Viongozi takriban 10 wa Afrika kuhudhuria maziko ya Mugabe

Ryan Herman

Member
Jul 26, 2019
42
46
Viongozi 10 wa kiafrika wanatarajiwa kuhudhuria shughuli ya maziko ya Rais wa kwanza Zimbabwe Robert Mugabe. Hayo yameelezwa na msemaji mkuu wa Serikali na Mwili wa marehemu ulirudishwa Zimbabwe Jumatano ukitokea Singapore alikofariki akiwa na umri wa miaka 95.

Miongoni mwa viongozi wa Afrika waliothibitisha kushiriki katika shughuli hiyo ni pamoja na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa,Uhuru Kenyatta wa Kenya,na Filipe Nyusi wa Msumbiji.

Marais wastaafu watakaoshiriki ni pamoja na Jacob Zuma wa Afrika Kusini,Kenneth Kaunda wa Zambia na Sam Nujoma wa Namibia.Serikali ya Zimbabwe imesema Mugabe atazikwa katika makaburi ya kijiji cha Kutama,kiasi kilomita 85 kutoka mjini mkuu Harare.Msemaji wa familia ya Mugabe pia amesema maziko yatafanyika wiki ijayo jumatatu au Jumanne.
 
Rais Magufuli yeye haendi? Aliagiza tuweke bendera nusu mlingoti, msiba wa kwetu huu mwambieni aende tafadhali.
 
Rais Magufuli yeye haendi? Aliagiza tuweke bendera nusu mlingoti, msiba wa kwetu huu mwambieni aende tafadhali.

Ataamua yeye, kuamuliwa au kuwakilishwa utapewa taarifa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais,au msemaji wa serikali muda bado
 
Back
Top Bottom