Viongozi wa ACT-Wazalendo Tunduru Washinda Kesi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
605
1,536
VIONGOZI ACT WAZALENDO TUNDURU WASHINDA KESI:

Viongozi wa ACT Wazalendo kutoka Mkoa wa Kichama wa Selous (Wenye Majimbo ya Tunduru Kusini, Tunduru Kaskazini na Namtumbo) waliokuwa na kesi ya kushambulia na kujeruhi katika Mahakama ya Wilaya Tunduru wameachiwa huru baada ya kukutwa hawana kesi ya kujibu katika kesi namba 70 ya mwaka 2021 ilivyokuwa ikiwakabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tunduru.

Viongozi hao ni Ndugu Mtutura Abdallah (Katibu wa Mkoa), Said Njinga (Kiongozi wa ACT Amani Mkoa), Yasin Mawila (Mwenyekiti Jimbo la Tunduru Kaskazini) na Issa Thabit (Mwanachama).

Viongozi hao walikamatwa na kufunguliwa mashtaka mwezi Mei kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwajeruhi wana-CCM waliovamia eneo lililopaswa kufanya Mkutano wa ACT Wazalendo na kutaka kufanya mkutano wa CCM wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Ligoma Jimbo la Tunduru Kusini Mwezi Mei 2021.

Chama cha ACT Wazalendo kinawapongeza Mawakili walioisimamia Kesi hiyo na kuhakikisha kuwa haki inapatikana. Tunamshukuru Wakili wa Kujitegemea Prosper Kaizelege na Wakili wa Chama Victor Kweka aliyeisimamia kesi hiyo mwanzoni.

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kuacha kutumika kisiasa wakati wa Uchaguzi kwa kuwakandamiza wapinzani na kukibeba Chama cha Mapinduzi (CCM). Jeshi la Polisi litekeleze majukumu yake kwa weledi na kuzingatia Sheria.

Imetolewa na:
Mbarala Maharagande
Katibu wa Haki za Binadamu na Makundi Maalum.
ACT Wazalendo
11 Mei, 2022.

IMG-20220511-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom