Viongozi TAMISEMI hawawaogopi wananchi ndio sababu ya kukithiri kwa ufisadi kila ripoti ya CAG. Tatizo ni mfumo

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,471
46,002
Kila mwaka CAG hutoa ripoti yake ya ukaguzi wa fedha za umma ambayo huwa inaonyesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma katika maeneo mbalimbali hasa TAMISEMI.Kuna taarifa za kufedhesha sana jinsi pesa za walipakodi zinavyokwapuliwa huko huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa huduma mbovu za kijamii.

Tayari wananchi wa Tanzania kama kawaida yao kwa mambo mengi "serious" wameshaizoea ripoti hiyo ya CAG kuja hivyo kila mwaka na sasa jambo la kuhuzunisha zaidi wameamua kuzifanyia taarifa hizo za ubadhirifu comedy na memes tu huku wakifarajiana kwa machozi ya samaki.

Hali hii ya ubadhirifu mkubwa wa fedha za serikali haitabadilika kama mfumo wa utawala na jinsi watawala wanavyopatikana hautabadilika.

Kama Wakuu wa mikoa, wilaya, DED, RAS, DAS, Wakuregenzi wa TRA, TANROADS, TARURA, TANESCO, Idara za Maji n.k wataendelea kuwa wateuliwa wa Rais au mawaziri badala ya kuchaguliwa kwa kupigiwa kura, kuajiriwa kwa usahili wa wazi na tume maalum za kuajiri au bodi za mashirika basi ufisadi inabidi tukubali ufisadi tutaishi nao siku zote.

Watu wanaoteuliwa mara zote kujali kwao, wajibu wao wa kwanza na hofu ni kwa yule anayewateua. Jambo lingine sio rahisi mteuaji kuweza kuwafuatilia kwa karibu watu wote anaowateua hasa kwa nchi kubwa kama Tanzania.

Nchi hii iliniweze kupambana na ufisadi inahitaji wananchi waweze kuwa ndio wanaochagua wengi wa viongozi wanaosimamia pesa zao na waweze kuwatimua kupitia sanduku huru la kura moja pale ambapo wanakuwa hawabebi maslahi ya raia tena.Hiyo ni kwa ma RC,DC, DED.Na hii ingetakiwa ifanyike kila baada ya miaka mitatu.
 
Back
Top Bottom