Viongozi wa Afrika kwenye hotuba zao huchomekea mambo yanayohusu ngono sijui wanadhani ni sifa?

Arovera

JF-Expert Member
Nov 19, 2013
10,953
28,422
Wakuu
Hivi hua ni sifa kwa kiongozi mkubwa akiwa anahutubia wananchi mifano yake baadhi anaitoa ikihusianisha na masuala ya ngono hua najiuliza ni kukosa jambo la kuongea au akili zao zinawaza ngono tu?
Sasa kwa mfano nisafiri kutoka mpitimbi kuja songea kumsikiliza kiongozi halafu anachohutubia hata hakieleweki zaidi anachomekea maneno ya ngono utadhani ndio ujumbe mahsusi ambao wananchi wanautaka.
Nadhani viongozi wetu wabadilike maana sio kila mwananchi hupenda kusikia maneno ya ngono isipokua anapokua kwenye eneo husika.
Unapohutubia watu jipange na uongee mambo ya maana ili wakuelewe sasa hapo hua mtu unaangalia kisaikolojia unabaki unaumia unasema bado tunasafari ndefu sana.
 
Ni namna tu ya kunogesha hotuba kwa sababu ni jambo ambalo linamhusu kila mmoja wetu kwa muda na wakati wake.
 
Ukiona anachomekea ujue na wananchi wake muda mwingi wanapiga story za dizaini hizo hizo.
 
Wanachomekea vimaneno vya hapa na pale ku stimulate attention ya wasikilizaji, unajua kwa sisi waafrika ukiongea bila kuchomekea vimaneno vya kimzaha mzaha unaweza kukuta watu wote wameshasinzia
 
Wanachomekea vimaneno vya hapa na pale ku stimulate attention ya wasikilizaji, unajua kwa sisi waafrika ukiongea bila kuchomekea vimaneno vya kimzaha mzaha unaweza kukuta watu wote wameshasinzia

Mbona Ulaya hawachomekei issue za ngono?
 
Back
Top Bottom