mashamba Kibaigwa,Je nani alimuruhusu kukopa fedha za wanachama,je NSSF inatoa huduma za mikopo,kama hapana kwanini yeye alipewa?Je alilipa na riba?ameisha rudisha hizo fedha.PLEASE IF YOU LIVE IN A GLASS HOUSE NEVER THROW A STONE TO YOUR NEIGHBOUR
   
Loading...