Viongozi vijana waonywa ujuaji

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
katiubi.jpg

Serikali imewataka viongozi vijana kuacha tabia ya kujiona kila kitu wanakijua katika ofisi, hivyo kuharibu taasisi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Dk. Laurean Ndumbaro, wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya uongozi ngazi ya cheti yanayotolewa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Aalto Executive Education cha Finland.

Alisema viongozi hao waache tabia ya kujiona wanaelewa, badala yake wajishushe ili waweze kupatiwa ushauri.

"Hii ni changamoto, lazima ujishushe ili uende na wananchi mfano, viongozi wengi vijana wameteuliwa, kuna taasisi moja inaongozwa na vijana na wasaidizi wake ni vijana, lakini anashangaa kwa nini yeye haeleweki kwa wenzake wanamshangaa kwa nini haeleweki."

Aliongeza: "Kumekuwa na mgogoro katika hii ofisi na watumishi wengi wanaingia na kutoka kwa sababu ni yeye anajiona anaelewa kila kitu… huko sio kujiamini ni kuharibu, ukiwa kama kiongozi unatakiwa kuliangalia hilo kwa kuwa tabia hiyo huwafanya baadhi ya watu kushindwa kukushauri.”

Alisema kiongozi mzuri anapaswa kujishusha na muda wote awe mtu wa kujifunza ili iwe rahisi watu wengine kufika ofisini kwake na kumshauri.

Dk. Ndumbaro alisema kiongozi anapaswa kujiamini kwa kutambua changamoto zilizopo, ambazo zinazunguka jamii ambayo anaiongoza badala ya kujifanya ni mjuaji wa kila kitu.

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Penina Mlama, alisema bado nchi inakabiliwa na changamoto ya wanawake kushika nafasi za chini za uongozi, hivyo ni wajibu wa vijana kushirikiana kuhakikisha wanatatua tatizo hilo.

"Tutaweza kulitatua jambo hilo kama wanawake waliopata nafasi za uongozi watatoa fursa kwa wenzao ili kuwapo na uwiano sawa,” alisema.

Awali akifungua mafunzo hayo, Katibu Mkuu Ikulu, Dk. Moses Kusiluka, alisema programu hiyo ni ishara ya kuunga juhudi za maendeleo nchini na kuimarisha uwezo wa viongozi inayofanywa na Taasisi ya Uongozi kuimarisha utawala bora.

"Nimefahamishwa kwamba programu za mafunzo kwa viongozi zinazoandaliwa na kutolewa na Taasisi ya Uongozi zinalenga kuimarisha uwezo wa viongozi katika maeneo matatu:

Kufanya maamuzi ya kimkakati, kuongoza rasilimali watu na rasilimali nyingine na kujenga sifa binafsi za kiongozi,” alisema.

Naye Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo, alisema mafunzo hayo ni programu ya miezi sita yenye moduli tatu na yanawalenga viongozi chipukizi na waandamizi wanaofanya kazi katika taasisi mbalimbali barani Afrika.

"Programu hii inatoa fursa kwa viongozi hususan wanawake ya kurudi nyenzo mpya za kiuongozi, kupata mbinu za uongozi wa kimkakati na kuwa mawakala wa mabadiliko," alisema Singo.

Aidha, alisema asilimia 54 ya washiriki waliopo kwenye programu hiyo ni wanawake waliopo katika ngazi mbalimbali za utawala na uongozi na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatatolewa kwa njia ya mtandao.

Chanzo: NIPASHE
 
Kijana ni yule aliye na umri kati ya miaka 18 mpaka 35 kulingana na sera ya vijana ya Tanzania. Nimekumbusha tu.
 
Hata wazee, tena kuna wengine wameshatufokea kuwa hawashauriki.
 
Hasa awamu hii yani umri ni kitu muhimu MTU anaokotwa kwakua ni mwanaccm age 30s hana uzoefu anakua RC. Huu ni mzaha kabisa. Jiulizeni Mwal Nyerere alikua anawapataje Wakuu wa mikoa na wilaya. Siku hizi alikua anafanyaje vetting? Siku hizi foji cheti kisha mtukane Mbowe lazima uwe mkuu wa mkoa au wilaya?

Eti mheshimiwa anapiga cm kwenye TV station anasema "huyo mweupe huyoo nampa cheo" hahaaahaa aiseee!!!
Ukiwa mtangazaji wewe sifia tuuu unapewa UDAs? Ajabu kabisa
 
Back
Top Bottom